Mwalimu wa sauti John Shabani kikazi zaidi, ni katika kuhakikisha watu wanfanyika kuwa waimbaji bora na si bora kuimba
Baada ya mafunzo darasani, wanafunzi hupelekwa studio ili kujipima nguvu
Mwalimu John akisimamia mazoezi ya pumzi
Haya ni masomo
machache sana niliyoyachagua kati ya mengi ili kukupa hamasa kujiunga na darasa
la uimbaji linaloendelea jirani na Landa mark Hotel Ubungo chini ya mwalimu
John Shabani na timu yake
Karibu
ujifunze
Mambo ya msingi yanayofunzishwa katika program hii:
·
Tofauti ya mwimbaji na mwanamuziki
·
Vyakula na vinywaji vinavyofaa na visivyofaa kwa mwimbaji
·
Sifa na mbinu za kuwa mwimbaji bora
·
Jinsi ya kuitunza na kuiponya sauti yako
·
Amri 10 za sauti/uimbaji
·
Matumizi ya kipaza sauti (Microphone technique)
·
Utunzi wa nyimbo
·
Sifa 4 za kuwa na Album bora
·
Nguzo 4 za muziki
·
Key 7 za muziki
·
Mazoezi ya viungo yanayofaa kwa mwimbaji na faida zake
·
Ushauri kwa wanaotaka kurekodi nyimbo
Kuimba ni kutamka maneno katika
hali ya ki-muziki au pia twaweza kusema ni kutamka maneno moja baada ya jingine
kwa sauti yenye lahani (sauti ya ala ya muziki, tuni) au ghani (Singing is the
act of producing musical
sounds with the voice)
Mwimbaji ni mtu yeyote
mwenye uwezo wa kuimba au bila vyombo vya muziki (be sung a cappella) au kwa kutumia vyombo.
Mwimbaji huyo kwa lugha ya ki-muziki anaitwa vocalist. Ikumbukwe kuwa pia
katika vikundi vya uimbaji wapo wale wanaoongoza wengine katika uimbaji (A lead singer) na wengine kazi yao ni
kuitikia (backing singers)
N.B
Mwanadamu yeyote
mwenye uwezo wa kuongea, anauwezo wa kuimba pia.
Kama vile tulivyo na ala za aina mbalimbali, mwimbaji naye pia anazo ala
mbili muhimu:
Mdomo wenye uwezo wa kutoa sauti ya uimbaji
Mwili
Kumbuka moja ya
vitu vya msingi katika uimbaji ni nguvu (energy)
Mckinney alisema: “As
you sing higher, you must need more energy, as you sing lower, you must
useless; as you sing higher, you must
use more space; asa you sing lower, youmust need use less””. Zipo nguvu za
kiroho na za kimwili. Ili kuwa na nguvu za kimwili unahitaji maji ya kutosha,
chakula kizuri, hewa pamoja na mazoezi
ya viungo au ya pumzi.Mwimbaji pia anahitaji Pumzi ya kutosha (Breathing
support), chakula kizuri na maji ya kutosha
Funguo (Keys) 7 za muziki
C-do, D-re, E-mi,
F-fa, G-sol, A-la, B-si
Tunaipata key kwa
njia mbili: wewe mwenyewe kujitafutia au kusaidiwa na chombo cha muziki. Wewe
mwenyewe ukijipa key, waweza kubadili, lakini ukipewa key na chombo huwezi
kwenda kinyume.
Hakuna wimbo unaweza
kuimbwa katika key zote saba, bali key moja ye mabadiliko ya key kadhaa.
Ninaposhuka key ninaita hiyo ni flat na nikipanda chumba hiyo ni sharp, lakini
key E na B hazina sharp. Tofauti ya key moja kwenda key nyingine ni vyumba
viwili unapokuwa unatumia vyomvo vya muziki.
Kuimba kwenye tempo ni kuimba kwa kufuata
mapigo ya drum au aina yoyote ya ngoma au mshindo
Ikiwa
mwimbaji hajajua kuimbia kwenye funguo (key) na
mapigo au mdundo (beat) bado huyo anatatizo kubwa. Hakuna muziki wa
zamani na wa sasa, isipokuwa nyimbo ndio zinaweza kuwa za zamani.
MAADHI YA MUZIKI DUNIANI
Tunaposema maadhi tuna maanisha mtindo f ulani
wa muziki au uimbaji.
Kuna maadhi ya aina nyingi duniani, yapo maadhi ya nchi, maadhi ya
kabila maadhi ya dini, maadhi ya koo n.k
Chini ni maadhi kadhaa:
Rumba, Reggae, chakacha, kwela, kwaito, Sukous, sebene, rock, kuna pop
n.k
Sauti ni mlio wa chochote kinachoweza kusikika
SIFA ZAKUWA MWIMBAJI BORA
Sauti, kwenda na mapigo na kusimama kwenye ufunguo (Key),
mwonekano, (appearance), Uwezo wa
kuitumia sauti na kuitawala (Manage your vocal), Stage presence (Muonekano
jukwaani), kujiamini, kujitambua, kujithamini Self Cofidance) n.k.
HATUA 4 ZA KUREKODI AU KUWA NA ALBAM BORA
1.
Mwimbaji
kuwa bora
2.
Tungo
au ujumbe bora
3.
Muziki
bora
4.
Studio
bora
NGUZO
4 ZA MUZIKI
1.
Kusikiliza
muziki/uimbaji
2.
Kuhifadhi
muziki/uimbaji
3.
Kufanyia
kazi muziki/uimbaji
4.
Kuzalisha
muziki/uimbaji
Mazoezi kwa mwimbaji
Pamoja na faida
nyingi za mazoezi lakini pia mazoezi huchangamsha mwili, hulainisha koo,
husaidia kuwa na pumzi ya kutosha, hukuhepusha au kupunguza baadhi ya magonjwa
kama kisukari, presha n.k, hung’arisha ngozi, na kusaidia mfumo wa mzunguko wa
damu, MAZOEZI HUSAIDIA KATIKA MFUMO WA USAGAJI CHAKULA KUWA MZURI , KUKUPA
NGUVU NA KUWEZA KUFANYA KAZI KWA NGUVU ZAKO BILA KUJISKIA UMECHOKA NA MWISHO WA
SIKU HUPUNGUZA MAFUTA MWILINI, HUPUNGUZA
UZITO, KUNYOOSHA NA KUIMARISHA MISULI YA MWILI, HUSAIDIA MAPIGO MAZURI YA MOYO
KWA KUONGEZA KASI YA MAPIGO YAKE WAKATI WA MAZOEZI, UNGUZA MRUNDIKO WA DAMU
KWENYE MISHIPA, HII NI MUHIMU KWA SABABU MGANDO WA DAMU HUSABABISHA MAGONJWA YA
MOYO PAMOJA NA KUPOTEZA FAHAMU, MAZOEZI HUIMARISHA MIFUPA YA MWILI, HUBORESHA
USINGIZI.
Ni vidokezo tu, karibu darasani
utajifunza mengi!
0713 778 778
No comments:
Post a Comment