Pages

30 December 2012

Naibu Waziri Wa Habari Akutana Viongozi na Wadau Wa Muziki na Filamu Nchini




Kwa mara nyingine tena kimefanyika kikao kikubwa kati ya wadau na viongozi mbalimbali wa muziki na filamu na Mheshimiwa Makala (Naibu waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo)
Kikao hicho kimefanyika katika  ukumbi mdogo uliopo gorofa ya tisa katika ofisi za wizara hiyo. Lengo la kikao hicho ni wasanii kufahamishwa jinsi serikali ilivyojipanga kuwasaidia wasanii wa Tanzania, ili wanufahike na kazi zao na kuwajengea heshima zaidi.
Katika kikao hicho chama cha muziki wa Injili Kimewakilishwa na  Addo November, John Shabani, Bahati Bukuku, Upendo Kilahiro, Cosmas Chidumule, George Mpella na Stella Joel.
  Mwimbaji wa nyimbo za Injili Bahati Bukuku, akizungumza wakati wa Mkutano na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makalla, jijini Dar es


Msanii JB akizungumza wakati wa Mkutano huo leo jijini, Dar es Salaam
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makalla akiwa na baadhi ya wasanii



 Naibu Waziri, Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla akizungumza na wasanii alipokutana nao katika Ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo

29 December 2012

VIONGOZI WA CHAMUITA WAMTEMBELEA MZEE MAKASY

Viongozi wa Chama chamuziki wa injili Tanzania wakiongozwa na Mchungaji Cosmas Chidumule, wamemtembelea mzee Makasy ili kumjulia hali pamoja na kumkabidhi mchango kwa ajili ya matibabu. Mwimbaji huyo mkongwa na mshauri wa chama cha muziki wa injili Chamuita Tanzania, amekuwa akisumbuliwa na tatizo la macho. Viongozi waliomtembelea Mzee makasy ni: Addo November Mwasongwe, John shabani, Stella Joel pamoja na Mzee cosmas Chidumule. Endapo utaguswa kumchangia chochote mzee makasy, wasiliana na viongozi wa chama cha muzili wa injili. Mungu akubariki

27 December 2012

NEW YEAR MESSAGE TO MY FRIENDS



Let the next twelve months be the most amazing days that one can have, May you achieve all your aspirations, May this year shower upon you the choicest blessings that you could ever hope for, May the New Year dispel any clouds of gloom from your life. May you have a stress free, May you have a year that is filled with love, laughter, brightness and hope, May the New Year bring with it all things beautiful and lovely. Have a blessed New Year.

26 December 2012

PADRI wa Kanisa Katoliki Mjini Zanzibar amepigwa risasi




PADRI Ambrose Mkenda wa Kanisa Katoliki, Mjini Zanzibar amepigwa risasi na watu wasiojulikana nje ya nyumba yake juzi saa 1:45 jioni wakati akitokea kanisani.
Hili ni tukio la kwanza katika historia ya Zanzibar kwa kiongozi wa kanisa kushambuliwa wakati wa Krismasi, lakini ni tukio la pili kwa kiongozi wa dini kushambuliwa mwaka huu.
Hivi karibuni, Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga alimwagiwa tindikali iliyomjeruhi vibaya usoni na kifuani na watu wasiojulikana. Shambulio hilo lilimlazimu kiongozi huyo kwenda kutibiwa India ambako ameambiwa anapaswa kuripoti hospitalini kila baada ya miezi sita.
Habari zilizopatikana jana zimeeleza kuwa Mkenda ambaye ni Paroko wa Parokia ya Mpendae, alipigwa risasi begani na shingoni na afya yake si nzuri.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Aziz Juma Mohammed alisema jana kuwa majeraha hayo yamemsababishia kutokwa na damu nyingi.
Alisema baada ya shambulio hilo, Padri Mkenda alipelekwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, Zanzibar. Hata hivyo, padri huyo alisafirishwa kwa ndege jana hadi Dar es Salaam ambako amelazwa katika chumba cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU), katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.


Kamanda Aziz alisema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, lakini akabainisha kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa alipigwa risasi baada ya watu hao kumshuku kuwa alikuwa na fedha za sadaka.
“Father Mkenda kitaaluma ni mhasibu na amekuwa akishika makusanyo ya fedha pale kanisani. Sasa huenda wahalifu hao waliona amechukua fedha na ndipo walipomfuata na kumpiga. Lakini hata hivyo, huo bado ni uchunguzi wa awali tu,” alisema Kamanda Aziz na kuongeza:


“Waliofanya tukio hili wamelifanya kwa madhumuni gani, ni swali gumu kujua sasa. Inawezekana kuna mambo mengine zaidi ya watu hao kutafuta fedha. Uchunguzi ukimalizika tutajua cha kufanya.”


Kamanda Aziz alisema walipata taarifa za tukio hilo saa 2:00 usiku na polisi walikwenda katika eneo hilo la Francis Maria anakoishi Padri Mkenda.


“Tulipofika tukakuta maganda mawili ya risasi za bastola na upande wa kulia wa kioo cha gari yake (padri) kuna damu katika viti vyake,” alisema Kamanda Aziz.
Alisema baadaye padri huyo alipelekwa hospitalini kwa ajili matibabu ambako madaktari walifanikiwa kumtoa mabaki ya risasi mwilini kabla ya jana kupelekwa Muhimbili.
“Tumempokea padri huyo saa 4:20 asubuhi leo (jana). Tulianza kumchunguza afya yake, baadaye kumfanyia uchunguzi kisha kumchukua kipimo cha CT Scan ili kubaini ilipo risasi hiyo,” alisema, mkurugenzi wa zamu katika hospitali hiyo, Agnes Mtawa.


