Pages

29 October 2012

JOHN SHABANI AONGOZA MAMIA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU VYA IRINGA KATIKA SIFA



John Shabani akisalimiana na viongozi wa umoja wa wanafunzi wakristo wa vyuo vikuu iringa


SEMINA YA NENO LA MUNGU KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU IRINGA YAFANA.

Mamia ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iringa wamefurika katika ukumbi wa Ruco, katika semina ya Neno la Mungu. Ni semina iliyoandaliwa na umoja wa wanafunzi wakristo wa vyuo vikuu vya Iringa. Umoja huo ujulikanao kama Joint Fellowship umeundwa na wanafunzi wa vyo vikuu vitatu:
Chuo kikuu cha Ruaha (RUAHA UNIVERSITY COLLEGE – RUCO) 
Chuo kikuu cha Mkwawa (MKWAWA UNIVERSITY COLLEGE OF EDUCATION- MUCE) na chuo cha Tumaini (TUMAINI UNIVERSITY)
Chuo kikuu cha Ruaha (RUAHA UNIVERSITY COLLEGE – RUCO)
 Chuo kikuu cha Mkwawa (MKWAWA UNIVERSITY COLLEGE OF EDUCATION- MUCE)

chuo cha Tumaini (TUMAINI UNIVERSITY)


Watumishi wa Mungu, JOHN SHABANI, MCH. EFRAHIMU MWANSASU na Emmanuel Mgogo na kundi lake (Sayuni bandi) kutoka mbeya waligusa mioyo ya wanafunzi kwa nyimbo za sifa na kuabudu. Pia vikundi vya uimbaji kutoka vyuo vyote vitatu waliimba.

Mnenaji katika semina hiyo alikua Mwinjilisti wa kimataifa Daniel Mwankenja. Baada ya Kongamano hilo la siku mbili, uongozi wa umoja huo ukiongozwa na  mwnyekiti Mr. Lameck Mtaka na makamu wake mr. Emmanuel Kibona, wamewashukuru bwana John Shabani, Mch. Efrahimu Mwansasu na watumishi wote kwa kukubali kuungana nao na kuifanya semina hiyo kuwa ya Baraka na kuacha gumzo Iringa.

Lengo kuu la umoja huo ni kuhimarisha umoja wa kiroho kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iringa.





John Shabani akimtukuza Bwana

Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu iringa wakiongozwa na John shabani,  
wakicheza mbele za Bwana
Mch. Efrahimu Mwansasu akimtukuza BwanaJWajjWakabbbMMwa
Emmanuel Mgogo na kundi lake (Sayuni bandi) kutoka mbeya, Wakimwimbia Bwana

John shabani akiwa katika picha na viongozi wa umoja wa wanafunzi pamoja na mlezi wa semina hiyo Mhe. diwani wa Iringa na mwenyekiti wa CCM iringa mjini - Madame Jesca

No comments:

Post a Comment