Pages

28 May 2014

ASKOFU MABOYA AZIDI KUWASHA MOTO WA INJILI MAREKANI

Ni semina ya pekee ndani ya Pennsylvania - USA


Kati ya watumishi wakitanzania ambao wamekuwa wakigusa mioyo ya wamarekani ni pamoja na  mkuu wa makanisa ya Calvary Assemblies of God, Askofu maboya. Tarehe 20 – 22/6/2014 ni semina kubwa ndani ya kanisa la Norristown New life church huko Pennsylvania. Katika semina hiyo yenye ujumbe wa “Nguvu ya Roho mtakatifu, chakula kitatolewa bure kwa kila atakayehudhuria

Watu wote wa maeneo ya jirani mnakaribisha

27 May 2014

RAIS BORA DUNIANI ASIYEAMINI KUHUSU UWEPO WA MUNGU



Huyu ndiye rais maskini duniani asiyeamini kuhusu Mungu wala uwepo wake

 Nyumba yake binafsi anamoishi

 Akitembea mtaani na mmbwa wake mmoja tena mwenye miguu mitatu

 Akiwa katika shughuli zake za kilimo

Hana mpango wa kwenda salon kunyoa, shughuli hiyo hufanyika nyumbani
Leo nimeamua kumleta kwenu Raisi masikini kuliko wote duniani anaitwa José Mujica
Kwamajina Kamili naitwa José Alberto "Pepe" Mujica Cordano
ni raisi wa Uruguay Tokea mwaka 2010..Alizaliwa 20 May 1935, ambaye ndiye rais bora kwa sasa akifuatiwa na rais wa Tanzania, Dk. J.K Kikwete, akifutiwa na Barack Obama wa Marekani
Raisi huyu kwa mwezi anapokea mshahara wa dola $12,000 kwa mwezi  lakini cha ajabu kabisa raisi huyu hutoa asilimia 90% ya mshahara wake kama sehemu ya msaada kwa wananchi wake wasiojiweza na hivyo kupokea mshara wa dola $775  hivyokumpelekeakuwa moja ya maraisi masikini zaidi ulimwenguni..
 Baada ya kuapishwa kuwa Raisi wa Uruguay alikata kuishi ikulu na kwenda kuishi nje ya kidogoya mji mahalipalipo shamba la mke wake.. Kitu cha thamani anachomiliki Raisi huyu ni gari aina ya Volkswagen Beetle, yenye Thamani ya dola $1,945..
Raisi Mujica alishapigwa risasi zaidi ya mara sita na kufungwa jela kwa zaidi ya miaka 14.
Mambo kadhaa kuhusu Rais Mujica:
1. Yani nguo zake zinafuliwa kawaida na kuanikwa nje tu, pia maji anayotumia ni ya kisima ambacho kina magugu mengi.
2. Analindwa na Polisi wawili na mbwa na alikataa kukaa kwenye nyumba ya serikali aliyopewa na badala yake kaenda kuishi kwenye nyumba ya mke wake huko mashambani ambako kuna mazingira ya kimasikini sana ikiwemo barabara mbovu nje kidogo ya mji wa Montevideo.
3. Rais na mkewe hufanya kazi ya kuotesha maua wao wenyewe yakiwa ni maisha ya kipekee kusikia ni ya Rais wa nchi.
4. Mujica anatoa asilimia tisini 90% ya mshahara wake wa kila mwezi kusaidia watu masikini huku akisema ‘naweza kuonekana kama mzee wa jadi lakini maisha haya nimeyachagua mwenyewe, naweza kuishi vizuri na kile nilichonacho.
5. Rais huyu kwa mwezi matumizi yake hayazidi shilingi milioni moja laki nne za Kitanzania ambapo kwenye kuorodhesha kiwango cha kipato cha kila kiongozi kwa mwaka na mali binafsi ikiwa ni lazima nchini humo kwa viongozi mbalimbali wa serikali mwaka 2010, alikutwa na kiasi cha dollar $ 1,800 tu kiasi ambacho hakizidi shilingi milioni tatu za kitanzania.
6. Gari anayotumia ni aina ya Volkswagen Beetle ambayo ni ya mwaka 1987
7. Mujica aliwahi kupigwa risasi mara sita na alitumikia kifungo miaka 14 jela ambapo muda wake mwingi kizuizini alikua katika mazingira magumu na kutengwa, mpaka alipoachiliwa huru mwaka 1985 wakati Uruguay ilivyorudi kwenye demokrasia.
8. Akiwa jela Mujica anasema hali ile ilimbadilishia mtazamo wake juu ya maisha na anakwambia ‘mimi naitwa rais maskini lakini mimi wala sihisi umaskini wowote, watu masikini ni wale ambao kazi yao ni kuishi maisha ya gharama ambayo inawasababisha kufanya kazi sana ili waendelee na maisha ya gahrama na kupata zaidi’

