Pages

24 March 2014

KADI ZA ZA CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI ZIMEBORESHWA ZAIDI, SASA ZINAPATIKANA

                                                                   Ewe mwimbaji binafsi, mwana kwaya, mwana band, mwana muziki na mdau wa nyimbo za muziki, jiunge sasa na chama chako cha muziki wa Injili Tanzania, jipatie kadi yako ya uanachama.

15 March 2014

LIGHTNES BAYO, MAMA ALIYEJITOLEA KUWAKOMBOA MABINTI WANAOZALISHWA KATIKA UMRI MDOGO NA KUTELEKEZWA


Kwa wakaaji wa karatu na vitongoji vyake, jina la Lightness Bayo si ngeni masikioni mwao, kwani ni mwana mama alieamua kuyatumia maisha yake katika kuwasaidia mabinti waliozalishwa na kutelekezwa, mabinti hao ni wale hasa wenye umri mdogo. Pamoja na mabinti pia mama huyo amekuwa akiwasaidia watu wenye uhitaji mbalimbali wakiwemo wajane na yatima. Ili kuweza kuwasaidia watu hao Bi Lightness akisaidiana na wafadhili mbalimbali, amejenga kituo cha ufundi “Lake Eyasi Girls Vocation Training Center”,katika kijiji cha Mang,ola wilaya ya karatu.
Kituo hicho kimeweza kuinua kipata cha mabinti waliokuwa hawajiwezi na wengine kutaka kujiua. Moja ya mambo yanayofanyika katika kituo hocho ni kujifunza ushonaji na ufumaji. Pia mama huyo ameweza kuwasaidia jamii ya wamang’ati kwa kuwaanzishia mrati wa kufuga mbuzi na nyuki wa asali. Pamoja na kituo hicho, pia anacho kituo cha kulea watoto yatima.

Hata hivyo shule anayoiongoza yeye na mume wake katika mji wa karatu Tumaini Junior School, ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri nchini.
Inawezekana wewe ni Binti, umezalishwa na kutelekezwa, au unaye binti wa aina hiyo, au ungependa kuwa rafiki wa maono haya ya Bi Lightness, kwa kumuombea, kumtia moyo au kuchangia chochote, basi usisite kuwasiliana naye kwa simu namba 0754317394

 John Shabani katika kijiji cha Mang'ola huko karatu

 John akiimba na kikundi cha wamang'ati

Bi Lightness akimuonyesha John shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo cha Lake Eyesi Vocation Training Center

11 March 2014

JOHN SHABANI’S TOUR-TO VISIT HADZABE TRIBE (BUSHMAN)






Small groups of Hadzabe bushmen live around Lake Eyasi. Their language resembles the click languages of other bushmen further south in the Kalahari. Their small population was seriously threatened, in particular during the period when Julius Nyere tried to introduce his Ujuma policy. The tribe resisted the forcible settlement policies of Julius Nyere and nowadays most of their children have never seen a doctor or school - the bush provides for all their needs and is a class room for their offspring.
They are often willing for visitors to come and see their simple bush homes where the tree canopy alone or a cave provides them with shelter. They live entirely off the bush and from hunting, generally small antelopes and baboons, although in rainy seasons gazelles and antelopes come down from the Ngorongoro or Serengeti to their then lush bush lands offering them richer pickings. In the recent past their hunting activities were resented by trophy hunters who tried to stop their "illegal" hunting.





The string on their lethal bows is made from giraffe tendons and the arrows are coated with a strong poison made from another tree. The commiphora tree povides excellent firewood which they kindle by rubbing wood, a green commiphora provides a mosquito-repelling sap, juice squeezed out of the sansaveria provides a cure for snake bites while aloe is used to heal cuts. Roots provide a wide range of medicines and the mighty baobab fruits as a source of drink. A few hours spent with the bushmen makes the apparently unhospitable bush country come to life and to watch them hunt a unique experience as they stealthily spot then creep up on their prey skillfully killing it.

They Need your help!

3 March 2014

ALINE VYUKA, MWANA DADA MWENYE NDOTO ZA KUFIKA MBALI, AENDELEA KUFANYA VIZURI HUKO USA

 Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Burundi na muigizaji wa filamu anayeishi huko Marekani, DUKUDE VYUKUSENGE aka ALINE VYUKA aendelea kujizolea sifa kwa kuvitumia vipaji alivyopewa na mwenyezi Mungu.

Akiongea na mwalimu John Shabani (Katibu mkuu wa chama cha muziki wa injili Tanzania), Aline amesema kuwa, anajua kule Mungu aliko mtoa, hivyo ana maono ya kwenda mbali zaidi ki huduma, kielimu na kijamii.



Aline Vyuka ambae alianza kuimba kwenye kwaya akiwa na umri wa miaka 7,  miwili iliyopita aliweka hewani album yake 'Vyukusenge Vol 1' na baada ya hapo  aliweka akaja na album yake ya pili 'Dukunde Vol2' Nyimbo ambazo zimempa chati sana. Lakini hata hivyo Aline hajaridhika na kiwango chake cha uimbaji, anatamani kufanya vizuri zaidi, hivyo basi katika kuboresha huduma yake ya uimbaji, mwanadada huyo amekuwa akifanya kila awezalo ili kuwa mwimbaji bora. Moja ya waalimu wa nyimbo za injili walioamua kusimama na Aline ni mwalimu John Shabani . Mungu akipenda mwaka huu mwana dada huyo anatarajia kutembelea nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Tanzania na kurekodi nyimbo zake mpya.
Pia Mwana dada huyo anajiusisha na mpango mzima wakuigiza filamu. Mwaka 2010 filamu yake 'Family issues' iliwekwa hewani na ikamletea sifa kemu kemu kwa upande wawapenzi wa filamu. Mwaka wa 2013 ali iweka wakfu filamu yake ya pili 'ORPHANS'. Ukizingatia kuwa dada huyo ana mpango kabambe wa kuwasaidia watoto yatima na mabinti waliozalishwa majumbani.Pamoja na ugumu kidogo wa kipato lakini kwa maombi yako na ushauri wako na hata pia mchango wako, vitamsaidia kufika mbali. Aline analo  kundi linalo igiza filamu zake na yeye ndio kiongozi wahilo kundi,linajulikana kama 'BAHOWOOD' akitambulika ka Director na Muandishi (Story writer) kwenye filamu zote ambazo zilishatoka.
Mwsho Aline ametujulisha kuwa :" Ninaandaa filamu itakayojulikana kama INTERPRET "
Endelea kumwombea!


 Akirekodi mkanda wa video

 Akiwa na rafiki yake baada ya ibada huko mareakani


Ndani ya studio