Kikundi kinachojiita
‘Al-Shabaab Tanzania’, kimetishia kuteketeza kwa mabomu eneo lote pamoja na
majengo ya Kanisa la Efatha, lililopo Mwenge, jijini Dar es Salaam, wakati
wowote kuanzia sasa, kuhakikisha linabaki kama uwanja wa kuchezea mpira,
taarifa ambazo Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai (DCI), Robert Manumba, amesema
hajazipata na kuahidi kuzifanyia kazi.Mpango huo umeelezwa na kikundi hicho
kuwa utatekelezwa kupinga uongozi wa kanisa hilo kujichukulia sheria mikononi
kila mara na kunyanyasa watu wasio na hatia bila sababu za msingi.Kanisa hilo
linamilikiwa na kuongozwa na Nabii na Mtume wake, Josephat Mwingira.
Mpango huo wa kikundi
hicho kinachojiita cha chenye msimamo mkali kinachopigania haki zilizoshindwa
kutekelezwa na serikali kwa wakati kupitia mamlaka zake zinazohusika hususan
mahakama, umebainishwa katika taarifa yake ya Aprili 20, mwaka huu.
Nakala ya taarifa ya
kikundi hicho yenye anuani ya sanduku la posta Tanga, Tanzania, imetumwa pia
kwa gazeti hili, ikivitaka vyombo vya habari kuhakikisha vinatangaza taarifa
hiyo.
“Vyombo vya habari
tunavitaka kutoa taarifa hii kwa umma kwamba tunao mpango wa kuteketeza kwa
mabomu eneo lote na majengo ya Efatha Ministry iliyopo Mwenge jijini Dar es
Salaam wakati wowote kuanzia sasa na kuhakikisha eneo hilo linabakia kama
uwanja wa kuchezea mpira,” inadai sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na mtu
anayedai kuwa ni mwakilishi mkazi wa kikundi hicho lakini hakujitaja jina.
Katika taarifa hiyo,
kikundi hicho kimewataka waumini wote kutohudhuria ibada ya aina yoyote katika
kanisani hilo.
Pia kimewataka
kutofanya kazi yoyote ya kiuchumi ili kuepuka milipuko inayoweza kutokea eneo
hilo wakati wowote.“Kwa hiyo, hatutaki kuwauwa watu wasio na hatia, lakini kwa
wale watakaopuuzia taarifa hii waendelee tu kuhudhuria kanisani hapo au katika
kitegauchumi chao cha benki halafu familia zao zitashuhudia kitakachowatokea,”
inadai taarifa hiyo.Kikundi hicho kinadai kuwa kitendo cha uongozi wa
kanisa hilo kujisafisha kupitia gazeti moja linalotolewa kwa lugha ya Kiswahili
kila wiki, hakina msingi, badala yake ni uongo mtupu.
Kimesema kujisafisha
kwa uongozi huo kwamba wanaongoza roho za watu na kujikinga kwa mwamvuli wa
kanisa na kuwaua wengine ni dhambi kubwa siyosamehewa.
“Hata hivyo, kama
kanisa hilo linaweza kuwa na haki kwa namna yoyote ile, Biblia yao kama mhimili
mkuu wa imani yao ni wapi pameandikwa kwamba ni haki kumvunjia jirani yako
nyumba yake?” kilihoji na kuongeza:
“Mbona Yesu alisema jirani yako akikupiga kofi
shavu la kulia mgeuzie na la kushoto? Iwapi kwa Efatha subira hii hadi kukiuka
agizo la mahakama na kuvunja sheria ya nchi.”
DCI MANUMBA
Kwa upande wake, DCI Manumba aliahidi kuzifanyia uchunguzi taarifa hizo ili kujua ukweli wa suala hilo.
“Tutachunguza jambo hilo kufahamu kama ni kweli au kuna kikundi cha watu wachache kinataka kutishia watu. Taarifa hizo zilikuwa hazijanifikia, wewe ndio unaniambia,” alisema Kamishna Manumba.
KAIMU RPC KINONDONI
Naye Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, John Mtalimbo, alisema taarifa za tishio za kikundi hicho dhidi ya kanisa hilo bado hajazipata.Alisema anachokifahamu katika kanisa hilo ni kuwa awali palikuwapo na mgogoro na kuahidi kulifanyia kazi jambo hilo ili kufahamu ukweli juu ya taarifa zilizoenezwa na kikundi hicho.
Kwa upande wake, DCI Manumba aliahidi kuzifanyia uchunguzi taarifa hizo ili kujua ukweli wa suala hilo.
