Pages

30 May 2012

UNGANA NA KITUO CHA MAFUNZO YA UIMBAJI

 John akiwa na wanafunzi wake kabla ya kuanza zoezi la uimba coco Beach

John Akiwa kazini

Je ungependa kujiunga na kundi la waimbaji chini ya mwalimu John Shabani, wasiliana nasi ili upewe ratiba ya mazaezi ya suti nay a mwili, ili uweze kufikia kiwango cha kimataifa.
Hey do you like to become a good singer? Are you ready to join our program?
Please, just communicate with us, so that we give you our vocal training program
Mob: +255 754 818 767
Welcom!  Karibu Sana!

JOHN SHABANI AFANYIWA MAOMBI MAALUM

 
 Mwalimu wa nyimbo za injili Afrika Mashariki, 
John Shabani, akiombewa na watumishi wa Mungu

John Akiimba na kucheza namama yake wa kiroho, Dr. Getrude Rwakatare.

Ilikua ni Jumapili ya uwepo wa Mungu. Baada ya kushusha sifa huku akiimba na kwaya yake The Joybringers, Watumishi waMunguWakiongozwa na Dk. Getrude Rwakatare, waliamua kumuombe John Shabani, Ili Mungu aendelee kukitunza kipawa cha utunzi na uimbaji, pamoja na kumfanikisha katika maono yake. Utukufu na heshima apewe Bwana.

28 May 2012

KANISA LA CHOMWA MOTO HUKO ZANZIBAR

  Mmoja wa waandamani wa Kundi la Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIKI) Kisiwani Unguja,Zanzibar akionyeshan kitambaa kilicho na Damu mapema leo Asubuhi wakati wakiendelea na maandamano yao ambayo yamesababisha vurugu kubwa kisiwani humo,iliyopelekea kuchomwa moto kw
Askari wa kutuliza ghasia wakifanya doria mitaa mbalimbali Zanzibar leo asubuhi
 

 Hali ya amani katika visiwa vya Zanzibar hasa kwa jamii ya Wakristo inazidi kuwa tete baada ya usiku wa Kuamkia leo, Kanisa la TAG visiwani Zanzibar linaloongozwa na Pastor Kaganga Visiwani humo kulipuliwa kwa kitu kinachosadikika kuwa ni bomu na kuteketeza sehemu kubwa ya madhabahuni mwa kanisa hilo na sehemu za Milango ya Kanisa hilo.

Kanisa hilo lililokuwa na uwezo wa kuchukua Waumini zaidi ya 1000 limechomwa moto ikiwa ni mara ya pili baada ya mara ya kwanza kitu kinachosadikika kuwa ni bomu kutupwa ndani ya kanisa hilo mwanzoni mwa mwaka huu na bomu hilo kushindwa kulipuka wakati wa Ibada. Baada ya Uchunguzi wa Polisi katika tukio la kwanza Polisi walisema bomu hilo lilokuwa na uwezo wa kuteketeza kila kitu kilichomo ndani ya Kanisa hilo lakini ajabu halikuweza kulipuka wakati lilikuwa tayari kwa kulipuka.

Kumekuwa na hali ya Sinto fahamu kwa Wakristo wengi wanaoabudu katika Makanisa visiwani Zanzibar na kasi ya serikali katika Kushughulikia masuala haya imekuwa si ya kuridhisha. Ndugu zetu wa Zanzibar wanahitaji maombi katika kusimama kwao katika ardhi hiyo inayosadikiwa watu zaidi ya 95% ni dini ya Kiislam.



 Gari la askofu Mganga likiwa limechomwa moto na watu wasiofahamika wakati limeegeshwa nje ya kanisa hilo jana usiku.

 Kanisa la Tanzania Assemblies of God(T.A.G), lililopo mtaa wa Kariakoo visiwani Zanzibar ambalo limechomwa moto usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana.

 Waandamanaji wa jumuiya ya uamsho na mihadhara ya kiislamu(JUMIKI)wakiwa katika maandamano leo asubuhi.

Bishop Dickson Maganga wa kanisa la T.A.G Zanzibar akizungumza na mwandishi wa habari.

