Pages

29 July 2013

MAZOEZI YA KUSIFU NA KUABUDU CHINI YA MWALIMU JOHN SHABANI NA WAALIMU WENGINE KWA AJILI YA MAANDALIZI YA MKUTANO WA MWINJILISTI BONNKE YAENDELEA VIZURI


 Zaidi ya waimbaji 500 kutoka makanisa mbalimbali, wakimsikiliza mwalimu John shabani, alipokuwa akielekeza kuhusu sifa na mbinu za kuwa mwimbaji bora


Mratibu wa mikutano ya Bonnke  barani Afrika, Mwinjilisti Pascal Ado kutoka Togo, akipongeza mazoezi pamoja na kuongea na waimbaji wanaoendelea kuhudhuria mazoezi hayo


Je wewe ni mwimbaji, kwaya au kikundi, mnakaribishwa kuungana waimbaji wengine kwa ajili ya maandalizi ya mkutano mkubwa wa injili utakaohubiriwa na muhubiri wa kimataifa Dr. Rehinard Bonnke
Ni jumamosi hii, pale magomeni mikumi, katika kanisa la T.A.G. Bado tuhitaji waimbaji, ili kukamilisha idadi ya watu 5000




22 July 2013

UZINDUZI WA KIKUNDI CHA KUSIFU NA KUABUDU KATIKA MKUTANO WA MWINJILISTI BONNKE WAFANYIKA DAR, KARIBU WAIMBAJI 500 WAJISAJILI.

 Zaidi ya waimbaji 500 ktoka kwaya, vikundi na waimbaji binafsi wakiimba kwa pamoja katika uzinduzi wa kuandaa kikundi cha sifa, kitakachotumika kwenye mkutano wa mwinjilisti Bonnke

Mratibu wa mikutano ya Bonnke  barani Afrika, Mwinjilisti Pascal Ado kutoka Togo, akiongea na waimbaji




 Mwalimu John Shabani, akisimamia zoezi hilo

Waimbaji  5000 wanahitajika ili kukamilisha kikundi cha kusifu na kuabudu, kitakachoongoza sifa katika mkutano wa Bonnke, unaotarajiwa kufanyika  kuanzia tarehe 21 mwezi ujao.

Akiongea na mamia ya waimbaji na wanamuziki, mratibu wa mikutano ya Bonnke  barani Afrika, Mwinjilisti Pascal Ado kutoka Togo, amesifia sana uimbaji wa Tanzania na kuwaasa waimbaji kufanya huduma hiyo kwa moyo wote. Amesema mkutano huo utatazamwa  katika nchi mbalimbali duniani, hivyo unadhifu na uchangamfu unahitajika sana. Pamoja na hayo, amependekeza  aina ya nyimbo zinazohitajika na kujiandaa kuwa na sare ya aina ya mavazi ya ki-Afrika


JE WEWE NI MWIMBAJI BINAFSI, KWAYA AU KIKUNDI, UNAKARIBISHWA KUUNGANA NA WAIMBAJI WENGINE KWA AJILI YA KUANDAA TIMU HIYO 

Ni jumamosi hii, pale magomeni mikumi, katika kanisa la T.A.G. Bado tuhitaji waimbaji.

18 July 2013

MCHUNGAJI DK. GETRUDE RWAKATARE AONGOZA MAOMBI YA KUWEKA WAKFU ALBAM YA MWIMBAJI EMMANUEL MGOGO



Ile album ijulikanayo kwa jina la “Msikilize Mungu” ya kwake Emmanuel  Mgogo, imewekwa wakfu katika kanisa la Mikocheni B’ Assemblies of God. Album hiyo iliyorekodiwa katika studio ya Eck Production, imekuwa gumzo  na hasa ule wimbo wa Msikilize Mungu.

