Pages

29 October 2012

JOHN SHABANI AONGOZA MAMIA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU VYA IRINGA KATIKA SIFA



John Shabani akisalimiana na viongozi wa umoja wa wanafunzi wakristo wa vyuo vikuu iringa


SEMINA YA NENO LA MUNGU KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU IRINGA YAFANA.

Mamia ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iringa wamefurika katika ukumbi wa Ruco, katika semina ya Neno la Mungu. Ni semina iliyoandaliwa na umoja wa wanafunzi wakristo wa vyuo vikuu vya Iringa. Umoja huo ujulikanao kama Joint Fellowship umeundwa na wanafunzi wa vyo vikuu vitatu:
Chuo kikuu cha Ruaha (RUAHA UNIVERSITY COLLEGE – RUCO) 
Chuo kikuu cha Mkwawa (MKWAWA UNIVERSITY COLLEGE OF EDUCATION- MUCE) na chuo cha Tumaini (TUMAINI UNIVERSITY)
Chuo kikuu cha Ruaha (RUAHA UNIVERSITY COLLEGE – RUCO)
 Chuo kikuu cha Mkwawa (MKWAWA UNIVERSITY COLLEGE OF EDUCATION- MUCE)

chuo cha Tumaini (TUMAINI UNIVERSITY)


Watumishi wa Mungu, JOHN SHABANI, MCH. EFRAHIMU MWANSASU na Emmanuel Mgogo na kundi lake (Sayuni bandi) kutoka mbeya waligusa mioyo ya wanafunzi kwa nyimbo za sifa na kuabudu. Pia vikundi vya uimbaji kutoka vyuo vyote vitatu waliimba.

Mnenaji katika semina hiyo alikua Mwinjilisti wa kimataifa Daniel Mwankenja. Baada ya Kongamano hilo la siku mbili, uongozi wa umoja huo ukiongozwa na  mwnyekiti Mr. Lameck Mtaka na makamu wake mr. Emmanuel Kibona, wamewashukuru bwana John Shabani, Mch. Efrahimu Mwansasu na watumishi wote kwa kukubali kuungana nao na kuifanya semina hiyo kuwa ya Baraka na kuacha gumzo Iringa.

Lengo kuu la umoja huo ni kuhimarisha umoja wa kiroho kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iringa.





John Shabani akimtukuza Bwana

Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu iringa wakiongozwa na John shabani,  
wakicheza mbele za Bwana
Mch. Efrahimu Mwansasu akimtukuza BwanaJWajjWakabbbMMwa
Emmanuel Mgogo na kundi lake (Sayuni bandi) kutoka mbeya, Wakimwimbia Bwana

John shabani akiwa katika picha na viongozi wa umoja wa wanafunzi pamoja na mlezi wa semina hiyo Mhe. diwani wa Iringa na mwenyekiti wa CCM iringa mjini - Madame Jesca

22 October 2012

KITUO CHA TELEVISION CHA AGAPE MAARUFU KAMA ATN CHAVAMIWA





Wakati wimbi la kuvamiwa Makanisa likiendelea na Makundi ya watu wanaosaidikika ni Waislam, Usiku wa kuamkia leo majira ya saa 3 usiku kundi la Watu wanakadiriwa kuwa zaidi ya 20 wakiwa na mapanga walivamia kituo Cha Television Cha Agape, Maarufu kama ATN kwa lengo la kutana kuiba katika Kituo hicho.

Kundi hilo la watu waliokuwa na Silaha hizo lili wazidi nguvu walinzi na Kufanikiwa kuingia ndani ya Ofisi na kwenda kubeba Flat Screen ya nchi 32, Monitor pamoja na laptop. Kabla hata kundi hilo halijatawanyika mmoja wa walinzi alifanikiwa kubonyeza kitufe za "Alarm" kutaarifu mashirika ya Ulinzi ambayo yalifika kwa wakati pamoja na Polisi katika eneo husika.

Hii sio kawaida ya wezi kwenda kuiba na mapanga wakiwa zaidi ya 20, tena hawana hata gari la kubebea mizigo watakayoiba hasa unapoenda kuiba kwenye kituo cha TV kisha ukaiba Flat Screen na Laptop ambazo hata uswazi zipo. Yamkini hawa watu walikuwa wamekwenda kwa lengo lingine katika kituo hicho sababu hata Ofisi ya Mchungaji na Vitu vingine Vya thamani havikuguswa.

Hiki ni Kipindi cha kuwa macho, vibaka pia hawakawii kujifanya "Wanauamsho" wakafanya uhalifu kwa kutumia upepo uliopo sasa hivi wa Kuchoma Makanisa.

18 October 2012

JESUS FOR UNIVERSITIES - KUTOKA IRINGA




NI SEMINA KUBWA ITAKAYOFANYIKA KWA SIKU MBILI IRINGA MJINI, IMEANDALIWA NA UMOJA WA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU-IRINGA {JOINT FELLOWSHIP}  KWA USHIRIKIANO MKUBWA NA WACHUNGAJI WALEZI   MKWAWA,   RUCO NA TUMAINI


MAHALI: UKUMBI MKUBWA WA RUCO
SIKU: TAREHE 27 NA 28/10/2012 {J.MOSI NA J.PILI}


NYOTE MNAKARIBISHWA

 


 



TAMASHA KUBWA LA KUMTUKUZA MUNGU




HAIJAWAHI KUTOKEA, Waimbaji wazuri unaowajua, kwapamoja watamsifu na kumwabudu Mungu Baba. Waandaaji wa tamash hilo ni COME AND SEE PROMOTERS katika kanisa la TAG Magomeni mikumi jumapili hii ya tarehe 21 kuanzia saa 8 mchana hadi saa 12 jioni hakuna kiingilio hii sio yakukosa
 WOOOOTE MNAKARIBISHWA

17 October 2012

SEMINA SEMINA SEMINA



Tunawaletea zawadi kwa ajili ya kuujenga ufalme wa Mungu, ni semina ambayo itatujengea uwezo hasa 'men' katika nyakati hizi. Semina hii itafanyika tar 3/Nov 2012 katika ukumbi wa PJ, Kinondoni.
Wote mnakaribishwa