Pages

28 September 2016

JIFUNZE AINA NNE ZA MARAFIKI


(Rafiki mzuri atakufanya uwe na furaha, tabasamu na kicheko)

Nilipokua nikijifunza somo la saikolojia hasa kwa habari za mahusiano, somo hili lilinisaidia sana kujihepusha na marafiki wasikua na tija katika maisha yangu. Acha nikusaidie pia;
UTANGULIZI
Katika lugha ya kingereza kuna Mithali moja inasema “A Friend in need is a friend indeed” kwa maana ya“Rafiki anayakutafuta ndiye rafiki wa kweli.Ni dhahiri kwamba hapa duniani kuna marafiki wa aina tofauti tofauti wakiwemo wenye nia njema na wenye nia mbaya.
Huyu anayezungumzwa hapo juu ni aina mojawapo ya rafiki mwenye upendo wa dhati na anayejali,kuthamini na kumpa furaha na amani mtu yule anayemtafuta.Mwandishi wa mashairi mmoja aliandika kwamba “Niambie nani rafiki yako nami nitakuambia wewe ni mtu wa aina gani.”Kwa mantiki kwamba rafiki wa mtu ana uwezo mkubwa sana wa kumusaidia mtu husika au kumpotosha kabisa katika njia isiyo salama.
Katika maisha ya kawaida ,ni muhimu sana kutambua na kuelewa kwa kina marafiki uliyonao kwa sababu wanaweza kuyajenga au kuyaathiri maisha yako kwa kiwango kikubwa sana.Hivyo basi ni vema ukagundua vigezo vinavyoashiria aina tofauti tofauti za marafiki ili uweze kubaini marafiki watakaoweza kukusaidia maishani na wale watakaoweza kukuharibia maisha yako .
Kwa kukosa kuyafahamu haya ,watu wengi wameumizwa na kujutia maisha yao baada ya kutendwa na wale waliodhania kuwa ni watu wao wa karibu kumbe walikuwa siyo watu wazuri
Kuna aina nne za Marafiki kama ifuatavyo:
1. Rafiki wa Kweli (Intimate Friend,Real Friend)
2. Rafiki Mnafiki (Hypocritic Friend)
3. Rafiki Mnyonyaji (Absorbant Friend)
4. Rafiki Mpoteza muda (Time loser Friend)
Ebu nikudadavulie rafiki mmoja baada ya mwingine :
1. RAFIKI WA KWELI: (INTIMATE FRIEND)
Ni Yule :
• Anayekujali kwa kila hali,
• Anayekujulia hali muda mwingi,
• Anakuthamini ,
• Anakuonyesha upendo wa dhati kwa vitendo si kwa maneno tu,
• Anakutafuta kwa hiari yake mwenyewe bila kushinikizwa na mtu
• Anakushirikisha mambo yake
• Ni mkweli na mwaminifu kwako
• Anatafuta mbinu za kukufanya ufurahi,utabasamu,ucheke na uwe na amani.
• Ndiye mfariji na mdhamini wako wa kwanza unapopatwa na magumu.
• Anakuamini katika mengi unayomwambia
• Muda mwingi anapenda kuwa na wewe,kutembea na wewe,kula na wewe nk..
• Mnapokuwa pamoja anaona fahari ya kuwa na wewe na hata anasahau ratiba zake zingine alizo nazo
• Anakuheshimu na kuheshimu mawazo ,maoni na mapendekezo yako.
• Hana maswali ya kimtego-mtego wala ya kijinga maana anahofia kukupoteza .Daima maswali yake yana msingi wa kujenga mahusiano yenu.
• Hataki kukuona ukinuna wala ukikwazika,
• Hawezi kukusema vibaya na Hataki kusikia ukisemwa na watu vibaya hata kidogo badala yake anakutetea
• Ni mwaminifu katika mambo yote
• Furaha yake ni kukuona:
 Umechangamka
 Una amani,
 Umefanikiwa
 Umestawi
 Umekua na afya njema
 Umefaulu
 Mambo yako yanakwenda vizuri
 Umefarijika
 Umeinuka
• Ni mstarabu ,mpole,muelewa na mtii kwako pia anaelewa hali ya mambo ilivyo pindi unapomuelekeza
• Siku zote anatafuta maslahi ya ninyi wote (wewe na yeye) ,
• Akiwa nacho anakukumbuka,asipokuwa nacho anakupa taarifa
• Ni mwepesi wa kukuomba msamaha,
• Anakuomba ushauri,
