Zaidi ya waimbaji 500 ktoka kwaya, vikundi na waimbaji binafsi wakiimba kwa pamoja katika uzinduzi wa kuandaa kikundi cha sifa, kitakachotumika kwenye mkutano wa mwinjilisti Bonnke
Mratibu wa mikutano ya Bonnke barani Afrika, Mwinjilisti Pascal Ado kutoka
Togo, akiongea na waimbaji
Mwalimu John Shabani, akisimamia zoezi hilo
Waimbaji 5000
wanahitajika ili kukamilisha kikundi cha kusifu na kuabudu, kitakachoongoza
sifa katika mkutano wa Bonnke, unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 21 mwezi ujao.
Akiongea na mamia ya
waimbaji na wanamuziki, mratibu wa mikutano ya Bonnke barani Afrika, Mwinjilisti Pascal Ado kutoka
Togo, amesifia sana uimbaji wa Tanzania na kuwaasa waimbaji kufanya huduma hiyo
kwa moyo wote. Amesema mkutano huo utatazamwa katika nchi mbalimbali duniani, hivyo unadhifu
na uchangamfu unahitajika sana. Pamoja na hayo, amependekeza aina ya nyimbo zinazohitajika na kujiandaa
kuwa na sare ya aina ya mavazi ya ki-Afrika
JE WEWE NI MWIMBAJI BINAFSI, KWAYA AU KIKUNDI, UNAKARIBISHWA
KUUNGANA NA WAIMBAJI WENGINE KWA AJILI YA KUANDAA TIMU HIYO
Ni jumamosi hii, pale magomeni mikumi, katika kanisa la T.A.G.
Bado tuhitaji waimbaji.
No comments:
Post a Comment