MTANGAZAJI WA PRAISE POWER RADIO YA DAR ES SALAAM AFUNGA PINGU Z MAISHA

Erick Brighton ktk pozi na mkewe mara baada ya kutoka Church

Hatimaye mtangazaji wa Praise Power Radio, bwana Erick Brighton afunga pingu za maisha. Mtangazaji huyo ambaye amekuwa akiongoza vipindi vya usiku na kugusa mioyo ya watu wengi, sasa ameagana na maisha ya upweke. Ndoa hiyo imefungwa katika kanisa la Tanzania Assemblies of God mikocheni B mlima wa moto kwa mchungaji Gertrude Rwakatare. Uongozi wa blog hii  unawapongeza maharusi na kuwatakia baraka na ulinzi wa Mungu katika maisha yao.

25 May 2012


BREAKING NEEEEEEEWZ!!!!!
TANZANIA WORSHIP EXPERIENCE KUANZA MCHAKATO WA KUMTAFUTA "MWABUDISHAJI HALISI" KATIKA HOTEL YA THE ATRIUMS SINZA AFRIKASANA

Mchakato huu unaanza leo saa 3 asubuhi na mpaka sasa watu wamenza kuingia kwa kasi sana.
Mchungaji Charles Mbogoma (kulia) akiwa kazini
Stage kwaajili ya waimbaji
Mtoto na mchungaji wa Mchungaji Mbogoma akilifunga banner
Wahudumu wa The Atriums Hotel wakiwa katika maandalizi
Kazi ya Mungu inasonga na wale wampendao
Blogger na Design, Rulea Sanga akikurushia matukio. Kumbuka hilo bango ndiye aliyelitengeneza..Ukiwa na kazi yoyote ya design unaweza kukutana nami kwa +255 715 85 15 23
 Blogger Samsasali akitupia vitu katika blog yake ya www.samsasali.blogspot.com
 Mwenyekiti Makaranga akiwaandikisha washiriki
 Mchungaji Charles Mbogoma (kushoto) akifuatilia uandikishaji
 Washiriki
Katibu wa TWE, Nasobile 

MHESHIMIWA DK FENELLA MUKANGARA KUWA MGENI RASMI KATIKA TAMASHA LA KUABUDU NA MAOMBI KWA TAIFA

 Dr. Fenella Mukangara
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
 
Dk/Rev. Getrude Rwakatare

Mh. Martha Mlata (MB)
Tarehe 10.06.2012, ni siku ambayo kwaya mbalimbali na waimbaji binafsi kwa pamoja wataungana  katika kumsifu na kumwabudu Mungu, sambamba na kuliombea Taifa letu la Tanzania. Dk/Rev. Getrude Rwakatare ndiye atakayeongoza maombi hayo. Pia Maaskofu mbalimbali, wachungaji, vingozi mbalimbali wa serikali pamoja na taasisi zisizokuwa za serikali, wamethibitisha kuwepo siku hiyo.

Mgeni rasmi katika tamasha hilo ni Mheshimiwa Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na michezo, Dr. Fenella Mukangara

Pamoja na kuliombea taifa, pia tovuti pamoja na mkanda wa video ya mwalimu wa muziki wa injili Afrika mashariki, bwana John Shabani vitazinduliwa. kabla ya saa maalumu ya sifa na kuabudu live, waimbaji mbalimbali wakiongozwa na Mh. Martha Mlata wataimba. Wengine ni Mzee makasy, Cosmas Chidumule, Jane Miso, Stella Joel, Faraja Ntaboba, Addo November, Albino Group, Calvary, Nicolina msungu, Bella Kombo, Celine Theophil, Joybringers Choir na wengine wengi. Tamasha litafanyika ndani ya jengo la kisasa katika kanisa la T.A.G Magomeni, kuanzia saa saba mchana.

Sambamba na wageni mbalimbali, Pia tumemwalika Mr Ruge Mutahaba, Mr Alex Msama pamoja na viongozi wa Chama Cha Muziki Wa injili Tanzania.

Vazi la tamasha ni rangi nyeupe na nyekundu.

Tunahitaji mchango wa hali na mali ili kufanikisha tamasha hilo la kipekee.