• Mara zote anakupa nafasi ya kutoa mapendekezo,mawazo na maoni yako kuhusu jambo lolote linalowahusu.
• Mnapopishana kwa jambo lolote anajitahidi kutafuta suluhu haraka iwezekanavyo ili myamalize.
2. RAFIKI MNAFIKI (HYPOCRYTIC FRIEND):
Ni Yule:
 Anayejidai kukupenda anapokuona lakini mnapoachana anakusahau kabisa
 Usipombipu,kumtumia meseji au kumpigia simu,hawezi kukujulia hali.
Anakupigia simu pindi anapokuwa na shida na wewe au anapohitaji faraja kutoka kwako.
 Anakuinjoyi mara nyingi na kujidai kukupenda kwa dhati pasipo kuwa na ukweli wowote.
 Ana maneno mengi ya udanganyifu
 Ni mtoa ahadi nyingi asizotekeleza
 Hana upendo wa dhati na wewe hata kidogo
 Anakusengenya ,kukushusha hadhi na kukubeza anapokuwa na watu wengine
 Anatangaza habari na taarifa zako nzuri na mbaya kwa wengine kwa lengo la kukuharibia sifa.
 Anakudadisi sana na kujiweka karibu na wewe ili apate maneno ya kukuchafulia jina.
 Hapendi mafanikio yako
 Siyo mwaminifu hata kidogo
 Hataki uwe na kitu chochote kinachomzidi yeye .
 Anatafuta visingizo kutafuta namna ya kukuacha.
3. RAFIKI MNYONYAJI (ABSORBANT FRIEND):
Ni Yule:
 Anatafuta faida kutoka kwako,anahitaji kunufaika kupitia wewe kwa namna moja ama nyingine .
 Ana agenda ya siri kuhusu wewe siri ya kukunyonya.
 Anakuweka karibu sana ili umpe kile anachohitaji:
o Mfano: PESA, MWILI WAKO, KUJIPATIA AJIRA kupitia wewe , MALI ya aina FULANI,….. akishafanikiwa kupata kile alichokuwa anawinda kwako basi anakupiga chini,anakusahau kabisa wala hataki kukuona na anabadili hata namba za simu .
 Si mwepesi kukuomba msamaha anapokukosea baada ya kupata kile alichokuwa anahitaji.
Hakubembelezi hata kidogo baada ya kupata alicholenga kwako.Hata anakuwa mkali kwako.
o Msimamo wake siku zote ni “POTELEA MBALI”
 Mara zote anakuwekea masharti yatakayomfanya afanikiwe kupata anachokitafuta kwako.
 Anapotaka kukuacha anatafuta sababu isiyo ya msingi yaani kisingizio
 Anapenda sana kuchunguza mambo yako .
 Haoni aibu kukuomba vitu mbalimbali kama vile Pesa , Mali, Mwili wako nk…
4. RAFIKI MPOTEZA MUDA (TIMELOSER FRIEND ):
Ni Yule:
o Anatoa ahadi kibao kwa asilimia kubwa sana lakini hatekelezi
o Anakukatisha tamaa unapotaka kufanya jambo linaloleta maendeleo
o Hakutii moyo hata siku moja.
o Anakuthibitishia kwamba huwezi kabisa kufanya kama wengine wanavyofanya.
o Anakucheleweshea mipango na ratiba zako
o Kwenye mahusiano anakuahidi kuwa mko pamoja sana lakini anakupotezea muda tena kwa makusudi
o Ana wivu wa kijinga jinga usiyokuwa na sababu za msingi
o Anakuvurugia mipango na ratiba zako
o Anakuwekea masharti mengi katika ushirikiano wenu
o Anajali maslahi yake binafsi ,haangalii maslahi yako.
o Amejaa maeneno ya uwongo na udanganyifu
o Ana mizaha mingi sana ,hana hekima wala busara.
o Haoni fursa,hajishughulishi kwa mambo yanayowahusu.
o Hana maono wala mipango inayohusu maendeleo yenu na hatima yenu baadaye.
o Anakuongezea msongo wa mawazo siku hadi siku kwa maneno yasiyokuwa ya kukujenga.
o Katika mahusiano haongei mambo ya msingi hana pointi zenye misingi.
o Anapenda mpoteze muda mwingi kwenye vitu visivyokuwa na tija kama vile starehe, michezo na burudani nk….
Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana namimi kwenye simu yangu au ukatembelea kituo chetu.
Nakupenda.

