Mbunge wa singida viti maalum CCM na mwimbaji
mkongwe wa nyimbo za injili Mh. Martha
Mlata, amejitokeza kugombea nafasi ya mwenyekiti wa wazazi taifa kupitia
chama cha mapinduzi ccm. Mwana mama huyo ambaye mara zote amekua mstari wa
mbele katika kutetea na kupigania haki za kinamama, mabinti, wanafunzi,
wanamuziki na watu wenye ulemavu hakika ameonekana kupendwa na watanzania
wengi.
Katika kufuatilia, tumegundua, watu wengi wamekuwa
na matarajio makubwa kwamba akiingia
katika jumuhia hiyo, atasaidia sana kuendeleza mapambano na kupigania haki za
binadamu kama: Haki za kinamama, vijana, wazee, vikongwe, wasanii n.k.
Hakika maombi na dua za watanzania zinahitajika.
MBUNGE wa Viti Maalumu mkoa wa Singida, Martha Mlata (CCM), na mpango kabambe wa kukuza taaluma katika sekondari za kata.
Martha, ambaye amekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii nchini, ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya elimu vyenye thamani ya sh. milioni 16.5 kwa Sekondari Kata ya Ndago wilayani Iramba, Singida.
Msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati huo, ambao utazifikia sekondari mbalimbali mkoani hapa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo hivi karibuni, Martha alisema fedha hizo zimetumika kununua magodoro 42, mashuka jozi 42, unga wa sembe kilo 500, maharage kilo 100, mchele kilo 200 na magunia 10 ya mahindi.
Pia, alisema zitatumika kuweka umeme wa jua (Solar) shuleni hapo huku kiasi cha sh. milioni 1.1. zitatumika kulipia wanafunzi mitihani.
Martha alisema kuwa mpango wake huo umelenga katika kusaidia harakati za serikali kuboresha elimu nchini.
Martha Mlata akitokwa na machozi ya furaha alipotangazwa Mshindi namba mbili UWT Singida. uchaguzi huo uliofanyika mjini SingidaMoja ya matukio ya Mh. Martha Mlata (MP) akitoa mchango wake wa Kanga ili ziuzwe na kuchangia mfuko wa ATWID - 19/12/2009 ATWID Fundraising Event
Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Singida, Martha Mlata, akiteta jambo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Nape Nnauye
Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Davis Mwanyange kulia akizungumza na mbunge wa Viti Maalum Singida, Martha Mlata katikati na kushoto ni mbunge wa viti maalum Arusha Namelock Sokoine mara baada ya kutoka katika ukumbi wa Bunge
Mh. Martha mlata ambaye ni miongoni mwa walezi wa chama cha muziki wa injili Tanzania akiongozana na viongozi wa chama hicho, Mr Addo November, John Shabani, Mzee Cosmas chidumule, Mzee makasy na wengineo, wakimpongeza Mr Alex Msama kwa mchango wake wa kupambana na wezi wa kazi za wasanii nchini.
Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Martha Mlata, baada ya kuwasili mpakani mwa Wilaya ya Singida Vijijini akitokea Wilaya ya Manyoni leo Sept 16. Kulia ni Mbunge Mteule wa Viti maalum Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe
Mheshimiwa Rais akizungumza na Mh. Martha
Mlata
No comments:
Post a Comment