MPIGIE KURA CHRISTINA SHUSHO, IPIGIE KURA TANZANIA, IINUE AFRICA
VIVA SHUSHO....VIVA TANZANIA
VIVA SHUSHO....VIVA TANZANIA
Christina Shusho,akihojiana na mablogaz wa Kitanzania katika hotel ya The Atriums iliyoko Sinza Africa sana
Siku ya jana jioni mablogaz wanaomiliki blogu za Kikristo Tanzania,
Rulea Sanga, Uncle Jimmy, Sam Sasali, K-Junior, Martin Macele walikuwa
na mahojiano na Christina Shusho katika hotel ya The Atriums Sinza
Africasana kuhusiana na shindano kubwa lililoko machochoni pa mtumishi
wa Mungu Christina Shusho.
Christina Shusho alimshukuru Mungu kwa kuweza kumtumia kama chombo kufikisha ujumbe kwa jamii kwa njia ya uimbaji na pia kuweza kushiriki katika Gospel Music Awards Africa. Pia aliwashukuru mablogaz kwa kazi yao nzito wanayofanya kumtangaza katika blogs zao na kupoteza muda wao kwaajili ya kumuinua Kristo.
Aliwaomba Watanzania na Africa nzima kumchangua Christina Shusho ili
kuliwakilisha Bara la Africa,Tanzania na kumuweka Kristo juu ya vyote.
Christina Shusho ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania na amekuwa
chachu kwa waimbaji wenzake na kwa watanzania kwa uimbaji wake na
ujumbe naoutoa ambao umekuwa na mguso katika kukarabati imani za watu.
Christina Shusho anategemea ku-perform DAR LIVE siku ya jumapili,
kwahiyo amewaomba Watanzania wote kufika mahali pale na kuweza kumpigia
kura, kutakuwepo na mablogaz na kompyuta zao ambapo utakutana nao na
watakuelekeza jinsi ya kupiga kura....
Tukutane Jumapili Dar Live
1.Emmy Kosgei-Kenya
2.Dena Mwana – Congo
3.Ntokozo Mbambo- South Africa
4.Rebecca- UK
5.Gifty Osei- Ghana
6.Kefee -Nigeria
7.Onos Ariyo- Nigeria
8.Diana Hamilton-UK
9.Christina Shusho -Tanzania
10.Lara George- Nigeria
2.Dena Mwana – Congo
3.Ntokozo Mbambo- South Africa
4.Rebecca- UK
5.Gifty Osei- Ghana
6.Kefee -Nigeria
7.Onos Ariyo- Nigeria
8.Diana Hamilton-UK
9.Christina Shusho -Tanzania
10.Lara George- Nigeria
VIVA SHUSHO, VIVA TANZANIA-MSIKILZE SHUSHO ALIPOKUWA ANAONGEA NA MABLOGAZ JANA THE ATRIUMS HOTEL SINZA AFRIKASANA
USIKOSE MTUMISHI WA MUNGU...NJOO TUFANYE KAZI YA BWANA KWA KUM-SUPPORT MTANZANIA MWENZETU
KAMA ULIKUWA HUJUI KUHUSIANA NA MASHINDANO HAYA, TAFADHALI SOMA HAPO CHINI
Siku 18 zimebakia kabla ya pazia la upigaji kura kufungwa kwa waimbaji wa gospel barani Afrika, ambao wanawania tuzo mbalimbali kupitia Africa gospel music awards ambazo zinatarajiwa kutolewa siku ya jumamosi ya tarehe 7 mwezi wa 7 mwaka huu huko jijini London nchini Uingereza. Ambapo kama ilivyokuwa kwa mwaka jana mwimbaji wetu mmoja tu, ametutoa kimasomaso kwa kupendekezwa katika kuwania kupata tuzo hizo mwimbaji huyo si mwingine bali ni Christina Shusho, ambaye mwaka jana alitoka mikono mitupu lakini mwaka huu tukiungana kwa pamoja watanzania wote kwa kumpigia kura lazima atarudi na tuzo zote mbili alizopendekezwa kuwania.
