28 May 2014
ASKOFU MABOYA AZIDI KUWASHA MOTO WA INJILI MAREKANI
23:50
No comments
Ni semina ya pekee ndani ya Pennsylvania - USA
Kati
ya watumishi wakitanzania ambao wamekuwa wakigusa mioyo ya wamarekani ni pamoja
na mkuu wa makanisa ya Calvary
Assemblies of God, Askofu maboya. Tarehe 20 – 22/6/2014 ni semina kubwa ndani
ya kanisa la Norristown New life church huko Pennsylvania. Katika semina hiyo
yenye ujumbe wa “Nguvu ya Roho mtakatifu, chakula kitatolewa bure kwa kila
atakayehudhuria
Watu
wote wa maeneo ya jirani mnakaribisha
27 May 2014
RAIS BORA DUNIANI ASIYEAMINI KUHUSU UWEPO WA MUNGU
23:55
No comments
Huyu ndiye rais maskini duniani asiyeamini kuhusu Mungu wala uwepo wake
Nyumba yake binafsi anamoishi
Akitembea mtaani na mmbwa wake mmoja tena mwenye miguu mitatu
Akiwa katika shughuli zake za kilimo
Hana mpango wa kwenda salon kunyoa, shughuli hiyo hufanyika nyumbani
Leo nimeamua kumleta kwenu Raisi
masikini kuliko wote duniani anaitwa José Mujica
Kwamajina Kamili naitwa José Alberto "Pepe" Mujica Cordano ni raisi wa Uruguay Tokea mwaka 2010..Alizaliwa 20 May 1935, ambaye ndiye rais bora kwa sasa akifuatiwa na rais wa Tanzania, Dk. J.K Kikwete, akifutiwa na Barack Obama wa Marekani
Kwamajina Kamili naitwa José Alberto "Pepe" Mujica Cordano ni raisi wa Uruguay Tokea mwaka 2010..Alizaliwa 20 May 1935, ambaye ndiye rais bora kwa sasa akifuatiwa na rais wa Tanzania, Dk. J.K Kikwete, akifutiwa na Barack Obama wa Marekani
Raisi huyu kwa mwezi anapokea mshahara wa dola $12,000 kwa mwezi lakini
cha ajabu kabisa raisi huyu hutoa asilimia 90% ya mshahara wake kama sehemu ya
msaada kwa wananchi wake wasiojiweza na hivyo kupokea mshara wa dola $775
hivyokumpelekeakuwa moja ya maraisi masikini zaidi ulimwenguni..
Baada ya kuapishwa kuwa Raisi wa Uruguay alikata kuishi ikulu na kwenda kuishi nje ya kidogoya mji mahalipalipo shamba la mke wake.. Kitu cha thamani anachomiliki Raisi huyu ni gari aina ya Volkswagen Beetle, yenye Thamani ya dola $1,945..
Raisi Mujica alishapigwa risasi zaidi ya mara sita na kufungwa jela kwa zaidi ya miaka 14.
Baada ya kuapishwa kuwa Raisi wa Uruguay alikata kuishi ikulu na kwenda kuishi nje ya kidogoya mji mahalipalipo shamba la mke wake.. Kitu cha thamani anachomiliki Raisi huyu ni gari aina ya Volkswagen Beetle, yenye Thamani ya dola $1,945..
Raisi Mujica alishapigwa risasi zaidi ya mara sita na kufungwa jela kwa zaidi ya miaka 14.
Mambo kadhaa kuhusu Rais Mujica:
1. Yani nguo zake zinafuliwa kawaida na kuanikwa
nje tu, pia maji anayotumia ni ya kisima ambacho kina magugu mengi.
2. Analindwa na Polisi wawili na mbwa na alikataa
kukaa kwenye nyumba ya serikali aliyopewa na badala yake kaenda kuishi kwenye
nyumba ya mke wake huko mashambani ambako kuna mazingira ya kimasikini sana
ikiwemo barabara mbovu nje kidogo ya mji wa Montevideo.
3. Rais na mkewe hufanya kazi ya kuotesha maua wao
wenyewe yakiwa ni maisha ya kipekee kusikia ni ya Rais wa nchi.
4. Mujica
anatoa asilimia tisini 90% ya mshahara wake wa kila mwezi kusaidia watu
masikini huku akisema ‘naweza kuonekana kama mzee wa jadi lakini maisha haya
nimeyachagua mwenyewe, naweza kuishi vizuri na kile nilichonacho.
