John akiwa katika picha na watoto wa kijiji cha makulu huko mvumi
John Shabani akiimba na kucheza
Katika kuhakikisha Injili ya Yesu inahubiriwa kwa njia ya
nyimbo na Neno l Mungu, John Shabani amekuwa akifanya ziara mbalimbali katika
mikoa na Vijiji kadhaa ndani na nnje ya nchi. Pia pamoja na kuimba na Neno pia
kutafiti maisha ya watu mbalimbali wakiwemo Vijana, watoto na hata watu wazima
wanaoishi katika mazingira magumu. Pia John amekuwa na mkakati wa kuibua na
kusaidia watoto na vijana wenye vipaji.
Katika kuhakikisha jamii inafikiwa kwa ukaribu zaidi, John
yuko mbioni kukamilisha usaili wa Tahasisi yake ya HOPE TRUST. Maombi yako
yanahitajika ili kukamilisha ndoto na maono haya makubwa.
Moja ya ziara ni ya wiki iliyopita ambayo amezunguka katika
mkoa wa dodoma hasa maeneo ya Mvumi . Mkutano
mkubwa uliandaliwa na Kanisa la T.A.G na kuhudhuriwa na mamia ya watu wakiwemo
maaskofu na wachungaji kutoka dini na madhehebu mbalimbali. Pia John aliweza
kufurahiya na watoto mbalimbali wanaosaidiwa na shrika la kimataifa la
Compation katika kijiji cha Makulu
John Shabani na mkakati wa kusaka na kuibua vipaji vya uimbaji vijijini
Wachungaji na maaskofu kutoka madhehebu mbalimbali wakimsikiliza John Shabani
No comments:
Post a Comment