Shusho yumo kwenye kuwania mwimbaji bora wa kike wa mwaka pamoja na mwimbaji bora wa mwaka Afrika ya mashariki, tuzo ambazo anawania na waimbaji wengine wanaofanya vyema kwenye gospel barani Afrika wakiwemo wakina Ntokozo Mbambo wa Afrika ya kusini na waimbaji wengine. Kikubwa ninachoweza kukwambia tukifanikiwa kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja kwa kumpigia kura atakuwa nanafasi kubwa ya kutwaa tuzo hizo, kwasababu waimbaji wengine wanaowania tuzo hizo wengi wao wanatoka nchi moja hali ambayo itafanya kura zao kugawana kitu ambacho kitatupa nguvu ya kumwezesha Shusho kurudi na tuzo kwani Tanzania nzima kura zetu tunaelekeza kwake.
Mikakati mbalimbali inafanywa ili kuhakikisha kila mtu anashiriki katika upigaji kura kwakuwa hauhitaji kulipa ili kupiga kura, kikubwa unatakiwa ujiandikishe kwenye tovuti ya shindano hilo ambayo maelekezo yake yapo chini ya habari hii, zaidi kama nilivyoandika mikakati inafanywa ili kuhakikisha watanzania wanashiriki kikamilifu katika zoezi hili katika siku 18 zilizobaki. Hapo jana bloggers walikutana na Christina Shusho katika hoteli ya Atriums iliyopo Sinza jijini Dar es salaam ili kupanga mikakati zaidi ya kuweza kupata tuzo hizo ambazo faida yake ni kumwinua Yesu pamoja na kuitangaza nchi yetu ya Tanzania duniani. Natumai umenielewa ili kupiga kura ingia kwenye link hii na kufuata maelekezo chini yake.
http://www.africagospelawards.com/nominate.html
AGMA 2012 VOTING GUIDELINES
1. Click on the 'VOTE NOW' button.
2. Register your email address, confirm and submit.
3. Check your email (inbox) and you will find the link to vote.
4. If you do not find the link in your email inbox, please check your junk mail folder.
5. Once you have connected to the voting page please make your selections and submit (you can only vote for one nominee from each category).
6. You do not have to vote in every category.
AGMA 2012 VOTING GUIDELINES
1. Click on the 'VOTE NOW' button.
2. Register your email address, confirm and submit.
3. Check your email (inbox) and you will find the link to vote.
4. If you do not find the link in your email inbox, please check your junk mail folder.
5. Once you have connected to the voting page please make your selections and submit (you can only vote for one nominee from each category).
6. You do not have to vote in every category.
ANGALIA BAADHI YA PICHA ZA BLOGGERS NA CHRISTINA SHUSHO HAPO JANA
Kikao kikiendelea
Blogger Victor kulia akinukuu jambo kutoka kwa Christina Shusho
Rulea Sanga alipoamua kupiga picha ya pamoja
Shusho akieleza jambo kwa mabloggers
Victor akizidi kuchangia nawazo yake
K-Junior akiwa busy na kuchukua maphotoz
Watumishi wa Mungu wakihakikisha kila kitu kinaenda sawa
Papaa akimuelezea Shusho mikakati ya mabloggerz kuhusiana na upigaji kura
Kutoka kulia ni Shusho, Martin Malecela pamoja na Victor Mboya wakimsikiliza Rulea Sanga akimpongeza Shusho kwa juhudi zake
Rulea Sanga akisikiliza kwa makini mchakato wa kupata tuzo ulivyo.
Mablogaz na mchungaji aliyoko upande wa kulia
K-junior wa kwanza upande wa kulia akimsikiliza mchungaji wa Vijana
Hakika kikao kilinoga wajameni.
Unclejimmy
Kikako kikiendelea na mabloggerz Tanzania waliojikita kumtangaza Kristo
''Inuka maana shughuli hii yakuhusu wewe, uwe na moyo mkuu, ukaitende (Ezra 10;4)''.
VIVA SHUSHO, VIVA TANZANIA.
No comments:
Post a Comment