Pages

29 September 2011

WAIMBAJI WA INJILI WAPAA MAREKANI




Katika kile kinachoonyesha kukua kwa Muziki wa Injili, sasa waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili, wamekuwa wakifanya ziara mbalimbali huko ulaya na marekani. Baadhi ya waimbaji walio paa majuu kwa sasa, ni mkongwe wa Muziki wa injili Askofu Jangalason. Wengine ni Upendo kilahiro na upendo nkone, hawa wameda majuzi tu na watafuatiw na Christina shusho.

ALL TANZANIA GOSPEL STARS Warekodi wimbo wa miaka 50 ya uhuru

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, waimbaji wa nyimbo za Injili wameungana kwa pamoja na kurekodi wimbo wa kumshukuru Mungu kwa ajili ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania. Chini ya mwalimu John Shabani na Amoni Kilahiro   waimbaji hao kila mmoja ameingiza ubeti wake. Waimbji Ambao tayari wamshiriki kuingiza suti mpaka sasa ni

1. Gloria kilahiro                                            18. Mzee Makassy
2. Amon Kilahiro                                            19. Mzungu Four
3. Masanja Mkandamizai                                     Jane Misso
4. Upendo kilahiro                                         Addo November
5. Stella Joel                                                  Martha Mlata
6. Nely Nyamanga                                         Ambwene mwasongwe
7. Joyce Ombeni                                           Victor Ahron                                                                             
8.  Bony Mwaitege                                          Douglas Pius
9. John Shabani                                              Mchumu Maximillian
10. Rose Manoza                                              Charles Thobias Malya
11. Yona Abiud                                                  Joshua makondeko
12. Miriam Lukindo Mauki                                  Daniel Safari
13. Robert Bukelebe                                          Naomy Mbwambo
14. Nicholaus Misuzi                                          Joseph kasigala
15. Christina Matai                                             Debora Said
 16. Tina Marego                                               Stara Thomas  
17. Martha Mwaipaja                                       
Wengine kwasababu mbalimbali, wameahidi kushiriki kwenye video inayotegemea kuandaliwa mapema iwezekanavyo. Kazi hii kubwa ya kuwakutanisha  waimbaji wa injili na kurekodi wimbo, imefanyika katika studio za PRO ARTS STUDIOS iliopo mbezi africana Dar es salaam, chini ya Producer TC (Timothy Chilula) Ambaye pia ni miongoni mwa waanzilishi wa wazo hili.

14 September 2011

MAMBO YA MIKOCHENI B ASSEMBLIES OF GOD (MLIMA WA MOTO)

John shabani akiwa amesimama na Dr Getrude Rwakatare. Ni picha ya kikundi cha kinamama (SINGLE LADIES). John ni mwalimu wa kwaya ya kikundi hicho. Pamoja na kikundi hicho, John pia ni mwalimu wa kwaya ya Joybringers na Praise team zote za mlima wa moto.

13 September 2011

JIANDAE KUJIPATIA CD YA DEBORA SHABANI

Baada ya wapenzi wa nyimbo za marehemu Debora shabani kuwa na shauku kubwa ya kupata nyimo zake, sasa tumeamua kukutengenezea cd nzuri ya nyota huyo na baadaye utapata video yake. Mungu wa mbinguni awabariki.