Baadhi ya miili ya watu
waliochomwa moto ndani ya jengo la kanisa.
Ombi limetolewa na mchungaji Yuguda Mburnvwa wa kanisa la
Church of Brethren la nchini Nigeria kuwaombea Wakristo wanaoishi
kaskazini mwa nchi hiyo kutokana na mauaji yanayofanywa na wapiganaji wa
kikundi cha kiislamu kiitwacho Boko haram dhidi ya wakristo wa nchi hiyo.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na kituo cha Premier
radio ya kikristo nchini Uingereza,mchungaji Yuguda amesema waumini wapatao 16
wameuwawa katika jimbo la Kano ambapo kwa mujibu wa vyanzo vya ulinzi vimesema
watu wenye bunduki wakiwa kwenye pikipiki walirusha bomu ndani ya ukumbi wa chuo
kikuu ambao unatumika kufanyia ibada na kuwafanya waumini kukimbia huku watu
hao wakiwamiminia risasi na kuwaua.
Kutokana na hilo makanisa mengi kaskazini mwa nchi hiyo
yamefungwa waumini wanaogopa kwenda kuabudu kutokana na vitisho pamoja na
mauaji yanayofanywa na kundi hilo.Amesema katika shambulio lililopangwa
lilisababisha mchungaji mmoja wa kanisa la Church of Christ kufariki dunia
pamoja na waumini wake wanne wakati wakiwa kwenye ibada katika jimbo la
Maiduguri lililopo kaskazini mwa nchi hiyo ambapo hakuna kundi lililojitokeza
kuhusika na mauaji hayo ingawa tukio hilo halina tofauti na matukio mengine
ambayo yamekuwa yakifanywa na kundi la Boko haram.
Mchungaji mwingine aitwaye Fred Williams ameiambia Premier
kwamba alikuwa akiongoza moja ya makanisa lakini kutokana na mapigano pamoja na
mauaji namba ya waumini imekuwa ikipungua kila leo ingawa licha ya hayo kutokea
kikundi hicho hakitaweza kuuondoa Ukristo eneo hilo.Ambapo tangu kuanza kwa
mwaka huu watu 450 wamefariki dunia.
Nchi ya Nigeria imejigawa kwa upande wa kidini ambapo
Wakristo wengi wapo kusini mwa nchi hiyo huku waislamu wakiwa wengi kaskazini
mwa nchi hiyo,kundi la Boko haram ambalo lilitangaza vita na serikali ya jimbo
la kati la nchi hiyo,limekataa mazungumzo ya amani yaliyokuwa yameitishwa na
serikali kwa madai ya kutaka wafuasi wao wanaoshikiliwa kuachiwa huru,ikiwa ni
pamoja na kutambuliwa kwa sheria zao za kiislamu nchini humo.
Kanisa likiwa limeteketea kwa moto.
Baadhi ya wanawake wakilia kwa uchungu baada ya kupoteza
ndugu na jamaa kwenye mauaji yanayofanywa na kundi la Boko haram.
No comments:
Post a Comment