Kushoto
ni Upendo Nkone,Upendo Kilahilo,Bahati Bukuku,Rose Muhando,Christina Shusho.
David Robert akihojiwa na Samweli Sasali.
Ni
kawaida kusikia Kanisa flani lina fanya maombi kwajili ya Taifa au Mkutano
fulani ulioandaliwa kwa sababu ya kuombea nchi. Hivi ndivyo imetokea kwa baadhi ya waimbaji
wa muziki wa injili kukutana na kutengeneza wimbo mmoja wenye lengo la kuiombea
amani Taifa la Tanzania, hii ni kwa mujibu wa David Robert ambaye ndiye msimamizi wa
shughuli nzima ya uandaaji wa wimbo huo.
WAZO LA KUWAKUTANISHA
WAIMBAJI
"Siku
Moja nikiwa na Bahati Bukuku Likatujia Wazo Kwanini Tusifanye Wimbo Wa Kuombea
Amani Tanzania, It was very strong in our hearts, then tukaanza utaratibu
wa Kuwatafuta Wanamuziki na Kuwasiliana nao walipo, Ilipata Muitikio Mkubwa
sana, Rose Muhando, Bahati Bukuku, Florah Mbasha na wengine wengi unaowajua
tukakaa pamoja tuka record, na Jana ndio tumemaliza shooting ya wimbo Huo, kwa
sasa tunasubiri tu Kukamilika Kisha tutauweka Wakfu wimbo huo"..Haya
yalikuwa ni baadhi ya Maneno Ya David Robert akihojiwa na Samweli Sasali.
No comments:
Post a Comment