Pages

2 October 2013

Hii kali: Ni Sherehe ya kuoga Uchi katika Mto Ganges ili kujitakasa na Dhambi




 Waumini wa dini ya Kihindu wakienda kuoga ili kujitakasa na dhambi walizotenda


Kutokana na wingi wa watu, treni kama unavyoona zinakuwa zimepakia hadi dereva hapati pa kuangalizia. Kila penye upenyo panakaa mtu isipokuwa tu kwenye magurudumu


Baada ya kuoga wateule hubeba maji kwenye vyungu vya vhuma kupeleka mahekaluni

Tofauti na imani ya Kikristo, ALLAHABAD, India, Mamilioni ya wai wa dini ya Hindu kila mwaka hufanya  hija yao ya kuoga katika makutano ya mito mitatu ya Ganges, Yamuna na Saraswati inapokutana. Kwa mujibu wa Imani ya Kihindu, binadamu anakuwa ametenda dhambi nyingi katika mzunguko wa mwaka na hivyo anahitaji kutakaswa na dhambi zake. Waumini wanaume wanajipaka majivu kuanzia utosini hadi unyayo na mara nyingi wanakuwa uchi wa mnyama ingawa sikuhizi wengine wanapendelea kuvaa pajama, wanaingia kwenye mto huo na kuoga nakuamini kuwa wameondolewa dhambi zao zote na nuksi nyingine zote. Hii ni sherehe kubwa na inayodumu muda mrefu kuliko zote duniani kwani inadumu kwa kipindi cha siku 55.

Mratibu mkuu wa sherehe hizo Mani Prasad Mishra alisema, mwaka huu karibu watu milioni zaidi ya  milioni 110 walikadiriwa kuoga kwenye eneo hilo liitwalo SANGAM. Hili ni eneo ambapo makutano ya mito ya GANGES, YAMUNA NASARASWATI . Sikukuu hii inatelemea mwonekano wa nyota zinazolandana angani. Baada ya nyota hizo kukaa katika mkao fulani basi wahindu wanaenda kuoga ili kujitakasa na madhambi yao na kuopuka kufo na kuzaliwa upya katika hali ya adhabu.






No comments:

Post a Comment