Pages

13 January 2011

KUSIFU NA KUABUDU




                                     KUSIFU NA KUABUDU
(Zaburi 147:1, 32,:1, 48:1, 96:4, 2nyakati 5:11-14, Yohana 4:20-23)

          Kuabudu ni moja ya sehemu muhimu sana katika huduma, maana kadiri tunapomwabudu Mungu katika roho na kweli ndipo tunapomsogelea Mungu zaidi.

          Inawezekana ikiwepo desturi ya kuimba, kucheza nk. Lakini kuabudu hakuna desturi. Anayestahili kuabudiwa ni Mungu peke yake na wanaostahili kuabudisha ni wale ambao maisha yao yametawaliwa na roho ya kuabudu. Pia ni tofauti au ni zaidi ya wale wanaofanya mazoezi kwa ajili ya kuimba jumapili kanisani.(kuwa na maisha ya kuabudu ni pamioja na kuishi maisha matakatifu).

Tunaweza kuimba kwa kufarijiana, kutiana moyo, kuburudisha n.k lakini siyo suala la kuabudu, Kuabudu kunatoka moyoni, huwezi kuabudu ukiwa mkame.

        Zaburi 100:1-5 (Hii inafahamika kama zaburi ya sifa)
Biblia inasema kelele za shangwe zielekezwe kwa Mungu na sio kwa kanisa au kwa wanadamu. Hizi ni tofauti na kelele zinginezo, ni kelele za shangwe.

        Kuna uponyaji, wokovu, uvuvio nk, katika hali ya kuabudu. Kama mpangilio wa kusifu na kuabudu hauko sawasawa kanisani, ibada nzima huaribika, kunakuwepo na hali ya ukame. Inawezekana  Mchungaji akakosa mpenyo na pi hata baadhi ya watu hujihisi kuchoshwa na kuondoka kabla ya ibada.

         Kama waabudishaji hawana uhusiano na Baba wa mbinguni, hawawezi kuwapeleka watu kwa Baba. Kuabadu kunaweza kushusha nguvu za Mungu kiasi kwamba kisifanyike kitu kingine hadi mwisho wa ibada. Hivyo ni jukumu la waabudishaji, watu wa sifa, waimbaji kuhakikisha watu wamefika katika kilele cha kumwabudu Mungu. Inawezekana wote tukawa waimbaji lakini tunahitaji zaidi waabudishaji.

Pia lazima kuwepo na mawasiliano kati ya mafundi mitambo, viongozi wa sifa, waimbaji wenyewe nk, ili kuepusha mambo madogomadogo yanayoweza kuharibu sifa. Pia kundi nzima la kusifu na kuabudu akiwepo fundi mitambo, lazima wawepo kanisani saa moja kabla ili kuweka mambo sawa na kuanza kuimba nyimbo zitakazo wafanya  watu wanaoingia kuandaliwa mioyo na kusahau mengine yote. Kumbuka sifa ikiharibika na ibada inaharibika.

Unapopata nafasi ya kusimama mbele za watu jione kuwa mwenye mamlaka mbele zao. Lazima wakuamini, wakukubali kwamba wewe ndiwe pekee utakaye wafikisha katika kilele cha kumsifu na kumwabudu Bwana. Tofauti na hapo utaitwa msanii.

Kumbuka ni watu wenye akili zao, wengine wana uwelewa mpaka kuliko hata wewe, wengine wasomi, wenye mamlaka, matajiri nk, lakini wameamua kupondeka na kuimimina mioyo yao mbele za Bwana.

Lazima kuwepo na nidhamu ya utumiaji na utunzaji wa vyombo au vifaa vya sifa au vya muziki. Mtumiaji wa kifaa asipokitunza vizuri, hata maisha yake yataonekana yako hivyohivyo. Vitu vyote vinavyohusika na muziki lazima vihakikishwe kuwa safi.

Kama kuna mtu aliyeteuliwa rasmi kufanya kitu, kama fundi mitambo, mpiga guitar nk, basi huyo anastahili kuheshimiwa. Hata kama ungekuwa na ujuzi zaidi yake, huruhusiwi kujifanya unajua sana na kuparamia mashin, guitar, vipaza sauti au chombo chochote bila utaratibu au ruhusa, maana yapo maandalizi yaliyofanyika kwa ajili ya ratiba ya kusifu na kumwabudu Mungu siku hiyo.

Zaburi 100:4

Neno hili kusifu kwa kiebrania lilikuwa na maana ya;

v  Tehila, yaani kutamka neno kwa kuongeza vionjo na mbwembwe zaidi. Mfano neno haleluya unalitamka (Ha, ha leluya huuu eee) Tehila ni kuwa kama kichaa unaposifu au kuabudu kwa utukufu wa Bwana. (Nilidhani labda hapa ndipo waswahili walipopata neno taahila).

v  Yadaa yaani kujiachia kwa Mungu (you just surrender yourself to the Lord).

v  Barak yaani kusaluti mbele za Bwana. Ni kuonyesha kwamba ni yeye peke yake anayestahili heshima na utukufu. Huwezi kumpigia saluti mtu usiyemwona, hivyo ni kwa njia ya kumwabudu Mungu katika roho na kweli ndipo tunapomwona kama alivyo na utukufu wake. Hatuhitaji kuwa na haraka tunapomwabudu Mungu au tunapo abudisha mpaka pale tutaktpohakikishakila mmoja wetu amefika katika kilele cha kuabudu. Wasiojionyesha kwa wanadamu, bali waliopendekezwa mbele za Mungu katika uongozi wa Roho mtakatifu.

