UNAPOKUWA KWENYE WAKATI MGUMU
Haijalishi uko kwenye wakati mgumu kiasi gani, acha kutia huruma haitakusaidia.
Wakati huna pesa, wakati mambo hayaendi, wakati hujafanikisha kodi ya nyumba, huna ada, huna biashara, au biashara haina faida, huna kazi, unauguza, wakati umetendwa na ndugu, rafiki, boss, mchumba, mume, mke, wakati wa maumivu ya kufiwa, kuachwa, kusemwa vibaya...huo ndio wakati wa kujiweka sawa, pendeza, changamka, kilichopo kula,
angalia movie nzuri, sikiliza nyimbo nzuri, soma makala na vitabu vizuri kama kile changu cha "MARUFUKU KUKATA TAMAA" toka kidogo, nenda sehemu nzuri yenye mazingira mazuri, fanya ibada pia kuwa busy na mambo yako,
the more you think about bad situation, the more weak and pissed off i become. I just have to let things be and let it go. That makes me cool and lively all time.
Bado kuna nafasi nyingi yakufanikiwa, bado kuna nafasi ya kupenda na kupendwa, kuna yale yamesababishwa na mazingira au watu wengine, yale umesababisha mwenyewe, kuna yale yameletwa na ibilisi lakini yapo yale yaliyo ruhusiwa na Mungu mwenyewe. Unachotakiwa kujua kuna namna Mungu anahitaji uwe kabla ya kulifikia kusudi lake.