Usipange kutokuhudhuria siku hiyo.

21 May 2012

JOHN SHABANI-KUFANYA TAMASHA LA KUABUDU, KULIOMBEA TAIFA LINALOITWA "SAA YA KUABUDU-WORSHIP HOUR" NA KUZINDUA BLOG YAKE


Baada ya kufanya vizuri katika kuwaongoza waimbaji wa injili nchini Tanzania na kuimba wimbo maalumu wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru Tanzania, sasa ameaandaa tamasha la kuabudu litakalofanyika katika kanisa la TAG Magomeni siku ya tarehe 10.06.2012 kuanzia saa 8:00 mchana

Mgeni rasmi ni Waziri wa Habari , Vijana na utamaduni, Dr. Fenella Mukangara.
Pia waheshimiwa mbambali, Maaskofu, wachungaji, viongozi mbalimbali wamethibitisha kuhudhuria siku hiyo. Itakuwa ni siku ya kwaya, bandi na waimbaji binafsi kumwabudu Mungu pamoja, wakiongozwa na watumishi mbalimbali.  
Tunahitaji maombi na ushauri wenu ili kufanikisha siku hiyo.

17 May 2012

SIKU YA WAIMBAJI WA INJILI KUMWINUA MUNGU PAMOJA, KUABUDU PAMOJA NA KULIOMBEA TAIFA PAMOJA IMEWADIA. NI TAMASHA LITALOZIKUTANISHA KWAYA NA WAIMBAJI WA BINAFSI PAMOJA





Baada ya kufanya vizuri katika kuwaongoza waimbaji wa injili nchini kuimba wimbo maalum kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru, mwalimu wa John Shabani chini ya udhamini na usimamizi wa chama cha Muziki wa Injili Tanzania, ameandaa tamasha la kipekee lijulikanalo kama WORSHIP HOUR (SAA YA KUABUDU) ni saa maalum ya sifa na kumwabudu Mungu live itakayoongozwa na mass choir chini ya mwalimu John Shabani, aliyeongoza waimbaji wa injili kuimba katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru pamoja na waalimu wengine. Pia kutakuwa na muda maalum wa kumshuku Mungu kwa amani aliyotupa pamoja na kuombea Baraka kwa ajili ya nchi yetu. Maombi hayo yataongozwa na Dk Getrude Rwakatare.tamasha hilo litaaambatana na uzinduzi wa Video na tovutiya ya Mlm john shabani. 
Kabla ya saa ya kuabudu, Tumealika waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi. Watakao mtumikia Mungu kwa mjia ya uimbaji. Siku hiyo Mheshimiwa Mbunge Martha Mlata ataimba pamoja na waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili kama vile Mzee Makasy, Cosmas Chidumule, Jangalason, Stella Joel, Safi kutoka Rwanda, Belle Kombo, Celine Theophil, Mwana mapinduzi group, Faraja Ntaboba kutoka Kongo, Upendo kilahiro, Addo November, Joseph Nyuki, Albino group na wengine wengi  pamoja na kwaya mbalimbali alizowahikufundisha Mlm John Shabani, na wengine wengi.
Viongozi mbali mbali wa Serikali na mashirika yasiyokuwa ya serikali na madhehebu ya dini, wakiwemo Mheshimiwa Rev. Dk. Getrude Rwakatare, Eng. Juliana Palangyo, Mheshimiwa Martha Mlata (MB), Mheshimiwa Dk. Mary Mwanjelwa (MB), watakuwepo.

Tamasha hilo linatarajia kufanyika katika ukumbi wa kisasa katika kanisa la T.A.G Magomeni, karibu na Hoteli ya Travetine, tarehe 10 .06. 2012 siki ya jumapili kuanzia saa nane mchana.  Hivyo basi, kwa wale wanaotaka kujiunga na mass choir kwa ajili ya kumtuku Mungu siku hiyo, wawasiliane na kamati ya tamasha hilo, ili mjulishwe siku za mazoezi na maali pa mazoezi.

