Ni kweli ni vizuri kuwa KIROHO; lakini kuwa kiroho isiwe sababu ya kuto-jichanganya na watu na kujenga mahusiano. Kuna baadhi WADADA WAPENDWA wanawaona WANAUME wote ni watenda dhambi. Yani mtu akitaka kuanza nae mahusiano ya kujuana/urafiki, yeye tayari anakuwa kwenye ALARM ya DANGER… yani anachokiona kwa kijana ni kwamba lazima atakuwa ana nia mbaya.
Ushauri wangu kwa WADADA ni kwamba ni muhimu tujenge mahusiano ya kirafiki na vijana makanisani mwetu. Urafiki ni hatua muhimu ya kufanya maamuzi yanayopelekea uchumba hadi ndoa. Tusivae SURA YA MAOMBI kila saa….!!
Kwa upande mwingine, VIONGOZI WA MAKANISA, tusiwawekee vijana wetu (KIKE/KIUME) vikwazo vingi ambavyo vinasababisha wasiweze kujenga mahusiano. Ni kweli lazima TUSISITIZIE UTAKATIFU lakini tusifanye WOKOVU UGEUKE GEREZA. Tusiporuhusu wajenge mahusiano, je, wataoanaje?? Tuwafundishe vijana wetu wawe na nidhamu ya kuweza kujisimamia na kujua MIPAKA ya urafiki na mahusiano kati yao. Vijana wetu wakibanwa sana wataanza mahusiano kwa siri ambayo mara nyingi huishia vibaya; pia wanaweza kutafuta marafiki nje ya kanisa ambayo pia matokeo yake siyo mazuri sana.
MITHALI 17:17 (BHN); "Rafiki wa kweli ni rafiki siku zote, ndugu huzaliwa asaidie wakati wa taabu."