Hatimaye waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania wakiongozwa na mwalimu wa muziki wa injili afrika mashariki bwana John Shabani, chini ya usimamizi wa chama cha muziki wa injili Tanzania (Chamuita) wamekamilisha video ya wimbo ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania. Pamoja na waimbaji mbalimbali kushiriki katika wimbo huo pia yumo mheshimiwa Martha Mlata ambaye amechangia sana katika kufanikisha kurekodi wimbo huo. Baadhi yam abo aliyo yafanya ni pamoja na kufanikisha kupata sare na bendera kutoka serekalini pamoja na kutoa feha za kufanikisha kurekodi video. Pia studio ya Pro arts studio ya jijini Dar es salaam ilijitolea kurekodi sauti. Wazo la kuwakusanya waimbaji wa injili na kurekodi wimbo wa miaka 50 ya uhuru, lilianzishwa na bwana Tc Timothy Chelula na kumshirikisha mwalimu John Shabani, ndipo walipo kihusisha chama cha muziki wa injili na vyombo mbalimbali vya habari. Muda si mrefu wimbo huo utasambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Baadhi ya waimbaji walioshiriki kurekodi wimbo huo ni:
1. Gloria kilahiro 18. Mzee Makassy
2. Amon Kilahiro 19. Mzungu Four
3. Masanja Mkandamizaji 20 Jane Misso
4. Upendo kilahiro 21 Addo November
5. Stella Joel 22. Martha Mlata
6. Nely Nyamanga 23. Ambwene mwasongwe
7. Joyce Ombeni
8. Bony Mwaitege 24. Douglas Pius
9. John Shabani 25. Mchumu Maximillian
10. Rose Manoza 26. Charles Thobias Malya
11. Yona Abiud 27. Joshua makondeko
12. Miriam Lukindo Mauki 28. Daniel Safari
13. Robert Bukelebe 29. Naomy Mbwambo
14. Nicholaus Misuzi 30. Joseph kasigala
15. Christina Matai 31. Debora Said
16. Tina Marego 32. Stara Thomas
17. Martha Mwaipaja 33. Victor Ahron
Na wengine wengi.
Mheshimiwa Martha, Mr Masanja na Malimu John wakitabasamuKampuni ya Pro arts wakiwa kazini
Masanja mkandamizaji akifanya vitu vyake
Baadhi ya magari mbalimbali ya waimbaji nnje ya jengo la studio
Mwimbaji mkongwe mzee makasi katika pozi
Mwalimu John Shabani akiwaongoza waimbaji wa Injili
Pamoja na hayo, viongozi wa chama cha muziki wa injili Tanzania tunatoa wito wa kujiunga na chama hicho, kwani kuna faida nyingi za kujiunga na chama. Fomu sasa zinapatyikana. kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0754818767, 0716560094.
No comments:
Post a Comment