Mawasiliano:
 Mob: 0716560094, 0754818767
Web: www.johnshabani.blogspot.com

Vazi la siku hiyo, ni rangi nyeupe na nyekundu

Kuhusu mgeni rasmi, mtajulishwa baadaye. Ila ni mheshimiwa waziri katika serikali yetu.
Tangazo limetengenezwa na Rulea Sanga +255 715 85 15 23 | www.rumaafrica.blogspot.com | rumatz2011@yahoo.com

TUNAHITAJI MAOMBI  NA USHAURI WENU

16 May 2012

BAADA KUFANYA VIZURI MWAKA JANA KWENYE CAMPAS NIGHT SOS MISSION INTERNATIONAL WAANDA MKUTANO MKUBWA WA INJILI DAR


SOS Mission walikuwepo mwaka jana kwenye tamasha kubwa la aina ya la Campas Night lililokuwa na timu kubwa, wakiongozwa na kiongozi wao Past Johnnes mwaka huu wanakuja na mkutano mkubwa wa injili utakao fanyika hapa Dar kuanzia Tar 13-17 Jun mkutano huo umepewa jina la sherehe za ishara na miujiza. maanadalizi ya mkutano huo yanaendelea kwa kasi kwa kuandaa watenda kazi wengi. Timu ya maombi teyali wanaendelea na maombi katika kanisa la mito ya baraka pale Jangwani kila wiki, wachungaji na wahudumu wengine nao wanaendelea kuandaliwa ili kuhakikisha kuwa kila idara ina kaa vizuri.
Mch Johnnes akihubiri kwenye Campas Night mwaka jana wana  

SOS watakaokuja Dar wanakadiliwa kuwa 200 hivi na watafanya uinjilisti mitaani kwa kutumia magari na helkopta kwa kutua kwenye openi na kuweza kufanya ushuhudiaji hivyo wanaobwa vijana waliookoka wanaoweza kutafsili kingeleza kuja kiswahili kujitokeza ili kuzunguka na timu hiyo na wengine watakuwa kwenye helkopta(haya ambao hamjawahi kupanda helkopta changamkia tenda) zaidi ya hapo wakati wa mkutano mtu atakyeleta watu 20 atapewa zawadi na watu hao watalipiwa nauli na mchungaji atakayelea watu 20 yeye atapewa zawadi ya vyombo vya mziki kwaajili ya huduma. hivyo jiandae kuleta watu uwezavyo ili ujinyakulie zawadi. na si hivyo tu wachungaji watapata kusaidiwa kielimu pia.


ikiachilia uinjilisti utakao fanywa SOS band watakuwepo kutumbuiza siku zote za mkutano na waimbaji wengine wa hapa kwetu Tanzania watakuwepo kama Kinondoni Revival, Temeke Revival, the Repers ,Upendo Nkone, Christina Shusho, Bony Mwaitege, John Shabani na wengineo. wapendwa tunaobwa kuja na watu wasiookoka, wagonjwa na wenye matatizo mbalimbali ili wakutane na Mungu wao na kupokea miujiza yao na kama unataka kuwa mhudumu utawasiliana na no hapo chini.














14 May 2012

HAPPY MNALE – MWANDISHI WA HABARI ALIYEDHAMIRIA KUINUA HUDUMA ZA WAIMBAJI WA INJILI KUPITA MAKALA MBALIMBALI



Kama kuna watu wanaostahili kupongezwa katika kuchangia kuinua huduma na vipaji vya wasanii wa Injili nchini, basi mwanadada Happy Mnale ni miongoni mwao.
Pamoja na makala mbalimbali, pia amekuwa mstari wa mbele kutangaza huduma na kazi za waimbaji wa nyimbo, wanamuziki, maproducer, ma MC na kila aina ya makundi yanayojihusha na shughuli za Injili. Makala hizo za injili zinapatikana katika gazeti la TANZANIA DAIMA kila siku ya ijumaa.

Waimbaji wengi wamepata kujulikana zaidi kuhusu huduma zao, maisha yao, mipango na maono yao na kila jambo linalo wahusu waimbaji wa injili linalofaa jamii kulifahamu.
Ewe mwimbaji unayetaka maendeleo ya huduma yako, usisite kuwasiliana na mwanadad huyo, hakika hutabaki kama ulivyo sasa.

