HISTORIA YA YAHANA MARIA MUZEEYI
Sambamba na mahadhimisho ya miaka 150 ya uinjilishaji Kanisa Katoliki Tanzania Bara, pia tunayo kumbukumbu muhimu sana ya Mtakatifu YOHANA MARIA MUZEEYI.
Sambamba na mahadhimisho ya miaka 150 ya uinjilishaji Kanisa Katoliki Tanzania Bara, pia tunayo kumbukumbu muhimu sana ya Mtakatifu YOHANA MARIA MUZEEYI.
Ni mmojawapo wa mashaidi 22 wa Uganda waliotangazwa rasmi na Papa Paulo VI tarehe 18 Octoba mwaka 1964 katika Mtagubo wa pili wa Vatikano kama watakatifu wa Kanisa
Kwa ufupi ni Mtanzania aliyefia Uganda hivyo waganda wanadai alizaliwa mpakani mwa Tanzania na Uganda Kaunti ya Buddu.
Mtakatifu Yahana Maria Muzeeyi ni mtoto wa Bahinda, amezaliwa katika kitongoji cha Kyanumbu, kijiji cha Kigazi kata ya Minziro wilaya ya Misenyi mkoa wa Kagera. Mahali hapo Minziro kuna kituo cha kitaifa cha Hija kinaitwa Kishomberwa, ni kituo cha Yohana Maria Mzeeyi na parokia ya Minziro inayoitwa jina hilohilo la Yohana Maria Mzeeyi.
Waumini wa dini ya kikirito (RC) kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera na Nje ya nchi walishiriki Missa ya Hija takatifu katika eneo la Kishomberwa,Minziro wilaya ya Missenyi. Hija hiyo iliongozwa na Askofu mkuu wa jimbo katoriki la Bukoba Desderius Rwoma (Pichani).
Ujumbe mkuu wa siku hiyo ya hija iliyofanyika jumapili ya Januari 27,2015 ni "tuombe Amani kwa ajili ya Taifa letu"
Askofu Rwoma akiwakumbusha waamini kuwa Yohana Maria Muzeeyi, Shahidi ndiye Mtakatifu Mtanzania wa kwanza kutangazwa rasmi mjini Roma Italy na Baba mtakatifu Paulo VI tarehe 18th October 1964 kati ya mashahidi 21 waliotangazwa wakati huo. 27 January 2015
Ni sehemu iliozungukwa na Mto Kagera. Pia mahali hapo pamezungukwa na msitu mkubwa wenye ndege, wanyama na vivutio mbalimbali vya kitalii. Jambo lingine ni kwamba upo mlima Kabale ambapo hadi leo hii utalikuta jiwe ambalo Yohana Maria Mzeeyi alikuwa akicheza bao.
Hivyo mahali hapo ni sehemu muhimu kwa utalii wa Kidini na wa kiasili. Mamia kwa maelfu ya watu wamekuwa wakifika mahali hapo kuhiji
Kwa uthibitisho wa haya yote basi vipo
vitukuu vya Mt. Yohana Maria Muzeeyi vipo na wanafafanya mambo mengi muhimu tu kwa jamii, na hii ni kutokana na asili na baraka za Mungu kwa kupitia Mtakatifu huyo.
Chakujivunia ni kwamba, huyu ndiye Mtakatifu Mtanzania aliyetangazwa rasmi kuwa mtakatifu na kanisa, hivyo ana maana kubwa sana kwa watanzania, kwa wakatoloki wote duniani na kwa kila binadamu. Hija hufanyika kila ifikapo tarehe 27 January. Hivyo basi nivizuri tukamtangaza, tukamuenzi, tukamuiga, Mungu mwenyewe alimuinua akawa mtakatifu katika maisha yetu. Wapo pia watakatifu wengine kwenye mchakato wa kutangazwa akiwemo mwalimu kambarage Nyerere na sister Mbawala.
HITIMISHO
Tumshukuru Mungu kwa kutujalia Mtakatifu Yohana Maria Muzeeyi, mmoja wa mashahidi ishirini na wawili wa Uganda. Ndiye Mtakatifu wa kwanza Mtanzania.
Ili kuelewa mazingira alimozaliwa, kukulia, kupata imani na hatimaye kufia ushahidi, tukumbuke kuwa zilikuwa nyakati za mataifa ya Ulaya kuvamia Afrika ili kujipatia nafasi za kufanyia biashara. Uvamizi huu ulijulikana kihistoria kama "Scamble and Partition of Africa." Katika mkutano wa nchi za Ulaya uliofanyika mjini Berlini, Ujerumani, Desemba 1884-1885, "Uvamizi wa Afrika" ulihalalishwa na kurasimishwa.
Tanganyika iliangukia kuwa chini ya himaya ya Wajerumani na Uganda chini ya himaya ya Waingereza. Lakini mipaka kati ya nchi hizi mbili haikuwa wazi na ya uhakika kama ilivyo saasa.
Mipaka ya tawala za jadi ilifuata vitenganishi asilia kama vile mito, misitu, mabonde, maziwa na milima. Hivyo, himaya ya Kabaka ilienea kusini hadi mto Kagera kama kitenganishi asilia. Ndiyo maana kata ya Minziro alimozaliwa Yohana Maria muzeeyi ilihesabika kama sehemu ya himaya ya Kabaka.

