Pages

16 October 2015

TUNAKULETEA KIFAA KINACHOTIBU MAGONJWA MENGI TENA KWA HARAKA SANA



 Ni kifaa kinachotibu zaidi ya magonjwa 50. Mamia ya watu waliokuwa wamekata tamaa 
ya kutopona magonjwa yao, sasa niwazima kabisa.








Ni kifaa kinachotumika kwa kulalia kama kitanda, ambacho ndani yake mna kifaa kidogo ambacho hutoa joto kuanzia chini ya makalio hadi shingoni. Kimeundwa kwa kutumia madini aina nne ambayo huleta mabadiliko mwilini haraka sana.
Kinatibu magonjwa kama; Shinikizo la damu, kupooza mwili, kisukari,vidonda vya tumbo, matatizo ya hedhi, uzazi na ugumba, maumivu ya vifundo, ganzi aina zote, aina mbalimbali za uvimbe na saratani, maumivu ya miguu, kupooza kwa mishipa ya fahamu, aleji yangozi na pumu, kupunguza moyo uliovimba n.k

Pia tunavyo vifaa vingine kama kile kinachosaidia kusukuma damu kwa kasi sana mwilini kwa kupitia mfumo maalum wa nerves zinazopatikana miguuni, hivyo kusaidia kurekebisha mfumo mzima wa mwili katika utendaji kazi na kuufanya mwili wako kuwa na nguvu pamoja na ubongo kuwa active. Pia hufanya massage ya mwili mzima(Whole Body Vibration Fitness Massager with Handles) na kupunguza mafuta ya ziada mwilini pamoja na kutibu magonjwa ya aina mbalimbali.
Inawezekana kabisa kwa kupitia vifaa tulivyonavyo, ukawa mzima bila kutumia kidonge wala sindano. Waambie ndugu, jamaa na marafiki.
Kituo kimefunguliwa kinondoni.
Tuwasiliane 0713778778

7 October 2015

YOU MUST NEVER FORGET WHO WAS THERE FOR YOU WHEN NOBODY ELSE WAS!

 John Shabani na Alex Msama wakiwa katika picha ya pamoja, baada ya kutambulishwa kama watendaji wa kampuni ya Msama Promotions, ni katika tamasha lililo andaliwa na kampuni ya hiyo miaka kadhaa iliyopita.

 John Shabani akiwajibika ofisini



Nimekumbuka miaka kadhaa iliyopita tangu mwaka 2004 nikifanya kazi kama msaidizi wa Msama na baadaye nikiwa kama mtaalam na mwalimu wa nyimbo za injili nikiwashauri waimbaji na kuakiki kazi za waimbaji waliokuwa wakizileta katika kampuni ya Msama Promotions.

Nimekumbuka tukiwa kwenye chumba kimoja pale mwananyamala na baadaye kuhamia kinondoni, nimekumbuka wakati ambao nilitembea kwa mguu nikitokea ofisini baada ya kutokuwa na nauli ya kurudi nyumbani na wakati mwingine nililazimika kulala ofisini bila kumwambia mkurugenzi wangu kwani hali ya kifedha ilikuwa mbaya, nimekumbuka wakati nilipobaki ofisini peke yangu wakati wafanya kazi wengine wakishindwa kuvumilia pale ambapo hali ya mshahara haikuwa vizuri, kuna wakati nilifanya kazi kama msaidizi, wakati mwingine kama katibu, wakati mwingine kama mratibu wa masuala Fulani ya kiofini; 
na leo hii Msama Promotions imekuwa ni moja ya makapuni makubwa inayoweza kuandaa matamasha makubwa yanayohudhuriwa na maelfu ya watu.

Ujumbe wangu kwako:
“USIMSAHAU  YULE ALIYESIMAMA NA WEWE KATIKA MWANZO WAKO MDOGO”