Mawasiliano:
0754818767, 0712003539

11 May 2012

Kikundi Cha Al-Shabaab Tanzania chatishia Kulipua Kanisa La Efatha



Kikundi kinachojiita ‘Al-Shabaab Tanzania’, kimetishia kuteketeza kwa mabomu eneo lote pamoja na majengo ya Kanisa la Efatha, lililopo Mwenge, jijini Dar es Salaam, wakati wowote kuanzia sasa, kuhakikisha linabaki kama uwanja wa kuchezea mpira, taarifa ambazo Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai (DCI), Robert Manumba, amesema hajazipata na kuahidi kuzifanyia kazi.Mpango huo umeelezwa na kikundi hicho kuwa utatekelezwa kupinga uongozi wa kanisa hilo kujichukulia sheria mikononi kila mara na kunyanyasa watu wasio na hatia bila sababu za msingi.Kanisa hilo linamilikiwa na kuongozwa na Nabii na Mtume wake, Josephat Mwingira.

Mpango huo wa kikundi hicho kinachojiita cha chenye msimamo mkali kinachopigania haki zilizoshindwa kutekelezwa na serikali kwa wakati kupitia mamlaka zake zinazohusika hususan mahakama, umebainishwa katika taarifa yake ya Aprili 20, mwaka huu.

Nakala ya taarifa ya kikundi hicho yenye anuani ya sanduku la posta Tanga, Tanzania, imetumwa pia kwa gazeti hili, ikivitaka vyombo vya habari kuhakikisha vinatangaza taarifa hiyo.
“Vyombo vya habari tunavitaka kutoa taarifa hii kwa umma kwamba tunao mpango wa kuteketeza kwa mabomu eneo lote na majengo ya Efatha Ministry iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam wakati wowote kuanzia sasa na kuhakikisha eneo hilo linabakia kama uwanja wa kuchezea mpira,” inadai sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na mtu anayedai kuwa ni mwakilishi mkazi wa kikundi hicho lakini hakujitaja jina.
Katika taarifa hiyo, kikundi hicho kimewataka waumini wote kutohudhuria ibada ya aina yoyote katika kanisani hilo.

Pia kimewataka kutofanya kazi yoyote ya kiuchumi ili kuepuka milipuko inayoweza kutokea eneo hilo wakati wowote.“Kwa hiyo, hatutaki kuwauwa watu wasio na hatia, lakini kwa wale watakaopuuzia taarifa hii waendelee tu kuhudhuria kanisani hapo au katika kitegauchumi chao cha benki halafu familia zao zitashuhudia kitakachowatokea,” inadai taarifa hiyo.Kikundi hicho kinadai kuwa kitendo cha uongozi wa kanisa hilo kujisafisha kupitia gazeti moja linalotolewa kwa lugha ya Kiswahili kila wiki, hakina msingi, badala yake ni uongo mtupu.
Kimesema kujisafisha kwa uongozi huo kwamba wanaongoza roho za watu na kujikinga kwa mwamvuli wa kanisa na kuwaua wengine ni dhambi kubwa siyosamehewa.

“Hata hivyo, kama kanisa hilo linaweza kuwa na haki kwa namna yoyote ile, Biblia yao kama mhimili mkuu wa imani yao ni wapi pameandikwa kwamba ni haki kumvunjia jirani yako nyumba yake?” kilihoji na kuongeza:
“Mbona Yesu alisema jirani yako akikupiga kofi shavu la kulia mgeuzie na la kushoto? Iwapi kwa Efatha subira hii hadi kukiuka agizo la mahakama na kuvunja sheria ya nchi.”

DCI MANUMBA
Kwa upande wake, DCI Manumba aliahidi kuzifanyia uchunguzi taarifa hizo ili kujua ukweli wa suala hilo.
“Tutachunguza jambo hilo kufahamu kama ni kweli au kuna kikundi cha watu wachache kinataka kutishia watu. Taarifa hizo zilikuwa hazijanifikia, wewe ndio unaniambia,” alisema Kamishna Manumba.
 

