MEMBERSHIP CARD
KADI ZA UANACHAMA
Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (Chamuita) ni chama halali kilichosajiliwa na kutambulika na Srekali ya Tanzania. Namba ya usajili ni BST 4598
Tunapenda kuwatangazia kuwa, Kadi za chama cha muziki wa injili Tanzania zimeanza kutolewaa kwa wanachama wanaoendelea kujaza fomu za kujiunga na chama hicho. Ewe mwimbaji, mwanamuziki, mtengenezaji, msambazaji na mpenzi wa nyimbo za injili, hakikisha umejiunga na chama cha muziki wa injili Tanzania (Tanzania Gospel Music Association) ili upate kadi yako. Kadi hii itakusaidia sana. Chama hiki kimesajiliwa na kutambuliwa na serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, pia ni moja ya vyama vinavyounda shirikisho la muziki Tanzania, shirikisho ambalo ni mwanachama wa shirikisho la muziki Duniani.
MALENGO NA MADHUMINI
Chama kitaendeshwa kama chombo kisicho na malengo ya kupata faida na chenye malengo na madhumini yafuatayo;-
i) Kulinda utamaduni wa Tanzania na heshima ya muziki wa Injili, sawa na Neno la Mungu
ii) Kuhamasisha maendeleo ya muziki wa Injili na nyanja zake nyingine
iii) Kutoa ushauri katika mambo yote yahusuyo muziki wa Injili, na watumishi wa Mungu waimbaji pia.
iv) Kuwakilisha na kulinda maslahi ya wanachama kitaifa na kimataifa.
v) kuwa chombo cha kuwezesha mawasiliano kati ya watu na vikundi katika kupeana taarifa kuhusu muziki wa Injili hapa nchini, na pia kuwezesha mawasiliano ya kimataifa.
vi) Kuwa na rejista ya wanamuziki wa Injili na kazi zao. Ili kusaidia kulinda na kutangaza haki za wanachama.
vii) Kutafuta mapato kwa njia ya ada, michango, harambee, maonyesho, kukopa, ufadhili au zaidi katika kuendeleza malengo na madhumuni ya Chama.
viii) Kuwawezesha wanamuziki wa Injili kwa njia ya kuwaongezea elimu
ix) Kuinua hadhi ya muziki wa Injili nchini
x) Kutambuliwa rasmi na Serikali yetu na wadau wengine
xi) Kuwekeza katika miradi, na kujipatia kipato kwa njia ya kuwakomboa jamii ya wanamuziki wa injili.
kwa maawasiliano: Mob: 0754 818 767, 0716 560094.
E-mail: touchingvoice@yahoo.com
No comments:
Post a Comment