Chaka chaka akiwa na mumewe Dr Mandlalele Mhinga.
Mwimbaji wa siku nyingi nchini Afrika ya kusini mwanamama Yvonne Chaka chaka yuko studio kwahivi sasa akijiandaa kutoa labum mpya ambayo kwa taarifa zilizopatikiana mpaka sasa katika album hiyo amewashirikisha waimbaji wengine kama Soweto gospel choir ambao juzi walikuwa studio(kwa kundi lililosalia afrika kusini wengine wako ziarani nchini Marekani) na mwimbaji huyo akiwa amewashirikisha katika nyimbo mbili,pamoja na mwanamuziki mwingine maarufu aitwaye Bono wa kundi la U2.
Chaka chaka ambaye amejizoelea mashabiki wengi barani Africa na duniani kutokana na muziki wake,itakumbukwa kwamba alipotembelea nchini Tanzania miaka ya karibuni alitangaza kwamba ameokoka na amekuwa ni mtu wa kanisani kumwabudu Mungu pamoja na kila kitu anachofanya anamtegemea Mungu,mpaka sasa haijajulikana ni nyimbo ngapi zitakazokuwemo kwenye album hiyo na ni nyimbo za aina gani, ingawa tayari amewashirikisha waimbaji kama Soweto gospel choir hata hivyo si kigezo album hiyo kuwa ya dini,ukweli utajulikana itakapotoka au yeye mwenyewe atakapotoa taarifa rasmi.
Chaka chaka ambaye mwishoni mwa mwezi January mwaka huu aliweza kuandika historia kwakuwa mwanamke wa kwanza kutoka Africa kupata tuzo ya World Economic Forum (WEF) iitwayo crystal award kutokana na juhudi zake katika kupambana na malaria pamoja na kazi nyingine za kijamii kwa ujumla,mwimbaji huyo ambaye enzi za utoto wake alikuwa mtoto wa kwanza mweusi kuonekana kwenye runinga ya taifa, south african television ambayo kwasasa inafahamika kama SABC,amekuwa na mafanikio mengi katika maisha yake ya muziki ambapo yeye na mumewe Dr Mandlalele Mhinga wanamiliki kampuni ya magari ya kifahari ya Limousine huko nchini kwao na shughuli nyingine.