KAIMU RPC KINONDONI
Naye Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, John Mtalimbo, alisema taarifa za tishio za kikundi hicho dhidi ya kanisa hilo bado hajazipata.Alisema anachokifahamu katika kanisa hilo ni kuwa awali palikuwapo na mgogoro na kuahidi kulifanyia kazi jambo hilo ili kufahamu ukweli juu ya taarifa zilizoenezwa na kikundi hicho.

Kikundi hicho kinadai kuwa jambo lingine linalothibitisha kwamba Efatha chini ya Mwingira ina huduma ya kutia shaka kiroho ni pale wanapojichukulia sheria mkononi kuvunja na kuharibu mali za jirani zao ilihali kesi ya msingi kuhusiana na eneo hilo ipo mahakamani na hukumu bado haijatoka.
Kinadai dini nchini zipo kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi, lakini dini ya aina yoyote haipaswi kuwa juu ya sheria, katiba, mahakama wala watu wenyewe. Kinadai kuwa mtu anayo haki, utashi na uhuru wa kuabudu na si kujificha chini ya kivuli cha dini au kanisa na kufanya uharibifu juu ya wengine.

Kutokana na hilo, kinadai kuwa hata kama Efatha ingekuwa mmiliki halali wa eneo hilo, haikupaswa kujichukulia sheria mkononi kwa kuwavunjia wengine ilhali mahakama haijatoa hukumu kwa kuwa mahakama ilitoa taarifa ya eneo hilo kuendelea na shughuli zake kama kawaida.“Hivyo, basi umma wa Watanzania na wapenda amani duniani kote wanaona kwamba kanisa la Efatha ni lazima liwajibike kulipa mali zote za kiwanda kilichoharibiwa ili iwe fundisho hata kwa madhehebu mengine yasiyofuata nyayo za Yesu au Mtume,” kilidai kikundi hicho.

Kikundi hicho kimetahadharisha kuwa taarifa yake hiyo haihusiani kwa namna yoyote ile na upande ulioathiriwa iwe kiwanda au wakazi wa Bagamoyo au Sumbawanga na kusisitiza kuwa taarifa hiyo ni ya kikundi maalum kilichodhamiria kuona haki inatendeka kwa namna yoyote ile.
“Na katika hili tunaamini kwamba tunakwendea peponi. Na hata hivyo huu ni mwanzo. Mengine yatafuata,” kilidai.
Mwenyekiti wa ulinzi wa Kanisa hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Kanali mstaafu Mama Kambo, alipoulizwa kuhusiana na taarifa hiyo alijibu kwa kifupi kuwa hajaipata.

Akizungumza na NIPASHE ambalo jana mchana lilifika kanisani hapo, Mama Kambo alisema hawajapata taarifa za tishio hilo na wala hajui hatua za kuchukua ili kukabiliana na tishio hilo.Hata hivyo, baada ya NIPASHE kumuonyesha nakala ya barua iliyoandikwa na kikundi hicho, Mama Kambo alijibu kwa kifupi kuwa hawajui hatua zozote za kuchukua na kutaka mwandishi ampe ushauri.Juhudi za mwandishi kuwaomba kumpata Mwingira kuelezea tishio hilo ziligonga mwamba baada ya wachungaji waliokuwapo kusema kuwa ni vigumu kumuona moja kwa moja.

“Yaani huwezi kumuona Mwingira na wala hatuwezi kukupa namba yake ya simu labda subiri tuendelee kuwasiliana na wasaidizi wake,” alisema Kambo.
Hivi karibuni, kanisa hilo liliingia katika mgogoro baada ya kubomoa kiwanda cha Afro Plus ambacho kipo ndani ya uzio wa Efatha.Katika uharibifu huo waumini zaidi ya 50 walikamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni na baadaye walifikishwa mahakamani.
Jana kulikuwa na ulinzi mkali katika kanisa hilo, na walinzi walijaribu kumzuia mwandishi asifike katika baadhi ya maeneo aliyotaka kupita na kumueleza kuwa utaratibu wa kanisa hauruhusu.
“Hiyo taarifa ni mpya na nimeisikia kutoka kwako. Ila tutaifuatilia ili tuweze kubaini ukweli wa jambo hilo na hatua kuchukuliwa dhidi yao,” alisema Mtalimbo.