Source: Mwananchi

21 December 2012

HATMAYE ALBUM YA DEBORA SHABANI IKO TAYARI


Kwa wale wapenzi wa nyimbo za Debora Shabani, sasa album hiyo ijulikanoayo kwa jina la Amesikia kilio chako iko tayari kwa mfumo wa Audio huku tukiendelea na mchakato wa kutengeneza video. Unaweza ukaipata kwa bei ya jumla na rejareja. Mungu akubariki.

20 December 2012

KONGAMANO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI l LATIKISA DAR ES SALAAM, PIA CHAMUITA WAIOMBA SERIKALI KUWABANA MAHARAMIA WA KAZI ZA MUZIKI




          Waimbaji mbalimbali na wadau wa muziki wa injili ndani ya ukumbi wa wanyama hotel sinza





                                                                           Mchungaji Abel
 Kongamano kubwa la waimbaji wa Muziki wa Injili lililo andaliwa na chama cha Muziki wa Injili Tanzania "CHAMUITA" limefanyika likiwa na lengo la kutambulisha viongozi wapya wa chama cha muziki wa Injili Tanzania pamoja na kutaja malengo ya chama.
Katika kongamano hilo CHAMA cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA), kimeiomba serikali kuhakikisha inasimamia vema kazi zao ili zisihujumiwe, na wao waweze kupata faida kupitia kazi hizo za Mungu.
Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa semina ya kutoa elimu kwa wadau mbalimbali juu ya kazi zao jijini Dar es Salaam jana, Rais wa chama hicho, Addo Mwasongwe Mwl John Shabani, Bahati bukuku pamoja na waimbaji mbali mbali kwa nyakati tofauti, wametoa ombi hilo kutokana na serikali kuwa na mamlaka makubwa hapa nchini ya kulisimamia suala hilo.
“Serikali ina uwezo mkubwa wa kuhakikisha sisi wasanii tunanufaika na kazi zetu, kwa kuwa wao wakianza kuwakamata ambao wanatuhujumu na kuwachukulia hatua, nina imani mambo haya yataisha na sisi tutazidi kujivunia kazi zetu ambazo zinaleta ajira hapa nchini,” alisema Mwasongwe.
Aidha, Mwasongwe alisema wanachukizwa na kitendo cha Wakristo kufanya wizi wa kazi za Mungu, wakati kila Jumapili huenda kwenye ibada na kumtukuza.
“Tunasikitishwa sana kwa kuwa miongoni mwa wezi wa kazi zetu na Wakristo nao wamo, inauma sana, mtu anakwenda kwa wale ‘wanaobani’ CD na kumuomba nichanganyie nyimbo ya Bukuku, Mkone na wengine, wakati yeye kama Mkristo anatakiwa kuwa mstari wa mbele kuacha kufanya hivyo. Hivyo basi tuna imani serikali itatusaidia,” aliongeza.
Katika hatua nyingine, CHAMUITA kiliwatambulisha viongozi wapya ambao ni Addo Mwasongwe (Mwenyekiti), Mchungaji Joseph Malumbu (Makamu Mwenyekiti), David Mwamsojo (Katibu), Stella Joel (Katibu Msaidizi), John Shabani (Naibu Mwenezi), na Upendo Kilahiro (Mweka Hazina), huku wajumbe wa Kamati Kuu wakiwa zaidi ya 60, wakiongozwa na Mbunge Martha Mlata, Christina Shusho na Bahati Bukuku.pamoja mh. Martha mlata (Mbunge wa singida viti maalum CCM na Mr Alex Msama ambao ni walezi wa chama hicho.


Miongoni mwa madhumuni ya semina hiyo ni kulinda utamaduni wa Tanzania na heshima ya muziki huo, kuhamasisha maendeleo ya muziki huo na nyanja zake nyingine, kuwa na chombo cha kuwezesha mawasiliano kati ya watu na vikundi katika kupeana taarifa mbalimbali na mengine mengi ambapo iliudhuriwa na wanamuziki wengi wa injili hapa nchini.
        Lulyalya Sayi Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki akieleza umuhimu wa mfuko wa LAPF               
 
                                          Abubakari Ndwaka Meneja Mafao wa LAPF.  

Katika kongamano hilo liliudhuriwa na viongozi wa mfuko wa pensheni wa LAPF ambao ndio waliokuwa wadhamini wakuu wa kungamano hilo. Mfuko huu ulizungumzia umuhimu kwa waimbaji wa muziki wa injili kujiunga nao kama sehemu mojawapo ya wao kuwekeza katika maisha ya baadae, pia kutoa fursa kwao kujipatia mikopo ya nyumba na kuwekeza katika akiba yao ya baadae.



Pia kampuni ya Grace products ltd inayojihusisha na kutengeneza mafuta ya ngozi, shampoo, sabuni na bidhaa mbalimbali zisizokuwa na kemikali, walikuwepo katika kongamano hilo wakiwaelimisha waimbaji na watumishi wa Mungu kutumia bidhaa nzuri kwaajili ya kulinda miili yao. Pia afisa kutoka TRA alifafanua jinsi serikali ilivyojipanga kuwasaidia wasanii nchini. Kongamano hilo limehudhuriwa pia na wachungaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi akiwemo Nabii Machibya kutoka wingereza.