5. Rais huyu kwa mwezi matumizi yake hayazidi
shilingi milioni moja laki nne za Kitanzania ambapo kwenye kuorodhesha kiwango
cha kipato cha kila kiongozi kwa mwaka na mali binafsi ikiwa ni lazima nchini
humo kwa viongozi mbalimbali wa serikali mwaka 2010, alikutwa na kiasi cha
dollar $ 1,800 tu kiasi ambacho hakizidi shilingi milioni tatu za kitanzania.
6. Gari anayotumia ni aina ya Volkswagen Beetle
ambayo ni ya mwaka 1987
7. Mujica
aliwahi kupigwa risasi mara sita na alitumikia kifungo miaka 14 jela ambapo
muda wake mwingi kizuizini alikua katika mazingira magumu na kutengwa, mpaka
alipoachiliwa huru mwaka 1985 wakati Uruguay ilivyorudi kwenye demokrasia.
8. Akiwa jela Mujica anasema hali ile
ilimbadilishia mtazamo wake juu ya maisha na anakwambia ‘mimi naitwa rais maskini
lakini mimi wala sihisi umaskini wowote, watu masikini ni wale ambao kazi yao
ni kuishi maisha ya gharama ambayo inawasababisha kufanya kazi sana ili
waendelee na maisha ya gahrama na kupata zaidi’
9. Ni Rais pekee asyeamini kuhusu Mungu au uwepo wa
Mungu.
Haya ni
baadhi ya maneno Ambayo aliyasema akiwa anahojiwa na kituo cha habari cha BBC
"I'm
called 'the poorest president', but I don't feel poor. Poor people are those
who only work to try to keep an expensive lifes
tyle, and
always want more and more," he says.
"This is a matter of freedom. If you don't
have many possessions then you don't need to work all your life like a slave to
sustain them, and therefore you have more time for yourself," he says.
"I may appear to be an eccentric old man... But this is a free choice."
The Uruguayan leader made a similar point when he addressed the Rio+20 summit in June this year: "We've been talking all afternoon about sustainable development. To get the masses out of poverty.
"But what are we thinking? Do we want the model of development and consumption of the rich countries? I ask you now: what would happen to this planet if Indians would have the same proportion of cars per household than Germans? How much oxygen would we have left?
"Does this planet have enough resources so seven or eight billion can have the same level of consumption and waste that today is seen in rich societies? It is this level of hyper-consumption that is harming our planet."
"I may appear to be an eccentric old man... But this is a free choice."
The Uruguayan leader made a similar point when he addressed the Rio+20 summit in June this year: "We've been talking all afternoon about sustainable development. To get the masses out of poverty.
"But what are we thinking? Do we want the model of development and consumption of the rich countries? I ask you now: what would happen to this planet if Indians would have the same proportion of cars per household than Germans? How much oxygen would we have left?
"Does this planet have enough resources so seven or eight billion can have the same level of consumption and waste that today is seen in rich societies? It is this level of hyper-consumption that is harming our planet."
PAPA ASHUTUMU MAPADRI WALAWITI KANISANI
08:44
No comments
alipokua ziarani huko mashariki ya kati
Mkuu
wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, amewasili Roma baada ya kukamilisha
ziara yake ya siku tatu Mashariki ya Kati ambapo alisema kuwa tabia ya
baadhi ya mapadri Wakatoliki waliokuwa wakiwanyanyasa watoto wadogo
kingono kanisani inaweza kulinganishwa tu na misa ya Mashetani.
Baba
Mtakatifu alifanya ziara ambayo ilihudhuriwa na maelfu ya watu wa imani
tofauti katika eneo hilo na wachambuzi wengi wamesema kuwa imekuwa ya
kufana.
Wengi
wanasema kuwa Baba Mtakatifu kulinganisha vitendo vibaya vya ngono
walivyofanyiwa watoto na mapadri na misa ya mashetani ni lugha nzito
hasa ikitambuliwa kuwa tayari Papa Francis amewahi kuomba msamaha kwa
vitendo hivyo kote duniani.
Vitendo hivyo vimeharibia sifa Kanisa Katoliki kwa muda mrefu sasa.
Taarifa
kutoka makao makuu ya Papa yanasema kuwa kwa mara ya kwanza tangu yeye
achukue wadhifa wake anatarajiwa kukutana na wale walionyanyaswa na
mapadri kingono.