             Lazima pawepo na makubaliano au uhusiano kati ya kikundi cha kuabudu, kiongozi wa kuabudisha (worship leader), na Mchungaji au kiongozi kanisani. Pia kikundi cha kuabudu lazima kiwe na muda wa kukutana, kuomba, kufunga, kusoma neno pamoja.

            Sababu ya watu wa sifa kukutana pamoja, sio tu kwa ajili ya mazoezi, bali kupata muda wa pamoja ili kuepusha misuguano, migongano, wivu, makundi nk. Pia ni njia mojawapo ya kufahamiana zaidi. Tukijua kwamba hakuna aliye wa muhimu kuliko mwingine katika kikundi cha kusifu na kuabudu. Kinachotakiwa ni utii na unyenyekevu.

             Waabudishaji wanatakiwa kuishi kama familia moja, watu wenye nia moja, watu wanachukuliana mizigo, watu waliojitenga na uovu wa kila namna .

                        
                         Vidokezo muhimu katika kusifu.

  1. Baadhi ya aina za kusifu na kuabudu:

- Kusimama (Zab 135:1-2, 134:1)               -Kuinua mikono (Zab 134:2, 28:2)
-Kuinama au kupiga magoti (Zab 95:6)       -Kupiga makofi (Zab 7:1)
-Kucheza (Zab 149:3, 150:4, 2Sam 6:14)    -Kicheko (Zab 126:2, Ayu 8:20-21)
-Kufurahi (Kumb 12:11-12, Law 23:40)      -Kutembea (2Nya 20:21-22)
-Shangwe (Zab 95:1)                                    -Kupiga kelele (Zab 66:1, Law 9:23-24)
-Kupiga vigelegele (Zab 33:1, 32:11)           -Ukimya (Mhu 3:7)
-Kupaza sauti (Isaya 12: 6, Zab 42:4)           -Kulia/ kutoa machozi katika roho mtakatifu.

A)    Mambo muhimu kwa kiongozi au kikundi cha sifa.

  1. Kuwa na maandalizi ya maombi (hasa ya kufunga na kuomba)
 (Ikibidi maombi yachukuwe asilimia 80 na huduma asilimia 20)
-          Kuomba utakaso au kujitakasa (Warumi 12:1)
-          Kuitakasa ibada na kuombea udhiirisho wa uwepo wa Mungu
-          Kuombea mtumishi wa Mungu, Neno la Mungu na huduma zote.
-          Kuomba roho mtakatifu akupe mbinu kuwafisha watun katika kiwango cha juu (patakatifu pa patakatifu) cha  kumwabudu Mungu (Yh 4:23-24)
-          Kuomba Mungu akupe roho ya kuabudu (siyo kama aliyelazimishwa)

  1. Jitahidi kuwa mfano wa kuigwa kwa matendo na mwenendo wako (Isaya 29:13)
  2. Kuwa nadhifu, msafi (muonekano wako wa nje usiwe kwazo)
  3. Kuwa na dhamira njema mbele za Mungu na wanadamu (mdo 24:16)
  4. Jitahidi kuwa mtu wa kwanza kufika kanisani na kuanza kuomba


  1. Andaa pia (kwa tahadhari) nyimbo za matukio mbalimbali katika ibada kama:
-          Wakati wa kuombea wagonjwa na wenye shida mbalimbali
-          Wakati wa kukemea pepo / za giza
-          Wakati wa utoaji (2nyakati 29:27-28)
-          Wakati wa kuwaita watu kwa Yesu
-          Ujazo wa roho mtakatifu nk.

  1. Usilazimishe watu kufanya kile ambacho hujaanza kukifanya wewe. Mfano: (kupiga makofi, kuinua mikono, kuruka n.k)
  2. Jitahidi kuwa na lugha nzuri nzuri na yenye kuvutia katika uongozaji.
  3. Hakikisha mtumishi wa Mungu anapanda madhabahuni kukiwepo na uwepo wa Mungu / moto wa Roho mtakatifu.
  4. Kuwa na mawasiliano ya karibu na madhabau (Mtumishi wa Mungu au Muhubiri) wa siku hiyo.


ONYO!
Inatupasa kuwa na uhakika kwamba katika kila tunalofanya, katika kusifu na kuabudu (iwe ni kucheza, kuruka, kupiga makofi au sifa na kuabudu kupitia Ala za Muziki n.k), yote tuyafanye kwa ajili ya Bwana na kwa utukufu wake na si vinginevyo (Kol 3:17, 12, Fil 4:8,, 2:3,Kut 32:19)

 
                                          ..................................................................
                                                         John Stephen Shabani  

2 comments:

  1. Mafundisho safi sana hayo.
    Mungu akubariki sana.

    ReplyDelete
  2. BWANA YESU asifiwe, tunaomba darasa la Namna ya kuimba litayarishwe pia kwa lugha ya KISWAHILI.
    UBARIKIWENA bwana.

    ReplyDelete