Pages

21 May 2013

NGUVU ZA MUNGU ZAENDELEA KUJIDHIHIRISHAKATIKA UKUMBI WA USTAWI WA JAMII SINZA



 Mchungaji Benjamin Bukuku, akiombea watu waliofurika katika ukumbi wa ustawi wa jamii


Mamia ya watu wameendelea kubarikiwa na  mafundisho ya Mch. Benjamin Bukuku  wa huduma yaKWELI ITAKUWEKA HURU”  YOHANA 8:32.
kupitia mafundisho hayo wengi wanafunguliwa. Maombezi kwa wenye shida mbalimbali yanafanyika pia. Bado hujachelewa, karibu jumapili hii. Mahali kwenye ukumbi wa chuo cha ustawi wa jamii Bamaga. saa ni saa 1:00 asubuhi mpaka saa 3:00.asubuhi Najioni saa 10:00mpaka saa 12:30 . waimbaji wengi unaowafahau wamekuwa wakimtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji 
 Mch. Yohana
 Sarah Mvungi
 Madam Ruth

Pia msikilize Mchungaji huyo katika kipindi kinachorushwa katika radio ya Praise power, kila siku ya jumatano saa 4 usiku
 Karibuni sana

13 May 2013

NABII FRORA AWAKUMBUKA VIJANA NA MABINTI, AWAOMBEA BARAKA ZA KUOA NA KUOLEWA



 Baadhi ya akina dada wanaombewa kupata wachumba na nabii Flora wakiwa wamejipanga kupokea baraka kutoka kwa Mungu

 Baadhi ya wababa na vijana walijipanga kwaajili ya kupokea upako wa mafanikio ya kibiashara

Hawa ni baadhi ya watu waliodondoshwa kupitia maombi ya Nabii Flora baada ya kutamka Neno la Upako

Nabii Flora

Ilikua ni jumapili ya kipekee katika kanisa linaloongozwa na Nabii Flora, kwani  vijana na mabinti mbalimbali wamepokea maombezi kutoka kwa nabii huyo, ili Mungu awakumbuke kupata wenzi wa maisha.

1 May 2013

DORCUS CHRISTIAN MINISTRY YADHAMIRIA KUFUNGUA MATAWI ZAIDI NDANI NA NJE YA NCHI

 Maefu ya wahumini wa tawi la Dorcus Christian ministrie wakimsikila Askofu Jane Muhegi

Askofu Jane katika picha



Dorcus Christian Ministries ni huduma inayoongozwa na  Askofu Jane Muhegi. Huduma hiyo yenye makao makuu maeneo ya Kunduchi Beach Dar es salaam Tanzania, imekuwa ikiandaa mikutano na makongamano makubwa ya kiroho. Tayari huduma hiyo imefungua matawi katika nchi kadhaa barani Afrika. Pamoja na huduma za kiroho pia wanacho kituo kikubwa kwa ajili ya watoto yatima pamoja na wazee.



Tutaendelea kukujulisha zaidi kuhusu huduma hii.