Pages

30 April 2012

KWA MARA NYINGINE CHRISTINA SHUSHO AIBUKA NA TUZO ZA GROOVE HUKO KENYA ,''LISEME'' WA SARAH K ,NAO WABEBA TUZO YA MWAKA.



Christina Shusho mwimbaji nyota wa muziki wa gospel Tanzania jioni ya leo ameibuka tena kidedea kwenye tuzo za groove zinazotolewa kila mwaka nchini Kenya kupitia kipengele cha mwanamuziki bora wa mwaka kutoka Tanzania tuzo ambayo alishinda mwaka jana akiwapita waimbaji wenzake waliopendekezwa kwenye kipengele hicho akiwemo Rose Muhando,Bahati Bukuku,Neema Mwaipopo pamoja na Boniface Mwaitege.

Sherehe za utolewaji wa tuzo hizo ziliongozwa na pastor Uche Agu mwimbaji wa Joyous pamoja na mwanadada Kambua ambao walikuwa wakiweka utani wa hapa na pale na kuchangamsha mamia ya wakazi wa Kenya waliojazana katika ukumbi wa kanisa la Baptist jijini Nairobi.wimbo ''LISEME'' wa mwanamama Sara Kiarie ama Sarah K umechukua tuzo ya wimbo bora wa kuabudu wa mwaka,huku mwanadada Emmy Kosgei akiondoka na tuzo ya mwimbaji bora wa kike wa mwaka pamoja na wimbo wake wa Ololo ukimpatia tuzo ya wimbo bora wa mwaka kwa upande wa eneo la Rift Valley.

Mwimbaji mkongwe wa muziki wa injili nchini Kenya Ruben Kigame alipewa tuzo maalumu kwa mchango wake mkubwa kwenye muziki wa gospel nchini humo. Mwimbaji huyo hakuwepo kwenye tuzo hizo kwakuwa yupo safarini nchini Marekani, ingawa tuzo yake alikabidhiwa kabla hajaondoka ambapo ilionyeshwa video fupi kutoka kwake akishukuru kwa tuzo hiyo ikiwa ni pamoja na kuwasifu waandaaji kwa kuzifanya tuzo hizo kuwa bora. Pia alitoa ushuhuda wake mfupi wa maisha yake kabla hajaokoka na hata alipookoka,aliweka bayana kwamba baada ya mkewe kufariki alifikiria kwamba asingeweza kuimba tena lakini Mungu ni mkuu akafanikiwa kutoa album yake ya ''TULIA''.
Baada ya video hiyo pastor Uche aliwanyanyua watu na kuongoza sala fupi juu ya Ruben Kigame akimuombea maisha marefu na baraka.
Tuzo hizo ambazo zilikuwa zikirushwa moja kwa moja na kituo cha KTN pamoja na kwenye mtandao zimesifiwa kwa kuzidisha ubora kila mwaka huku kukiwa hakuna malalamiko ya upendeleo na kuonyesha mfano wa kuigwa kwa tuzo nyinginezo ikiwa ni pamoja na uboreshwaji wa zawadi,pia waimbaji wa nchi hiyo waliweza kuonyesha viwango vya juu katika uimbaji.pastor Uche alihitimisha ngwe hiyo kwa wimbo wake My God is good.

ANGALIA BAADHI YA PICHA ZA TUKIO HILO KAMA ZILIVYOTOLEWA NA WAANDAAJI
WA TUKIO HILO GROOVE AWARDS 2012.TUTAKULETEA PICHA NYINGINE ZIKIPATIKANA.

Mambo yakiwa sawia eneo la zuria jekundu (red carpet
Mwanadada Neema kulia akiimba na mwenzie wimbo Wema na fadhili wa Ruben Kigame maalumu kwa ajili ya mwimbaji huyo.
Hapa wakati jukwaa likiwekwa sawa
Umati wa watu ukiwa eneo la Red carpet kwa viburudisho wakisubiri kuingia ukumbini

No comments:

Post a Comment