Pages

29 January 2013

NAMSHUKURU MUNGU KWA KUMALIZA MASOMO YANGU KATIKA CHUO CHA KIMATAIFA CHA HUDUMA (INTERNATINAL SCHOOL OF MINISTRY)




Baadhi ya waalimu wa chuo cha ISOM

 Baadhi ya wanafunzi huko Singapore
Baadhi ya wanafunzi huko wingereza - Uk

Baadhi ya wanafunzi huko Marekani 
Kwa neema ya Mungu nimemaliza masomo yangu kwa ngazi ya diploma katika chuo cha kimataifa cha huduma, Graduation ni mwezi tatu mwishoni, nitakapo kualika usisite kuhudhuria. Endelea pia kuniombea kwa ajili ya kuendelea na degree yangu.

Nawewe unayetaka kujiunga na chuo hiki, tayari wamefungua tawi hapa Dar es salaam, bado hujachelewa. Kwa habari kuhusu ISOM (International School of Ministry) tembelea

24 January 2013

JE NYIMBO HIZI ZA MAREHEMU DEBORA SHABANI ZIMEKUWA ZA BARAKA KWAKO? JE UNGEPENDA KUJIPATIA CD HII ILI KUCHANGIA ELIMU YA BINTI YETU? TUWASILIANE BASI NA MUNGU ATAKUBARIK

                                          Mwanadamu anaweza kutoweka, lakini ujumbe wenye uvuvio wa neno la Mungu unadumu milele, amen!

14 January 2013

MTANGAZAJI MAHIRI WA TOP RADIO MOROGORO BI LEVINA STEVEN KUJA KIVINGINE KATIKA MUZIKI WA INJILI, AMSHIRIKISHA MWL JOHN SHABANI


                                      John Shabani akiwa na Bi Levina Steven

Mwana dada Levina Steven anayetangaza Top Radio, amekua gumzo kwa watanzania baada ya kuachia ngoma kadhaa za nyimbo za injili. Chini ya usimamizi wa Mwl John Shabani, Nyimbo zake zinaonekana kufanya vizuri sana. Kabla ya kuhamia morogoro, mtangazaji huyo machachari alikuwa akifanya kazi katika kituo cha Praise Power radio cha jijini Dar es salaam.
Endelea kumuombea.

13 January 2013

MIRACLES WITH BISHOP MABOYA






Sunday 13 jan the lady with bishop maboya crying was healed in the sunday service from a n operation done in september and had alot of pain and purse was coming out was healed instantly and started crying with joy"


This lady is 56years of age had a headache from when she was 15 God healed her completely! On new years service!

 Jesus power sunday service!!




12 January 2013

UJUMBE WA January 2013 na John Shabani




Mfumo wa maisha ya mwanadamu huwa kama unavyoziona picha hizi;
Kuna wakati wa kuonekana umefifia(upo kama haupo), wakati wa mchoro wako wa kimaisha kuanza kuonekana kwa mbali, wakati wa kuonekana katika rangi nyingine, wakati wa rangi yako ya ki uchumi au kiroho n.k  kuanza kuonekana kwa mbali, wakati wa wewe kung’aa katika rangi yako na baadaye kuchanua.
Picha hizo zinaashiria changamoto mbalimbaliza kimaisha, yawe ya kiroho, kia-afya na ki-uchumi. Katika kila changamoto, usiogope, usikiate tamaa bali zione changamoto kama daraja la kuvukia upande wa pili wa mafanikio yako. Kuna wakati wa kudharauliwa,  kuchekwa, kushushwa chini na kuachwa/kutengwa. Lakini wakati wa kung’aa kwako na baadaye kuchanua utafika tu!
MARUFUKU KUKATA TAMAA