John shabani akikabidhiwa cheti na askofu kitonga
Band ya matarumbeta ikiwaongoza wahitimu kuelekea ukumbini
Bishop Kitonga sambamba na Mtume Prosper Ntepa
Mmoja wa watoto wanaolelewa kihuduma na John shabani
Picha na mwakilishi wa Isom kutoka Marekani, Dr Lee
Hatimaye maelfu ya watu wameshuudia mahafali ya kwanza ya
chuo cha kimataifa cha huduma (International School of Ministry – Isom). Chuo hicho chenye makao makuu huko California
Marekani, mpaka sasa kimeenea katika
nchi 145 duniani na kufundishwa katika lugha zaidi ya 65 za mataifa mbalimbali.
Mahafali hayo ya kwanza kwa Tanzania yameacha historia,
yakiwa yamehudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi. Mgeni Rasmi alikuwa Askofu Arthur Kitonga (Mwanzilishi
wa makanisa ya Redeemed, kanisa linaloongoza kwa wingi nchini Kenya na kuenea
duniani kote). Pia aliyeleta vyeti kutoka marekani ni Dk.
Lee (Mwakilishi wa isom kutoka Marekani)
Mgeni rasmi alimwaga sifa za chuo hicho,kwamba mtaala
wake ni wa kimataifa na kinafundishwa na watumishi wenye huduma zinazotikisa
Dunia. Baadhi ya waalimu wanaofundisha katika chuo hicho ni: Mwinjilist Rehnard
Bonnke, Joyce Meyen, T. L Hosborn na wengine kibao.
Hivyo watu mbalimbli wamehamasishwa kujiunga na chuo hicho
chenye mtaala wa kimataifa.
No comments:
Post a Comment