Msama katika harakati za kusaka maharamia wa kazi za sanaa Tanzania
Msama akiwa na Mheshimiwa Rais Wa Jamhuri ya muunganao wa Tanzania
Dr. J.K Kikwete
Mmoja
wa mapromota maarufu wa muziki wa injili afrika mashariki na mkurugenzi wa
makampuni ya msama promotions, Mr Alex msama, ni miongoni mwa wageni maalum
watakao hudhuria katika tamasha la kumtukuza Mungu Baba pamoja na maombi
maalumu kwa ajili ya nchi yetu.
Msama
ambaye pia ndiye meneja wa mwalimu John Shabani, amethibitisha kuwepo katika
tamasha hilo, ili kuwatia moyo waimbaji na pia kuungana na mheshimiwa Mgeni
Rasmi Dr. Fenella Mukangara, Waziri wa Hahari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Tamasha
hilo litafanyika katika ukumbi wa kisasa katika kanisa la T.A.G Magomeni,
karibu na Hoteli ya Travetine, tarehe 10.06.2012
Viongozi
mbali mbali wa Serikali na mashirika yasiyokuwa ya serikali na madhehebu ya
dini, wakiwemo Mheshimiwa Rev. Dk. Getrude Rwakatare, Eng. Juliana Palangyo,
Mheshimiwa Martha Mlata (MB), Mheshimiwa Dk. Mary Mwanjelwa (MB), na wengine
wengi wamethibitisha kuhudhuria.
Mheshimiwa
Mbunge Martha Mlata ataimba pamoja na waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili
kama vile Mzee Makasy, Cosmas Chidumule, Stella Joel, Safi kutoka Rwanda,
Faraja Ntaboba kutoka Kongo, Upendo kilahiro, Christina Shusho, Addo November, Joybringes
kwaya, Revival kwaya ya T.A.G Magomeni, Albino group na wengine wengi.
Katika
tamasha hilo Mr Msama atatoa nasaha kwa waimbaji pia jinsi alivyojipanga
kutokomeza maaramia wa kazi za sanaa nchini na kuinua vipaji vya wasanii.
No comments:
Post a Comment