Kwa wakaaji wa karatu na
vitongoji vyake, jina la Lightness Bayo si ngeni masikioni mwao, kwani ni mwana
mama alieamua kuyatumia maisha yake katika kuwasaidia mabinti waliozalishwa na
kutelekezwa, mabinti hao ni wale hasa wenye umri mdogo. Pamoja na mabinti pia
mama huyo amekuwa akiwasaidia watu wenye uhitaji mbalimbali wakiwemo wajane na
yatima. Ili kuweza kuwasaidia watu hao Bi Lightness akisaidiana na wafadhili
mbalimbali, amejenga kituo cha ufundi “Lake Eyasi Girls Vocation
Training Center”,katika kijiji cha Mang,ola wilaya ya karatu.
Kituo hicho kimeweza kuinua
kipata cha mabinti waliokuwa hawajiwezi na wengine kutaka kujiua. Moja ya mambo
yanayofanyika katika kituo hocho ni kujifunza ushonaji na ufumaji. Pia mama
huyo ameweza kuwasaidia jamii ya wamang’ati kwa kuwaanzishia mrati wa kufuga
mbuzi na nyuki wa asali. Pamoja na kituo hicho, pia anacho kituo cha kulea
watoto yatima.
Hata hivyo shule anayoiongoza yeye na mume wake katika mji wa karatu Tumaini Junior School, ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri nchini.
Inawezekana wewe ni Binti,
umezalishwa na kutelekezwa, au unaye binti wa aina hiyo, au ungependa kuwa
rafiki wa maono haya ya Bi Lightness, kwa kumuombea, kumtia moyo au kuchangia
chochote, basi usisite kuwasiliana naye kwa simu namba 0754317394
John Shabani katika kijiji cha Mang'ola huko karatu
John akiimba na kikundi cha wamang'ati
No comments:
Post a Comment