Tamasha la Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka Tanzania baada ya kuwa na uzoefu wa kualika waimbaji wa Gospel kutoka nchi jirani kama Zambia, Kenya, Rwanda na Uganda, mwaka huu limevuka boda mpaka kwa mzee Mandela na kumpa mwaliko malkia wa GOSPEL AFRIKA Rebecca Malope ambae ameukubali.
Malope atakua mmoja kati wanamuzili wa injili watakiaoimba siku hiyo ya april 8, akiwemo Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Epraim Sekeleti (Zambia), Anastazia Mukabwa na wakali wengine ambapo Mgeni rasmi ni Waziri wa mambo ya nje Benard Membe na time hii kwa mara ya kwanza tamasha hilo litafanyika kwenye uwanja wa Taifa.
No comments:
Post a Comment