Wakatoliki
wengi walikasirishwa na vitendo hivyo na wamefurahi kuwa Papa anaweza
kuomba msamaha na kisha akutane na walioathirika na wengi wanasubiri
kusikia atakachowambia atakapokutana nao.
Chanzo BBC SWAHILI
MUNGU NI MWEMA, OPERESHENI YA DEBORA JOHN IMEENDA VIZURI
01:17
No comments
Dada Debora baada ya oparesheni
Hapa mama mchungaji, Debora John akimsifu Mungu,
huku akienda sambamba na Mch. John Bagenyeka
Akimshuku Mungu Mchungaji John
Bagenyeka amesema, anashukuru kwa maombi kwani Operesheni
imeenda vizuri na Deborah anaendelea vizuri
26 May 2014
DEBORA JOHN HALI YAKE SIO NZURI. SEMA NENO JUU YAKE
15:02
No comments
Kila unapopiga goti, usisahau kumwambea dada yetu Debora John Said, hali yake bado si swari
Tunahitajika kumuombea ndugu yetu na rafiki yetu Debora John Saidi kwa
wakati huu mgumu anaopitia. Hiki ni kipindi kigumu sana kwake kwania anateseka
sana na maumivu makali. Mwimbaji huyo wa Injili na mama Mchungaji John Saidi,
ambaye hali yake inaelezwa kwamba si nzuri na sasa yuko chumba cha upasuaji
hospitali ya Mwananyamala kuondolewa uvimbe mkubwa tumboni ambao umesababisha asumbuliwe
na maumivu makali yanayosababisha atokwe na machozi mara kwa mara.
Wito wetu kwa watumishi wa Mungu, tamka neon moja mbele za Mungu kwa ajili ya uponyaji wake; pia panga kumjulia hali.
Wito wetu kwa watumishi wa Mungu, tamka neon moja mbele za Mungu kwa ajili ya uponyaji wake; pia panga kumjulia hali.
Mbunge Vicky Kamata augua
00:17
No comments
- Augua ghafla, alazwa hospital, daktari kasema hatoweza kuhimili mikikimikiki ya harusi
- Ndoa yake gizani
- Paroko kanisa katoliki asema hakukidhi vigezo ya kufunga ndoa
Dodoma/Dar es Salaam. Ni matukio nadra kutokea katika maisha, lakini haya ndiyo yaliyomkuta Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Vicky Kamata, baada ya kuugua ghafla saa 36 kabla ya harusi yake.
Kuugua kwa bibi harusi huyo mtarajiwa, kumezua gumzo katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma na maeneo mengine nchini, kutokana na kile kilichoelezwa kwamba harusi hiyo ilipangwa kuwa ya kifahari ikitarajiwa kutumia Sh96 milioni.
Kamata ilikuwa afunge ndoa leo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza Dar es Salaam na tayari kadi za mialiko zilishasambazwa kwa watu mbalimbali wakiwamo wabunge.
Habari za kuugua ghafla kwa mbunge huyo ambaye pia ni msanii wa muziki aliyetamba na kibao chake cha ‘Wanawake na Maendeleo’ zilianza kuzagaa kwa kasi juzi jioni nchini.
Kamata ambaye pia ni mtetezi wa haki za wanawake, aliugua usiku wa kuamkia jana na kupelekwa katika Hospitali ya Tabata General, iliyopo Segerea ambapo amelazwa.
“Niliugua tumbo ghafla, nilipata maumivu makali sana nikampigia daktari wangu na nilipomweleza jinsi ninavyojisikia, aliniambia niende hospitali haraka na kutokana na hali ilivyo, waliamua nilazwe,” alisema Kamata akiwa kitandani katika hospitali hiyo.
Kamata alifafanua kuwa, pamoja na mambo mengine, hali yake ya ujauzito imekuwa ikimsumbua na kuchangia yeye kulazwa kwa mara ya pili sasa katika kipindi cha wiki mbili. Mbunge huyo ambaye alitakiwa kufunga ndoa leo, alisema kuwa kutokana na maradhi hayo, haelewi hatima ya ndoa yake, ingawa wanafamilia na wanakamati wanaendelea na mipango ya harusi kama ilivyopangwa.