9. Ni Rais pekee asyeamini kuhusu Mungu au uwepo wa Mungu.

Haya ni baadhi ya maneno Ambayo aliyasema akiwa anahojiwa na kituo cha habari cha BBC
 "I'm called 'the poorest president', but I don't feel poor. Poor people are those who only work to try to keep an expensive lifes
tyle, and always want more and more," he says.
"This is a matter of freedom. If you don't have many possessions then you don't need to work all your life like a slave to sustain them, and therefore you have more time for yourself," he says.
"I may appear to be an eccentric old man... But this is a free choice."
The Uruguayan leader made a similar point when he addressed the Rio+20 summit in June this year: "We've been talking all afternoon about sustainable development. To get the masses out of poverty.
"But what are we thinking? Do we want the model of development and consumption of the rich countries? I ask you now: what would happen to this planet if Indians would have the same proportion of cars per household than Germans? How much oxygen would we have left?
"Does this planet have enough resources so seven or eight billion can have the same level of consumption and waste that today is seen in rich societies? It is this level of hyper-consumption that is harming our planet."

PAPA ASHUTUMU MAPADRI WALAWITI KANISANI




alipokua ziarani huko mashariki ya kati
 
Mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, amewasili Roma baada ya kukamilisha ziara yake ya siku tatu Mashariki ya Kati ambapo alisema kuwa tabia ya baadhi ya mapadri Wakatoliki waliokuwa wakiwanyanyasa watoto wadogo kingono kanisani inaweza kulinganishwa tu na misa ya Mashetani.
Baba Mtakatifu alifanya ziara ambayo ilihudhuriwa na maelfu ya watu wa imani tofauti katika eneo hilo na wachambuzi wengi wamesema kuwa imekuwa ya kufana.
Wengi wanasema kuwa Baba Mtakatifu kulinganisha vitendo vibaya vya ngono walivyofanyiwa watoto na mapadri na misa ya mashetani ni lugha nzito hasa ikitambuliwa kuwa tayari Papa Francis amewahi kuomba msamaha kwa vitendo hivyo kote duniani.
Vitendo hivyo vimeharibia sifa Kanisa Katoliki kwa muda mrefu sasa. Taarifa kutoka makao makuu ya Papa yanasema kuwa kwa mara ya kwanza tangu yeye achukue wadhifa wake anatarajiwa kukutana na wale walionyanyaswa na mapadri kingono. Wakatoliki wengi walikasirishwa na vitendo hivyo na wamefurahi kuwa Papa anaweza kuomba msamaha na kisha akutane na walioathirika na wengi wanasubiri kusikia atakachowambia atakapokutana nao.
Chanzo BBC SWAHILI

MUNGU NI MWEMA, OPERESHENI YA DEBORA JOHN IMEENDA VIZURI


Dada Debora baada ya oparesheni





Hapa mama mchungaji, Debora John akimsifu Mungu, 
huku akienda sambamba na  Mch. John Bagenyeka