16 September 2016

VIDEO MPYA YA MWALIMU JOHN SHABANI




Kaa tayari kuabudu na mwalimu wa nyimbo za injili Afrika Mashariki, John Shabani akishirikiana na mwimbaji wa kimataifa Georgina Ngatunga.

Ni CD na DVD itakayoponya maisha yako, itakayo burudisha moyo wako na kukusogeza kwenye ibada.

ONDOA WASIWASI, PALE ULIPOSHINDWA ANZA UPYA, PALE ULIPOLIZWA FUTA MACHOZI, PALE ULIPOCHAFUKA SAFISHA UPYA, MAISHA YANAENDELEA



Nimeweka picha hii ya rafiki yangu na dada yangu katika Bwana maana ni mtu mwenye ushuhuda mkubwa lakini hakati tamaa. Nimejifunza mengi kutoka kwa dada huyu.

Nianze kwa kusema kwa mfano huu;
Mwanamke mmoja ambaye baada ya kufiwa na mume wake, alianza kujiona mpweke na kuvunjika moyo. Siku moja alipokuwa akitoka shuleni alikokuwa akifundisha, alianza kufikiri na kujisemea moyoni mwake kuwa shule aliyopo ni ya kimaskini, pia barabara anayopita wakati wa kwenda na kurudi nyumbani kwake ni mbaya, hivyo aliamua kuchukua uamuzi wa kujinyonga.
Alifikia hatua hiyo baada ya kuona kila kitu kwake hakiwezekani. “Sioni faida ya kuishi. Ninaamka kila asubuhi, kukabiliana na maisha. Nina hofu ya kila kitu, hofu ya kutokumpata tena mtu sahihi wakunioa, hofu ya kutoweza kumudu kuliendesha gari langu, hofu ya kushindwa kulipa kodi ya nyumba, hofu ya kutokuwa na chakula cha kutosha. Nina hofu ya afya yangu nami sina fedha ya kumwona daktari.
"Yote hayo yalimfanya kufikiria kujinyonga. Siku moja alisoma kifungu kimoja kilichomuinua kutoka katika ile hali iliyokuwa inamkabili na kumpa moyo wa kuendelea kuishi. Kifungu alichosoma kilisema: "Kila siku ni maisha mapya kwa mtu mwenye busara."
Alikiandika kifungu kile na kukibandika kwenye kioo cha gari yake alipoweza kukiona kila mara alipokuwa akiendesha.
Aligundua kuwa kuishi si jambo gumu kama alivyofikiria awali, alijifunza kusahau yaliyopita na kutokufikiria mambo ya kesho. Kila siku alijisemea moyoni mwake kuwa, ‘leo ni siku mpya’.
Alifanikiwa kuishinda hofu iliyokuwa ikimkabili ya upweke aliyojitakia. Tangu hapo akawa mtu wa furaha, mwenye mafanikio na anayependa kuishi.
Kuanzia hapo alisema kuwa hataogopa tena, bila kujali maisha yatakuwa ya aina gani kwake. Aligundua kuwa hataogopa maisha yajayo na ndiyo maana kila siku ni mpya kwa mtu mwenye busara.