“Tutachunguza jambo hilo kufahamu kama ni kweli au kuna kikundi cha watu wachache kinataka kutishia watu. Taarifa hizo zilikuwa hazijanifikia, wewe ndio unaniambia,” alisema Kamishna Manumba.
KAIMU RPC KINONDONI
Naye Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, John Mtalimbo, alisema taarifa za tishio za kikundi hicho dhidi ya kanisa hilo bado hajazipata.Alisema anachokifahamu katika kanisa hilo ni kuwa awali palikuwapo na mgogoro na kuahidi kulifanyia kazi jambo hilo ili kufahamu ukweli juu ya taarifa zilizoenezwa na kikundi hicho.
Kikundi hicho kinadai
kuwa jambo lingine linalothibitisha kwamba Efatha chini ya Mwingira ina huduma
ya kutia shaka kiroho ni pale wanapojichukulia sheria mkononi kuvunja na
kuharibu mali za jirani zao ilihali kesi ya msingi kuhusiana na eneo hilo ipo
mahakamani na hukumu bado haijatoka.
Kinadai dini nchini zipo
kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi, lakini dini ya aina yoyote haipaswi
kuwa juu ya sheria, katiba, mahakama wala watu wenyewe. Kinadai kuwa mtu
anayo haki, utashi na uhuru wa kuabudu na si kujificha chini ya kivuli cha dini
au kanisa na kufanya uharibifu juu ya wengine.
Kutokana na hilo, kinadai
kuwa hata kama Efatha ingekuwa mmiliki halali wa eneo hilo, haikupaswa kujichukulia
sheria mkononi kwa kuwavunjia wengine ilhali mahakama haijatoa hukumu kwa kuwa
mahakama ilitoa taarifa ya eneo hilo kuendelea na shughuli zake kama
kawaida.“Hivyo, basi umma wa Watanzania na wapenda amani duniani kote wanaona
kwamba kanisa la Efatha ni lazima liwajibike kulipa mali zote za kiwanda
kilichoharibiwa ili iwe fundisho hata kwa madhehebu mengine yasiyofuata nyayo
za Yesu au Mtume,” kilidai kikundi hicho.
Kikundi hicho
kimetahadharisha kuwa taarifa yake hiyo haihusiani kwa namna yoyote ile na
upande ulioathiriwa iwe kiwanda au wakazi wa Bagamoyo au Sumbawanga na
kusisitiza kuwa taarifa hiyo ni ya kikundi maalum kilichodhamiria kuona haki
inatendeka kwa namna yoyote ile.
“Na katika hili tunaamini
kwamba tunakwendea peponi. Na hata hivyo huu ni mwanzo. Mengine yatafuata,”
kilidai.
Mwenyekiti wa ulinzi wa
Kanisa hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Kanali mstaafu Mama Kambo,
alipoulizwa kuhusiana na taarifa hiyo alijibu kwa kifupi kuwa hajaipata.
Akizungumza na NIPASHE
ambalo jana mchana lilifika kanisani hapo, Mama Kambo alisema hawajapata
taarifa za tishio hilo na wala hajui hatua za kuchukua ili kukabiliana na
tishio hilo.Hata hivyo, baada ya NIPASHE kumuonyesha nakala ya barua
iliyoandikwa na kikundi hicho, Mama Kambo alijibu kwa kifupi kuwa hawajui hatua
zozote za kuchukua na kutaka mwandishi ampe ushauri.Juhudi za mwandishi
kuwaomba kumpata Mwingira kuelezea tishio hilo ziligonga mwamba baada ya
wachungaji waliokuwapo kusema kuwa ni vigumu kumuona moja kwa moja.
“Yaani huwezi kumuona Mwingira
na wala hatuwezi kukupa namba yake ya simu labda subiri tuendelee kuwasiliana
na wasaidizi wake,” alisema Kambo.
Hivi karibuni, kanisa
hilo liliingia katika mgogoro baada ya kubomoa kiwanda cha Afro Plus ambacho
kipo ndani ya uzio wa Efatha.Katika uharibifu huo waumini zaidi ya 50
walikamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni na baadaye walifikishwa
mahakamani.
Jana kulikuwa na ulinzi
mkali katika kanisa hilo, na walinzi walijaribu kumzuia mwandishi asifike
katika baadhi ya maeneo aliyotaka kupita na kumueleza kuwa utaratibu wa kanisa
hauruhusu.
“Hiyo taarifa ni mpya na
nimeisikia kutoka kwako. Ila tutaifuatilia ili tuweze kubaini ukweli wa jambo
hilo na hatua kuchukuliwa dhidi yao,” alisema Mtalimbo.
No comments:
Post a Comment