Pamoja
na serikali kuahidi kwamba juhudi zinachukuliwa ili kuleta
heshima na thamani ya wasanii na kazi zao nchini, lakini kinyume chake hivi sasa kazi feki zimezagaa hadi
vichochoroni.
Pamoja
na wasanii kujinyima, kukopa, na kuangaika hapa na pale ili kuweza kuandaa kazi
zao zinazogharimu mamilioni ya pesa lakini watu wanazitumia bila kutoa jasho
lolote, tena wanaziuza bei chee. Hili ni janga, huu ni msiba mkubwa kwa wasanii
nchini.
Uchunguzi
uliofanywa kwa muda mrefu umebaini
kuwapo kwa kundi kubwa la wafanyabiashara wanaouza kazi za Wasanii mbalimbali
zilizodurufiwa (duplicated) kwa bei ya chini na kusababisha wasanii
kutofaidika na kazi zao.
Nani
awafute machozi wasanii, nani alete matumaini kwa wasanii? Nani atuondolee
mtandao huu wa maharamia wa kazi za wasanii?
Ikiwa malaria haikubaliki, na uharamia huu
haukubaliki.
Chama cha muziki wa injili nchini (CHAMUITA)
kinapinga tabia hii
Kazi feki zikitayarishwa kuchomwa huko China
No comments:
Post a Comment