Waimbaji mbalimbali na wadau wa muziki wa injili ndani ya ukumbi wa wanyama hotel sinza
Mchungaji Abel
Kongamano kubwa la waimbaji wa Muziki wa
Injili lililo andaliwa na chama cha Muziki wa Injili Tanzania "CHAMUITA" limefanyika likiwa na lengo la kutambulisha
viongozi wapya wa chama cha muziki wa Injili Tanzania pamoja na kutaja malengo
ya chama.
Katika kongamano hilo CHAMA cha
Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA), kimeiomba serikali kuhakikisha inasimamia
vema kazi zao ili zisihujumiwe, na wao waweze kupata faida kupitia kazi hizo za
Mungu.
Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa
semina ya kutoa elimu kwa wadau mbalimbali juu ya kazi zao jijini Dar es Salaam
jana, Rais wa chama hicho, Addo Mwasongwe Mwl John Shabani, Bahati bukuku
pamoja na waimbaji mbali mbali kwa nyakati tofauti, wametoa ombi hilo kutokana
na serikali kuwa na mamlaka makubwa hapa nchini ya kulisimamia suala hilo.
“Serikali ina uwezo mkubwa wa
kuhakikisha sisi wasanii tunanufaika na kazi zetu, kwa kuwa wao wakianza
kuwakamata ambao wanatuhujumu na kuwachukulia hatua, nina imani mambo haya
yataisha na sisi tutazidi kujivunia kazi zetu ambazo zinaleta ajira hapa
nchini,” alisema Mwasongwe.
Aidha, Mwasongwe alisema
wanachukizwa na kitendo cha Wakristo kufanya wizi wa kazi za Mungu, wakati kila
Jumapili huenda kwenye ibada na kumtukuza.
“Tunasikitishwa sana kwa kuwa
miongoni mwa wezi wa kazi zetu na Wakristo nao wamo, inauma sana, mtu anakwenda
kwa wale ‘wanaobani’ CD na kumuomba nichanganyie nyimbo ya Bukuku, Mkone na
wengine, wakati yeye kama Mkristo anatakiwa kuwa mstari wa mbele kuacha kufanya
hivyo. Hivyo basi tuna imani serikali itatusaidia,” aliongeza.
Katika hatua nyingine, CHAMUITA
kiliwatambulisha viongozi wapya ambao ni Addo Mwasongwe (Mwenyekiti), Mchungaji
Joseph Malumbu (Makamu Mwenyekiti), David Mwamsojo (Katibu), Stella Joel
(Katibu Msaidizi), John Shabani (Naibu Mwenezi), na Upendo Kilahiro (Mweka
Hazina), huku wajumbe wa Kamati Kuu wakiwa zaidi ya 60, wakiongozwa na Mbunge
Martha Mlata, Christina Shusho na Bahati Bukuku.pamoja
mh. Martha mlata (Mbunge wa singida viti maalum CCM na Mr Alex Msama ambao ni
walezi wa chama hicho.
Miongoni mwa madhumuni ya semina hiyo ni kulinda
utamaduni wa Tanzania na heshima ya muziki huo, kuhamasisha maendeleo ya muziki
huo na nyanja zake nyingine, kuwa na chombo cha kuwezesha mawasiliano kati ya
watu na vikundi katika kupeana taarifa mbalimbali na mengine mengi ambapo
iliudhuriwa na wanamuziki wengi wa injili hapa nchini.
Lulyalya
Sayi Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki akieleza umuhimu wa mfuko wa LAPF
Abubakari Ndwaka Meneja Mafao wa LAPF.
Katika kongamano hilo liliudhuriwa na viongozi wa mfuko wa pensheni wa LAPF ambao ndio waliokuwa wadhamini wakuu wa kungamano hilo. Mfuko huu ulizungumzia umuhimu kwa waimbaji wa muziki wa injili kujiunga nao kama sehemu mojawapo ya wao kuwekeza katika maisha ya baadae, pia kutoa fursa kwao kujipatia mikopo ya nyumba na kuwekeza katika akiba yao ya baadae.
Pia
kampuni ya Grace products ltd inayojihusisha na kutengeneza mafuta ya ngozi, shampoo,
sabuni na bidhaa mbalimbali zisizokuwa na kemikali, walikuwepo katika kongamano
hilo wakiwaelimisha waimbaji na watumishi wa Mungu kutumia bidhaa nzuri
kwaajili ya kulinda miili yao. Pia afisa kutoka TRA alifafanua jinsi serikali
ilivyojipanga kuwasaidia wasanii nchini. Kongamano hilo limehudhuriwa pia na
wachungaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi akiwemo Nabii Machibya kutoka
wingereza.
No comments:
Post a Comment