Mnamo mwaka 1890, mpaka kati ya Uganda, chini ya Waingereza, na Tanganyika chini ya Wajerumani ulisimikwa kufuata nyuzi 1 (1̊) kusini mwa Ikweta. Kwa mantiki hii mahali alipozaliwa Yohane Maria Muzeeyi paliangukia Tanganyika ambayo sasa ni Tanzania, na pamebaki hivyo hadi sasa. Hili ndilo "kosa lenye heri!" Kama si wakoloni kugawa maeneo kwa faida yao ya biashara na kutawala, Yohane Maria Muzeeyi angebaki ni Mtakatifu wa Uganda. Lakini imethibitishwa na Monsinyori Timoteo Ssemogerere aliyekuwa msimamizi wa mchakato wa kuwatangaza mashahidi wa Uganda kuwa watakatifu, kwamba Yohana Maria Muzeeyi alizaliwa Kishomberwa ya Tanzania.
Tunapowaleteeni historia ya Mtakatifu Yohana Maria Muzeeyi, tunapenda kukariri maneno aliyosema Padre Mapeera mara baada ya kuwabatiza wakristo hao shujaa tarehe 1 Novemba 1885 katika sikukuu ya Watakatifu wote, akisema, " Tunahisi kwamba nchi ya Uganda itapata matatizo mengi. Hadi kufikia sikukuu nyingine ya watakatifu wote, baadhi ya Wakristo wapya, atakuwa wamekwisha kumwaga damu yao kwa ajili ya dini zao. Ndio mashahidi wa mbingni watakaopokelewa huko mara moja na watakuwa ni waombezi wetu. Damu yao itamwagwa juu ya ardhi hii ili iweze kuzaa wakristo wengi sana. Yesu kristo atashinda na shetanni atashindwa.Watu wengi sana wataokolewa".
Maisha ya Mtakatifu Yohana Maria Muzeeyi yanaonesha wazi kuwa ushahidi wa kumwaga damu ni kilele tu cha ushahidi wa kuvuja jasho yaani ushahidi wa maisha. Alipambana na matatizo mengi sana dhidi ya imani na maisha safi ya kikristo, hatimaye akawa mshindi hata ilipomdai kutolea maisha yake. Nao utabiri wa Padre Mapeera umetimia, Kristo ameshinda na shetani ameshindwa. Watu wengi sana wanaokolewa. Sisi tulio wazao na warithi wa imani kuu ya Mashahidi wa Uganda, hususan Mt. Yohana Maria Muzeeyi tunayo heshima na wajibu wa kuiga mfano wake. Tumfahamu uli tumuige.
Nawakaribisheni kwenye hija yetu ya kila mwaka Kituoni kishomberwa – Minziro, Jimbo Katoliki la Bukoba.
Yohana Maria Muzeeyi Ndiye Mtanzania Pekee Kutangazwa Mtakatifu
Yohana Maria Muzeeyi Ndiye Mtanzania Pekee Kutangazwa Mtakatifu
Na Askofu Methodius Kilaini (Askofu Msaidizi, Jimbo Katoliki la Bukoba)
Mtakatifu Yohana Maria Muzeeyi ni mmojawapo kati ya Mashahidi ishirini na wawili wa Uganda waliotangazwa rasmi na Papa Paulo VI tarehe 18 Oktoba 1964, katika Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatikano kama watakatifu wa kanisa. Mtakatifu Yohana Maria Muzeeyi ndiye Mtakaifu pekee Mtanzania aliyetangazwa rasmi kuwa Mtakatifu na kanisa na hivyo ana maana kubwa sana kwa Tanzania.
Katika hija ya hapo Namugongo – Kampala, nchini Uganda, mahali ambapo kiongozi wa vijana mashahidi, Kalori Lwanga, aliuawa kwa kuchomwa moto, Mhashamu Askofu Mkuu Cyprian Lwanga wa Jimbo Kuu la Kampala aliwatangazia mahujaji kwamba Yohana Maria Muzeeyi ni shahidi kutoka Tanzania na akamweleza kama kiungo cha damu kati ya Tanzania na Uganda.
Tunamshukuru sana Baba Askofu Nestor Timanywa wa Jimbo la Bukoba ambaye amefanya juhudi nyingi kukiendeleza kituo cha hija cha Kishomberwa alipozaliwa Mtakatifu Yohana Maria Muzeeyi na kufungua parokia mpya ya Minziro ili kukipa umuhimu na uangalizi. Tuna jukumu kubwa la kulinda urithi huu wa kumbukumbu ya shujaa wetu wa imani.

Nachukua fursa hii kumshukuru Padre Thomas Rutashubanyuma ambaye amekamilisha utafiti juu ya shahidi huyu shujaa kiasi kwamba sasa tunamjua zaidi na tunaweza kufuasa katika nyayo zake. Tunawashukuru vilevile kwa kutupa kimaandishi utaratibu wa ibada ya hija inayofanyika kila mwaka katika kituo hiki cha Kishomberwa. Kijitabu hiki kitasaidia sana kumjua Mtakatifu Yohana Maria Muzeeyi, kurahisisha hija katika kituo cha Kishomberwa na kueneza habari zake kwa watu wenye mapenzi mema.
Tukirudia tamko la Baba Askofu Nestor Timanywa, tunawakaribisha waamini wote kutoka sehemu zote za Tanzania, Afrika Mashariki, Afrika na dunia nzima kuja kushuhudia makuu ya Mungu hapa Kishomberwa kupitia kwa shahidi wake, Yohana Maria Muzeeyi wakati wowote lakini hasa Jumapili ya mwisho ya mwezi Januari, ikikumbukwa kwamba alifariki tarehe 27 Januari 1887.
Karibuni tuhiji, karibuni tumuige Mtakatifu huyo karibuni atuombee maisha yetu yawe ya baraka pia ili nasisi tuwezekuwa watakatifu.
Father Faustin Kamugisha
( Paroko wa Parokia ya Minziro)