BAHATI BUKUKU HAJAFA
NI MZIMA KABISA
CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI NA WATU MBALIMBALI WATOA
TAMKO KALI
Bahati Bukuku
Bahati, Rose Muhando na Mwl John Shabani
Bahati na Jenifer mgendi
Habari za uzushi
za kifo cha Bahati bukuku
zimewashtua watanzania na watu mbalimbali duniani. Chama cha muziki wa injili Tanzania, kimefanya kazi kubwa ya
kukanusha uzushi huo, ukizingatia kuwa Bahati ni kati ya waimbaji wanaofanya
vizuri katika tasnia ya muziki wa Injili pia ni kiuongozi katika chama cha
muziki wa injili Tanzania (Chamuita). Hivyo chama cha muziki wa Injili
kimekemea tabia hiyo ambayo imekuwa ikijirudia mara kwa mara. Sisi tunasema
hafi mtu na injili inasonga mbele.
Baadhi ya watu
waliokemea tabia hiyo ni :
ADDo November
(Mwenyekiti wa chama cha muziki wa injili)
.....Ni Aibu kwa wanaoeneza Maneno ya Uongo dhidi ya Bahati
Bukuku, kiukweli Bahati Bukuku ni Mzima wa Afya na nimeongea naye muda si mrefu
natoaa wito tuziddi kuwaombea Wanamuziki wa Injili na kuwafunika kwa Damu ya
Yesu...!! Hafi Mtu na Injili Inasonga In Jesus Name...!!
John Shabani (Naibu
katibu mwenezi wa chama na mwalimu wa muziki wa Injili Afrika Mashariki) Hakika
hii si tabia nzuri na tena imekuwa ikijirudia si kwa Bahatati tu, pia hata kwa
waimbaji na wasanii mbalimbali nchini. Sisi tunakemea hali hii.
Producer Eck: Hakika habari hizi zilinishtua sana,
ukizingatioa ngoma mpya ya bahati ya Dunia haina huruma niliyoitengeneza hapa
studio ndio kwanza inafanya vizuri. Hivyo nililazimika kuwasiliana nia kiongozi
wa Chama cha muziki wa Injili bwana John shabani, majibu ya shabani yalikuwa
kwamba Bahati ni mzima kabisa. Lakini pia ilibidi nimtafute bahati, akaniambia
waambie mimi sijafa.
Deborah
Harold roho ya mauti haina mamlaka kwa waimbaj wa gospel wote katika
jina la yesu aliye hai,amen
Rachel
Sozigwa hafu kwa nini watu huwa wanajifanya wanajua watu sana na
kuwasingizia vitu vya uongo?hata kama umjui mara kaolewa kaachwa anaumwa sana
haipendezi loh
Benedicta Mrema
N a kwanini umtangulize mwenzio...kama umechoka kuishi tangulia wewe,tuache
sisi tufanye kazi tuliyoitiwa KUHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE KWA NAMNA YOYOTE
ILE, alaaaaaa!
Mtitu
Alex Mdidi Lazima mkubali kuwa tupo duniani na wengi wanaenenda kwa
kumfuata mkuu wa anga na matendo yake. Watasema mengi lkn watahukumiwa kuwa ni
wakosaji
Jordan Mwanjala ASANTE MUNGU "NAMI
NILIPOSIKIA NILISISTUKA SANA NA IKANILAZIMU NIINGIE FB SIKUKUTA KITU IKABIDI
NIWAULIZE IR NA NEG
Jordan
Mwanjala NAO AWAJANIJIBU NASHUKURU KWA TAALIFA YAKO MUNGU AMUONGEZE
SIKU BUKUKU SAUTI YAKE NZITO IZIDI LINDIMA KTK KUTANGAZA NEN
Jordan
Mwanjala NA IWAPO KAMA ANA ANAUMWA MUNGU AMUONDOLEE MAUMIVU
AMUONGEZE NGUVU ILI AWEZE KULITANGA NENO LA MUNGU AMINA
Jordan
Mwanjala NA IWAPO KAMA ANAUMWA MUNGU AMUONDOLEE MAUMIVU AMUONGEZE
NGUVU ILI AWEZE KULITANGAZA NENO LA MUNGU AMINA
Obby
Mwakyoma kaka nashukuru.,yatupasa tuombeane uzima na afya tele huku
tukilindwa na damu ya yesu
Neema Mkakata
mmmh huyo ni shetani tu baba wa uongo anajaribu kupindisha mambo,lkn Mungu
mwema awafunike wanamuzik wa gospel ktk damu ya Yesu na roho za umauti.dah
niliona jana post moja nilishtuka sana Na nkakosa amani kweli Dunia haina
huruma
Thomas
Luvanda Aisee afadhali umetufahamisha ukweli maana mm nimepata sms 3
alafu nyingine imenifikia kwamba rose muhando kapata ajali aisee mungu
awafunike na kuwalinda roho ya mauti kifo imeshindwa haiwezi kuwapata kwa jina
la yesu kristo wa nazaret amen
Bilionear
Macdaut Shayo BRO ADDO MI KIUWELI NIMESHTUKA SANA KIASI NILIKUWA
NIMEKAAA NILISIMAMA GHAFLA NA ZAIDI KILICHONIUA KABISA NIKAJUA NI KWELI
NAFUNGUA REDIO UWAPO NAKUTANA NA NYIMBO YAKE ILE YA DUNIA SINA HURUMA
KILICHONISTUA NI UZUSHI NI MTANGAZAJI ALIKUWA ANACHEKA NA ANARAHA NA TENA
ANASEMA NASIKILIZA MOJA YA NYIMBO ZA BAHATI HISTORIA YA KWELI ILA ANACHEKA
NIKAJUA UONGO ASANTE KWAKULIWEKA HILI KUWA NI UONGO KESHO NITALIKEMEA NIKIWA
KWENYE KIPINDI CHANGU PALE ATN TV SIO VIZURI KABISAA BAHATI UBARIKIWE MAMA
MUNGU AKUWEKE DAIMA NA UISHI MAISHA MAREFU KABISAA WANAOSEMA WABAKIE MIDOMO
WAZI
No comments:
Post a Comment