Kabla mwimbaji huyo hajaanza kuimba jumapili hii, aliweza kuzileta Cd kadhaa madhabahuni, ndipo Mchungaji kiongozi wa Mlima wa moto pamoja na jopo la watumishi walipoziinua na kuziweka nyimbo hizo wakfu kwa maombi, ili Mungu amtumie zaidi kijana huyo.

Endelea kunyenyekea, ili Mungu akuinue zaidi.

13 July 2013

NIMEGUSWA SANA NA HABARI HII YA WAIMBAJI WA INJILI AFRIKA YA KUSINI WALIPOKUSANYIKA NJE YA HOSPITALI ALIYOLAZWA MANDELA



Solly na Deborah katikati wakiimba na wenzao nje ya hospitali kumtakia afya njema mzee Mandela

Kundi la waimbaji muziki wa injili nchini Afrika ya kusini jumatano wiki hii walikusanyika nje ya hospitali ya Medi-clinic Heart alikolazwa baba wa taifa hilo mzee Nelson Mandela jijini Pretoria akipatiwa matibabu ya ugonjwa ambapo walikuwa wamebeba maua kumtakia afya njema.

Kundi hilo la wanamuziki wapatao 10 wakiongozwa na mchungaji Solly Mahlangu na mwanamama Debora Frazer na waimbaji wengineo walikaririwa wakisema kuwa, kama waimbaji muziki wa injili nchini humo walifika hospitalini hapo kuonyesha upendo wao na heshima kwa Rais huyo mstaafu ambaye wanasema bado wanamuhitaji, ambapo walitumia muda nje ya hospitali hiyo wakiimba pamoja na kufanya maombi kwa kiongozi huyo mstaafu.

Aidha mwimbaji anayeitwa Zanele Mbokazi amesema wao hawana fedha wala dhahabu lakini wanalo jina la Yesu ambalo ndio wanalolitoa kwa mzee Madiba na familia yake.Kwa upande wake Deborah amelitaka taifa hilo kuendelea na maombi juu ya mzee Madiba kwakuwa nchi hiyo na dunia kwa ujumla bado wanamuhitaji mzee Madiba "Ni baba wa kwetu sote, Mungu ampe maisha marefu zaidi duniani", amesema Deborah

Ni siku ya 35 tangu mzee Madiba kupelekwa hospitalini hapo kwa matibabu kutokana na maradhi ya mapafu yanayomfanya kushindwa kupumua vyema. Huku mzozo ambao ulikuwa umeigubika familia yake kuhusiana na masuala ya maziko yameonekana kumalizwa kama wajukuu wa mzee huyo walivyonukuliwa na vyombo vya habari wakijibu maswali ya watu waliokuwa wakiwauliza maswali kwenye mtandao wa twitter.

10 July 2013

MAELFU YA WATU WAENDELEA KUFUNGULIWA KATIKA SEMINA INAYOENDELEA KATIKA KANISA LA MIKOCHENI B’ ASSEMBLIES OF GOD - MLIMA WA MOTO



 Mwimbaji wa kimataifa, Sarah K, akimtukuza Mungu akitika siku ya ufunguzi wa semina

 Mchungaji Getrude Rwakatare akiombea watu

Mnenaji wa semina, Askofu Mrisa

 Sehemu ya umati wa watu wanaoendelea kuhudhuria smina hiyo

 Mchungaji Msaidizi, Noah Lukumai akifungua kwa maombi

Papag Mphella akiweka mambo sawa

                                                    Mwinjilisti Stanley akimtukuza Bwana
Ni siku nane za kukupeleka kwenye hatma yako. Haijawahi kutokea, moto wa Roho Mtakatifu, unateketeza kila roho chafu, kila mikosi na balaa na kila kifungo. Mnenaji katika semina hiyo ni Muhubiri wa kimataifa, Askofu Mrisa akishirikiana na mwenyeji wake Dk Getrudw Rwakatare 

Panga kuhudhuria semina hiyo. 
Kwa mawasiliano zaidi: 0715524441