“Mama anaenda nyumbani sasa hivi kuniandalia nguo na kila kitu, lakini sijui itakuwaje kwa sababu daktari amesema kutokana na hali yangu ilivyo, itakuwa vigumu kuvaa viatu virefu na kupata usumbufu wote wa purukushani za harusi,” alisema.
Aliongeza kuwa mipango yote ya harusi ipo tayari kinachosubiriwa na siku yenyewe, lakini kwa bahati mbaya jambo hilo limetokea na haliwezi kuepukika.
Vicky alisema wanakamati wa Dar es Salaam na wale wa Dodoma, wanaendelea na vikao ingawa, wamechanganyikiwa kutokana na sintofahamu iliyopo, kama harusi itafanyika au haitafanyika.
Ndugu wa mbunge huyo akiwemo mama yake mzazi Kamata walionekana hospitalini hapo wakiendelea kumfariji na kujadili kuhusu hatima ya harusi hiyo, iliyokuwa ikingojewa kwa hamu na wanafamilia wote.
Daktari wa Kamata, aliyefahamika kwa jina la Diwani Msemo, alieleza kuwa mbunge huyo alifika hospitalini hapo akiwa na maumivu makali ya tumbo yaliyofanana na uchungu wa kuzaa, hali iliyoonyesha kuwa ujauzito wake unatishia kutoka.
“Ukipata
yale maumivu kama mimba ni changa inakuwa kama tishio la mimba kutoka, siyo
hivyo tu, bali alikuwa anatapika na presha ikashuka. Kwa kweli mimba yake
ipo katika hatari,” alisema
Alisema
pamoja na kumpa matibabu, walishauriana kuwa apumzike kwa siku tano ili
kuhakikisha kiumbe kilichopo tumboni kipo salama.
“Ilikuwa
ni uamuzi mgumu kwa sababu ni siku yake ya harusi, lakini tunaangalia umuhimu
wa kiumbe na kama ataenda, itabidi asaini ili ijulikane kuwa hatukumkubalia.
Kwa kifupi hayuko fiti kwa shughuli hiyo,” alisema.
Harusi ya
Kamata iliandikwa pia na mitandao mbalimbali ya kijamii nchini na jana redio
moja ilitangaza kuugua kwake, ikisema kumetokana na matatizo ya ujauzito.
Kumekuwa
na uvumi unaosambazwa kwa kasi juu ya sababu za kuahirishwa kwa harusi hiyo,
lakini kwa sababu ya maadili ya uandishi hatutaweza kuziandika katika gazeti
hili.
Paroko
aliyekuwa afungishe ndoa anena
Padri
wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi , Sinza Dar es
Salaam, Cuthbert Maganga alipohojiwa kuhusu taarifa za kufungwa kwa ndoa hiyo,
alikiri kwamba iliandikishwa ili ifungwe kanisani hapo.
Hata
hivyo akasema ilishindikana, baada ya wahusika kukwama kuwasilisha baadhi ya
nyaraka muhimu zilizohitajika, ili kukamilisha sakramenti hiyo.
“Ilitarajiwa
kufungwa Mei 24 mwaka huu yaani kesho (leo), lakini kwa taratibu za
kanisa letu ilishindikana kwa sababu bibi harusi alishindwa kuwasilisha cheti
chake cha ubatizo, pia hakuwa amepata kipaimara, vitu hivyo ni miongoni mwa
vitu muhimu vinavyohitajika ili kukamilisha Sakramenti ya Ndoa,” alisema Padri
Maganga.
Alisema Kamata
ndiye aliyekwenda kuandikisha ndoa hiyo, kwa kuwa ni muumini wa kanisa hilo
anayetokea Kanda D.
Juhudi za
kumtafuta bwana harusi, Charles Gardner hazikuweza kufanikiwa baada ya simu
yake kuita bila kupokelewa, hata alipotumiwa ujumbe wa maandishi hakuwa tayari
kujibu.
Hata
hivyo, baadhi ya rafiki wa karibu wa Gardner walieleza kuwa wamejulishwa kuwa
ndoa hiyo haipo na kwamba jana bwana harusi huyo mtarajiwa alionekana akiwa
katika hali isiyo ya kawaida.
“Nilijaribu
kumuuliza kuhusu harusi yake, lakini hakuwa tayari kunieleza bayana, ila hayupo
katika hali yake ya kawaida,” alisema mmoja wa rafiki zake.
Imeandikwa
na Florence Majani, Daniel Mjema na Beatrice Moses
Subscribe to:
Posts (Atom)