Pages

19 August 2013

DARE ES SALAAM BONNKE CRUSADE 2013 - SHILINGI MILIONI 319 ZAOMBWA KUFANIKISHA MKUTANO WA BONNKE DAR ES SALAAM





BAJETI iliyowasilishwa na Kamati ya Maandalizi ili kufanikisha mkutano wa Injili wa mhubiri wa kimataifa, Mwinjilisti  Reinhard Bonnke unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania Agosti 21 hadi 25, mwaka huu ni dola 199,314.38 sawa na Shilingi za kitanzania 318,903,000.

Kamati hiyo inaongozwa na Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG, Magnus Mhiche (mwenyekiti), Mchungaji Kiongozi wa huduma ya The Oasis Healing Ministry, Prosper Ntepa (makamu mwenyekiti), Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania-Pentecoste Council of Tanzania (PCT), Askofu David Mwasota (katibu), na Askofu Bathlomew Sheggah, ambaye ni mhamasishaji.

Hadi Jumatano Agosti 14, kamati hiyo ilikuwa imepokea dola 60,000 sawa na Shilingi za kitanzania karibu milioni 100. Kwa mujibu wa bajeti hiyo, waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali ambao watahudhuria mkutano (press conference) kabla ya Bonnke kuanza kuhubiri, watatia kibindoni shilingi laki moja kila mmoja. Bajeti kwa ajili ya tukio hilo tu imepangwa kuwa dola za Marekani 1,212.50 sawa na shilingi za kitanzania 1,940,000.00
Katika bajeti hiyo imeelezwa kuwa viongozi watano wa kamati hiyo kila mmoja atapata malipo ya shilingi za kitanzania 200,000 kwa ajili ya mawasiliano na shilingi 350, 000 kwa ajili ya mafuta ya gari kwa siku moja. Bajeti hiyo inaonesha kutenga shilingi za kitanzania 2,100,000 kwa ajili ya wamama watakaokesha kuombea mkutano huo. Bajeti kamili imewatengea Wamama Shilingi za kitanzania 11,180,000.
 Bajeti kamili imekaa kama ifuatavyo:
Hospitality  Tsh 765, 0000   USD 478.13
Protocol      Tsh 9,665,000   USD 6,040.63
Counselling & Follow-up  Tsh 10,779,000 USD 6,736.88
Transport  Tsh 32,300,000   USD 20,187.50
Security Tsh 9,902,000   USD 6,188.75
Intercessory  Tsh 7,800,000  USD 4,875.00
Ushers  Tsh 4,600,000   USD 2,875.00
Music and Praise Tsh 8,400,000  USD 5,250.00
Administration & Central Committee    Tsh 50,940,000.00 USD 31,837.50
Women  Tsh 11, 180, 000  USD 6,987.50
Publicity  Tsh 83,100,000    USD  51,937.50
Interpretation  Tsh 3,000,000 USD 1,875.00
Technical  Tsh 4,000,000     USD 2,500.00
Fire Conference Tsh 6,000,00 USD 3,750.00
Youth  Tsh 5,000,000    USD  3,125.00
Bajeti hiyo haigusi gharama za malazi ya Bonnke na watumishi atakaoambatana nao akiwemo Mchungaji Daniel Kolenda. Zinahusisha malipo katika ukumbi wa watu maalum katika uwanja wa ndege (VIP Lounge) kwa siku mbili watu 11 ambapo zimeombwa shilingi za kitanzania 2,200,000.
Aidha, bajeti hiyo inahusisha pia usafiri wa Bonnke na watu atakaoongozana kutoka na kwenda uwanja wa ndege ambapo zimeombwa shilingi za kitanzania 1,000,000. 
Bajeti kamili ya kamati hiyo ni kama ifuatavyo:

 “Bahasha” kwa waandishi wa habari wanapohudhuria mikutano kama hiyo ambayo mara nyingi huchukua muda mfupi tu, ni kosa la kimaadili kwao na hata kwa wanatoa, lakini kiwango hicho cha “bahasha” kinaelezwa kuwa kikubwahivi KaLakini, inadaiwa kiasi hicho cha fedha ni kikubwa

No comments:

Post a Comment