Akimshuku Mungu Mchungaji John Bagenyeka amesema, anashukuru kwa maombi kwani Operesheni imeenda vizuri na Deborah anaendelea vizuri

26 May 2014

DEBORA JOHN HALI YAKE SIO NZURI. SEMA NENO JUU YAKE

Kila unapopiga goti, usisahau kumwambea dada yetu Debora John Said, hali yake bado si swari



Tunahitajika kumuombea ndugu yetu na rafiki yetu Debora John Saidi kwa wakati huu mgumu anaopitia. Hiki ni kipindi kigumu sana kwake kwania anateseka sana na maumivu makali. Mwimbaji huyo wa Injili na mama Mchungaji John Saidi, ambaye hali yake inaelezwa kwamba si nzuri na sasa yuko chumba cha upasuaji hospitali ya Mwananyamala kuondolewa uvimbe mkubwa tumboni ambao umesababisha asumbuliwe na maumivu makali yanayosababisha atokwe na machozi mara kwa mara.

Wito wetu kwa watumishi wa Mungu, tamka neon moja mbele za Mungu kwa ajili ya uponyaji wake; pia panga kumjulia hali.

Mbunge Vicky Kamata augua

  •  Augua ghafla, alazwa hospital, daktari kasema hatoweza kuhimili mikikimikiki ya harusi
  • Ndoa yake gizani
  • Paroko kanisa katoliki asema hakukidhi vigezo ya kufunga ndoa