JINSI YA KUONDOA WASIWASI
Kumbuka kuwa hali ya wasiwasi inakuondolea uwezo wa kufikiri. Kwani unapokuwa na hofu akili yako 'inaruka' na kufikiri hapa na kule na kila mahali, na unapoteza nguvu yote ya maamuzi. Hata hivyo, wakati unapojilazimisha kufikiria jambo linalokufanya upatwe na hali hiyo na kuikubali katika akili yako, unaiweka katika kupata muafaka wa jambo linalokukwaza.
Unapokuwa na wasiwasi unaweza kupata vidonda vya tumbo, pia uzito wako unaweza kupungua ghafla pamoja na kupata maradhi mbalimbali. Ili kuondokana na hali hiyo, inakupasa kuacha kufikiria na kujipa ujasiri katika kila jambo unalolifanya, pamoja na kuamua kufanikisha mipango yako ya baadaye. Pia unaposafiri maeneo mbalimbali inakusaidia kukutana na watu tofauti na kupata mawazo mapya ya maisha hivyo kujikuta unaondokana na hali uliyokuwa nayo.
“Hofu inasababisha wasiwasi. Pia wasiwasi huo, unakufanya uwe katika hali ya kutotulia na ya fadhaa, huathiri misuli ya tumbo lako, hubadili tumbo lako kutoka katika hali ya kawaida, ambayo mara nyingi huchangia kupata vidonda vya tumbo,”.
Naye Dk. Joseph Montague anasema huwezi kupata vidonda vya tumbo kutoka kwenye kile ulacho, bali unapata vidonda hivyo kutoka kwa kile kinachokutafuna.
Hofu, wasiwasi, chuki, ubinafsi na kutokuwa na uwezo wa kukabiliana na ukweli wa mambo katika ulimwengu huu, ni sababu kubwa za maumivu ya tumbo, pamoja na vidonda…vidonda vya tumbo vinaweza kukuua. Pia utafiti uliofanywa umebaini kuwa wafanyabiashara wengi ambao hawajafikisha miaka 45 hupatwa na magonjwa ya moyo, vidonda vya tumbo na shinikizo la damu, kutokana na kuishi maisha ya wasiwasi. Mtu anaweza kupata mafanikio katika biashara yake na kujisababishia matatizo makubwa ya afya yake. Itamsaidia nini kupata ulimwengu wote kwa utajiri na kupoteza afya yake? Hata kama amekuwa tajiri wa dunia inambidi alale katika kitanda kimoja kwa wakati na kula mlo mara tatu kwa siku, siyo kujishughulisha kupita kiasi na kusahau muda wake wa kula, pamoja na kulala.
Zaidi ya nusu ya wagonjwa wanaolazwa hospitalini huwa na matatizo yaliyosababishwa na hofu, wasiwasi, mshtuko, dukuduku na hali ya kutofanya lolote la maana. Mtu mmoja alisema kuwa kosa linalofanywa na wataalamu wanakuwa wanajitahidi kuponya mwili, badala ya kuangalia chanzo cha tatizo na kukishughulikia. Ingawa mwili na ufahamu ni mmoja na hautakiwi kutenganishwa.
Wasiwasi unaweza kukuweka kwenye kiti cha walemavu kutokana na ugonjwa wa viungo na ugonjwa wa baridi yabisi. Dk. Russell Cecil ameorodhesha vitu vinne vinavyochangia ugonjwa wa baridi yabisi kuwa ni: kuvunjika kwa ndoa, majanga ya kutokuwa na fedha pamoja na huzuni, upweke na wasiwasi pamoja na hali ya kutaka kupata faraja kuchukua muda mrefu tofauti na matarajio.

Asante kwa kusoma ujumbe huu. Kwa ushauri zaidi tembelea kituo chetu cha ushauri kilichopo Ukonga. Lakini pia utakua ukinisikia hivi karibuni kupitia Sibuka Fm.
Pia unaweza ukarekodi tatizo lako kwa ufupi ukanitumia kwenye namba yangu ya whatsap 0716560094, nitakusaidia.