Pages

29 September 2014

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI ALIYEVAA MADHABAHUNI VAZI LA UFUKWENI AKERA WENGI



Huyu ni muimbaji wa kike wa nyimbo za injili ambae yuko nchini Marekani. Na katika mkesha mmoja nchini humo alipanda kuhudumu akiwa amevaa mavazi haya, jambo ambalo liliwashangaza hata baadhi ya wamarekani.
Naamini kabisa hata kufikia maamuzi ya kuvaa hivi ana sababu zake binafsi na pia hata maandiko ya kujitetea anayo, na andiko ambalo wanapenda kulitumia hata watumishi wa type ya huyu mama ni Mungu anaangalia moyo haangalii mavazi, lakini wanasahau kabisa lile andiko linalosema makwazo hayana budi kuja, na ole wake yule ayaletae.
Andiko lingine wanalopenda kujifichia ni lile ambalo Paulo anasema kwa Warumi alikuwa kama Mrumi ili awapate warumi. Huku wakisahau kuwa kanisani sio kwa Warumi hivyo unatakiwa uwe kama mtumishi ili injili yako isipate kikwazo. Maana huwezi kuvaa vazi la kikahaba na kuanza kutabiri alafu watu wakaupokea ujumbe wako kwa amani, lazima watazaa maswali wmbayo majibu yao yatafanya wakukatae wewe na ujumbe wako hata kama ni mzuri kiasi gani.
Ushauri wangu kwenu ndugu zangu dada zangu wa type hii, msibebe biashara ile na kuinadi kwa njia ya bible alafu mkazuga kuwa mmechanganywa na utamu wa Yesu.
Huo ni ushauri wangu kwenu na pia ni mawazo yangu.
Ewe Mtume, Nabii, Mchungaji, Muinjilisti, Mwalimu, Askofu,Mzee, Shemasi, hata muumini wa kawaida kemea tabia na uvaaji kama huu maana hizi ni hila za shetani ndani ya kanisa. Maana kitendo cha mtu kuvaa kihuni alafu ukampa madhabahu, hata wanaokutazama watahisi na wewe una hitirafu kichwani ndio maana unakubaliana na uhuni.


Habari kutoka Mr Bashando

10 September 2014

HATIMAYE JOHN SHABANI ATEMBELEA OFISI ZA BBC AKABIDHI WIMBO WA EBOLA



                      John Shabani akifanya mahojiano na mtangazaji wa bbc, bwana John Solombi


John shabani akikabidhi CD 
 
Baada ya mchakato wa takribani miezi miwili ya kuandaa wimbo unaoelezea janga la Ebola, hatimaye mwalimu maaarufu wa muziki wa injili Afrika mashariki akishirikiana na waimbaji mbalimbali amekalisha wimbo huo na kuanza kuhusambaza katika vyombo mbalimbali vya habari.

Wimbo huo unaelezea chanzo cha gonjwa la Ebola, namna unavyoenea, na jinsi ya kujikinga. Imechukua muda kidogo kuandaa wimbo huo, kwani ilihitajika ushirikishwaji wa baadhi ya madaktari na watafiti wa gonjwa hilo. Hata hivyo baada ya kupokelewa ofisi hizo za kituo cha kimataifa cha BBC, John Amepongezwa kwa kuwa msanii wa kwanza duniani kujitolea kurekodi wimbo wa Janga hilo lililogusa dunia.

Pamoja na wimbo wa janga la Ebola, pia John amekabidhi wimbo unaotetea haki za watoto na wanawake. Mmoja kati ya maripota wa bbc bwana John Solombi, ameweza kufanya mahojiano ya kina na John Shabani na kuahidi kupanga muda mzuri zaidi wa mahojiano.

Kwa pamoja tuseme hapana kwa Ebola.

6 September 2014

HATIMAYE MWANADADA ALINE VYUKA AKAMILISHA ALBAM YAKE MPYA

Ilikuwa si kazi rahisi!
Kwa muda mfupi sana mwanadada Aline vyuka chini wa usimamizi wa mwalimu John Shabani, ameweza kukamilisha Albam yake mpya ya nyimbo za Injili kwa nfumo wa Audio na Video.

Mwimbaji huyo anayeishi nchini Marekani, pamoja na shughuli nyingi zinazomkabili pia ikizingatiwa bado anaendelea na masomo yake, lakini kwa ajili ya mzigo wa kumtumikia Bwana, alifunga safari hadi Tanzania na kufanikiwa kurekodi Albam hiyo ilibeba jina "NI SALAMA".
 Ndani ya Shilo Studio - Boko Dar es salaam

 Akiredi mkanda wa video

Mwonekano wa kazi yake mpya

Unaweza kumuunga mkono Aline kwa kunua  nakala za kazi zake. Kwa habari zaidi tembelea ukurasa wa facebook wa Aline Vyuka, au wasiliana na Emmanuel Mabisa au pia wawezatembelea ofisi za Rumaafrika - Dar es salaam.

Kila la heri Aline