 Dodoma/Dar es Salaam. Ni matukio nadra kutokea katika maisha, lakini haya ndiyo yaliyomkuta Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Vicky Kamata, baada ya kuugua ghafla saa 36 kabla ya harusi yake.
Kuugua kwa bibi harusi huyo mtarajiwa, kumezua gumzo katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma na maeneo mengine nchini, kutokana na kile kilichoelezwa kwamba harusi hiyo ilipangwa kuwa ya kifahari ikitarajiwa kutumia Sh96 milioni.
Kamata ilikuwa afunge ndoa leo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza Dar es Salaam na tayari kadi za mialiko zilishasambazwa kwa watu mbalimbali wakiwamo wabunge.
Habari za kuugua ghafla kwa mbunge huyo ambaye pia ni msanii wa muziki aliyetamba na kibao chake cha ‘Wanawake na Maendeleo’ zilianza kuzagaa kwa kasi juzi jioni nchini.
 Kamata ambaye pia ni mtetezi wa haki za wanawake,  aliugua usiku wa kuamkia jana na kupelekwa katika Hospitali ya Tabata General, iliyopo Segerea ambapo amelazwa.
“Niliugua tumbo ghafla, nilipata maumivu makali sana nikampigia daktari wangu na nilipomweleza jinsi ninavyojisikia, aliniambia niende hospitali haraka na kutokana na hali ilivyo, waliamua nilazwe,” alisema Kamata akiwa kitandani katika hospitali hiyo.
Kamata alifafanua kuwa, pamoja na mambo mengine, hali yake ya ujauzito imekuwa ikimsumbua na kuchangia yeye kulazwa kwa mara ya pili sasa katika kipindi cha wiki mbili. Mbunge huyo ambaye alitakiwa kufunga ndoa leo, alisema kuwa kutokana na maradhi hayo, haelewi hatima ya ndoa yake, ingawa wanafamilia na wanakamati wanaendelea na mipango ya harusi kama ilivyopangwa.
“Mama anaenda nyumbani sasa hivi kuniandalia nguo na kila kitu, lakini sijui itakuwaje kwa sababu daktari amesema kutokana na hali yangu ilivyo, itakuwa vigumu kuvaa viatu virefu na kupata usumbufu wote wa purukushani za harusi,” alisema.
Aliongeza kuwa mipango yote ya harusi ipo tayari kinachosubiriwa na siku yenyewe, lakini kwa bahati mbaya jambo hilo limetokea na haliwezi kuepukika.
Vicky alisema wanakamati wa Dar es Salaam na wale wa Dodoma, wanaendelea na vikao ingawa, wamechanganyikiwa  kutokana na sintofahamu iliyopo, kama harusi itafanyika au haitafanyika.
 Ndugu wa mbunge huyo akiwemo mama yake mzazi Kamata walionekana hospitalini hapo  wakiendelea kumfariji na kujadili kuhusu hatima ya harusi hiyo, iliyokuwa ikingojewa kwa hamu na wanafamilia wote.
Daktari wa Kamata, aliyefahamika kwa jina la Diwani Msemo, alieleza kuwa mbunge huyo alifika hospitalini hapo akiwa na maumivu makali ya tumbo yaliyofanana na uchungu wa kuzaa, hali iliyoonyesha kuwa ujauzito wake unatishia kutoka.
“Ukipata yale maumivu kama mimba ni changa inakuwa kama tishio la mimba kutoka, siyo hivyo tu, bali alikuwa anatapika na presha ikashuka. Kwa kweli mimba yake  ipo katika hatari,” alisema
Alisema pamoja na kumpa matibabu, walishauriana kuwa apumzike kwa siku tano ili kuhakikisha kiumbe kilichopo tumboni kipo salama.
“Ilikuwa ni uamuzi mgumu kwa sababu ni siku yake ya harusi, lakini tunaangalia umuhimu wa kiumbe na kama ataenda, itabidi asaini ili ijulikane kuwa hatukumkubalia. Kwa kifupi hayuko fiti kwa shughuli hiyo,” alisema.
Harusi ya Kamata iliandikwa pia na mitandao mbalimbali ya kijamii nchini na jana redio moja ilitangaza kuugua kwake, ikisema kumetokana na matatizo ya ujauzito.
Kumekuwa na uvumi unaosambazwa kwa kasi juu ya sababu za kuahirishwa kwa harusi hiyo, lakini kwa sababu ya maadili ya uandishi hatutaweza kuziandika katika gazeti hili.
Paroko aliyekuwa afungishe ndoa anena
 Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi , Sinza Dar es Salaam, Cuthbert Maganga alipohojiwa kuhusu taarifa za kufungwa kwa ndoa hiyo, alikiri kwamba iliandikishwa ili ifungwe kanisani hapo.
Hata hivyo akasema ilishindikana, baada ya wahusika kukwama kuwasilisha baadhi ya nyaraka muhimu zilizohitajika, ili kukamilisha sakramenti hiyo. 
“Ilitarajiwa kufungwa Mei 24 mwaka huu yaani  kesho (leo), lakini kwa taratibu za kanisa letu ilishindikana kwa sababu bibi harusi alishindwa kuwasilisha cheti chake cha ubatizo, pia hakuwa amepata kipaimara, vitu hivyo ni miongoni mwa vitu muhimu vinavyohitajika ili kukamilisha Sakramenti ya Ndoa,” alisema Padri Maganga.
Alisema Kamata ndiye aliyekwenda kuandikisha ndoa hiyo, kwa kuwa ni muumini wa kanisa hilo anayetokea Kanda D.
Juhudi za kumtafuta bwana harusi, Charles Gardner hazikuweza kufanikiwa baada ya simu yake kuita bila kupokelewa, hata alipotumiwa ujumbe wa maandishi hakuwa tayari kujibu.
Hata hivyo, baadhi ya rafiki wa karibu wa Gardner walieleza kuwa wamejulishwa kuwa ndoa hiyo haipo na kwamba jana bwana harusi huyo mtarajiwa alionekana akiwa katika hali isiyo ya kawaida.
“Nilijaribu kumuuliza kuhusu harusi yake, lakini hakuwa tayari kunieleza bayana, ila hayupo katika hali yake ya kawaida,” alisema mmoja wa rafiki zake. 
Imeandikwa na Florence Majani, Daniel Mjema na Beatrice Moses