Mwimbaji nyota wa gospel nchini Tanzania Upendo Kilahiro
ameweza kupokelewa vyema nchini Canada
huku tamasha lake la kwanza kufanyika jijini Ottawa
ndani ya kanisa la Christ Chapel Bible kufanyika kwa mafanikio ikiwa ni pamoja
na watu watatu kukabidhi maisha yao
kwa Yesu na mwengine akipokea uponyaji.
Tamasha hilo ambalo lengo lake lilikuwa ni kwa ajili ya
kukusanya fedha za umaliziaji wa shule ya watoto yatima ya mkoani Morogoro
nchini Tanzania iitwayo Dayspring Orphanage boarding school ambayo inafadhiliwa
na kanisa hilo,ambapo watu wengi walihudhuria wakiwemo kutoka makanisa ya
jirani kama River Jordan Community kwakuwa ni kawaida makanisa jirani
kusaidiana na kuwa pamoja kwenye matukio kama hilo,tamasha hilo liliongozwa na
viongozi wa kanisa hilo akiwemo Bishop Afolabi,Peter Mwaiteleke huku wageni
rasmi walikuwa maafisa ubalozi wa Tanzania nchini humo pamoja na Dada Niku Kyungu
Mordi na mumewe ambao hufanya huduma ya kuhubiri huko Maryland Marekani.
No comments:
Post a Comment