Upendo kilahiro akiwa na mwalimu John Shabani
G stars wakiimba mbele ya marais na waheshimiwa mbalimbali
Mwalimu maarufu wa nyimbo za injili Afrika mashariki
(John shabani), akiimba kwa hisia kali mbele ya rais
Mzee makasy (Mwimbaji mkongwe), Akiimba mbele ya rais
Mheshimiwa martha mlata akiimba kwa hisia
Mtoto wa miaka 6 Gloria kilahiro akiimba kwa hisia kali mbele ya waheshimiwa
Wimbo wa kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania ulioimbwa na Tanzania Gospel All stars (Waimbaji nyota wa muziki wa injili Tanzania), umepata hadhi na heshima ya kuwa wimbo maalumu katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara.
Chini ya mwalimu John shabani na usimamizi wa chama cha muziki wa injili Tanzania(Chamuita), Waimbaji hao walipewa nafasi maalum ya kuimba wimbo huo mbele ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete na mbele ya marais wa nchi mbalimbali, mawaziri, wabunge, mabalozi, pomoja na maelfu ya watu waliohudhuria katika maadhimisho hayo. Viongozi na watu mbalimbali wamewapongeza waimbaji hao wa injili kwa umoja na mshikamano wao, pia wameupongeza wimbo huo, hivyo kuwaomba kuusambaza wimbo huo kwa watanzania ili kila mtu abarikiwe na wimbo huo
Hii ni mara ya kwanza kwa waimbaji wa injili kuungana pamoja na kurekodi wimbo wa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya uhuru wa Tanzania.
Video ya wimbo huo inategemea kusambazwa kwa watanzania kwa gharama ndogo.
Waimbaji walioshiriki kurekodi wimbo huo ni:
1. Gloria kilahiro 18. Mzee Makassy
2. Amon Kilahiro 19. Mzungu Four
3. Masanja Mkandamizaji 20 Jane Misso
4. Upendo kilahiro 21 Addo November
5. Stella Joel 22. Mheshimiwa Martha Mlata
6. Nely Nyamanga 23. Ambwene mwasongwe
7. Joyce Ombeni
8. Bony Mwaitege 24. Douglas Pius
9. John Shabani 25. Mchumu Maximillian
10. Rose Manoza 26. Charles Thobias Malya
11. Yona Abiud 27. Joshua makondeko
12. Miriam Lukindo Mauki 28. Daniel Safari
13. Robert Bukelebe 29. Naomy Mbwambo
14. Nicholaus Misuzi 30. Joseph kasigala
15. Christina Matai 31. Debora Said
16. Tina Marego 32. Stara Thomas
17. Martha Mwaipaja 33. Victor Ahron
Na wengine wengi.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania
No comments:
Post a Comment