Utakumbuka kuwa wiki
iliyopita mwanamziki wa Injili Stara Thomas ambaye ameokoka na kuacha kuimba
mziki wa kidunia alilalamika kuwa wanamziki wa gospel hawampi support ya
kutosha. akimujibu Stara, John Shabani ambaye pia ni kiongozi wa chama
cha muziki wa injili Tanzania alisema atapata support ya kutosha
wala asihofu, maana wao ndiyo kazi yao aliongeza kusema kuwa wao wanafurahi
wanapoona wanamziki wanaokoka na kuamua kumwimbia Mungu, na kazi yao kama chama
kuwa kila mwimbaji amutukuze Mungu kwa njia ya nyimbo. akizungumza mbele ya
waziri wa Habari, vijana utamaduni na michezo Dr Fenella Mkangara alisema
wamesha fanya hivyo kwa wanamziki wengi kama akina Chidumule, Mzee makasi na
wengine wengi.
John Shabani akizungumzia ushirikano wa waimbaji wa injili mbele ya waziri wa habari, vijana , utamaduni na michezo
hayo yalizungumzwa katika Tamasha lililo andaliwa na
John shabani katika kanisa la TAG Magomeni. Stara Thomas nae alipewa nafasi ya
kusema machache na aliimba wimbo, waimbaji wengine ambao waliwahi kuimba kwenye
bendi za duniani na wakaokoka alikuwepo Chidumule na Mzee makasi ambao kila mtu
alimba na Chidumule alitumia ukongwe kwenye fani hivyo kwa nyimbo zake mpya
huku akiwa amejifua vyema kwenye upande wa kulitawala jukwaa tofauti na huko
nyuma. John shabani aliweza kukusanya waimbaji wengi sana ambao siku hiyo
waliimba akiwepo Upendo Kirailo ambae alitumia kipaji chake na sauti yake kwa
kuimba live wimbo wa zindonga ambao ulisababisha ukumbi wote kuchangamka.
wengine alikuwepo Faraja Ntaboba, Victor Haron, Stella Joeli, Kwaya ya
Joybrigers mikocheni B, kwaya ya Revival Magomeni. NK.
Mchungaji Danstan Kanemba wa T.A.G magomeni sambamba na Mheshimiwa Dr. Fenella Mukangara - waziri wa habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, wakisikiliza kwa makini Risala ya John Shabani
Stara akifurahia jambo na mkongwe wa Muziki, Mzee CosmaChidumule
Mwana muziki maarufu barani Afrika, mzee Makasy akiimba kwa hisia katika tamasha hilo
No comments:
Post a Comment