Meneja wa LAPF akiongelea faida za kujiunga na mfuko huo
Mfanyakazi wa LAPF akiwamakini kuandika maswali ya wasanii
Nahibu katibu mwenezi wa chama cha muziki wa injili bwana John Shabani akitoa mchango wake katika kuboresha maisha ya wasanii nchini
Waandishi wa habari hawakuwa mbali kurekodi matukio
Mgao wa kalenda za LAPF
Katibu wa shirikisho la muziki Tanzania akichangia jambo.
Wasanii wakijaza famu za kujiunga na mfuko huo
Mfuko
wa pensheni wa LAPF, watoa semina kwa wasanii ili waweze kujiunga na mfuko huo
na kufaidika na pensheni mbalimbali kwa maisha yao yasasa na ya baadaye.
Mafao
yanayotolewa na LAPF ni: Pensheni ya uzee, pensheni ya urithi, pensheni ya
ulemavu, mafao ya uzazi, mafao ya mazishi, mikopo ya nyumba pamoja na mikopo ya
wanachama kupitia saccos.
Kikao
hicho cha aina yake kimefanyika katika majengo ya LAPF MILLENIUM TOWER kijitonyama Dar es salaam, katika ukumbi wa
mikutano gorofa ya nane.
Mengi
yamezungumzwa na pia viongozi wa vyama mbalimbali vya wasanii wakiwemo wa
nyimbi za injili, walipata fursa ya kuuliza maswali na baada ya hapo tukio la
kujaza fomu za kujiunga na mfuko huo
liliendelea.
Kikao
hicho kimedhuriwa na viongozi na wawakilishi wa vyama hai vinavyounda
shirikisho la muziki Tanzania.
Baadhi
ya mapendekezo yaliyotolewa na wasanii, ni kuangalia suala suala la matibabu
pamoja na kujegewa nyumba za wasanii ili waendelee kulipia taratibu na baadaye
kuwa wamiliki halali wa nyumba hizo.
No comments:
Post a Comment