THE OFFICIAL JOHN SHABANI AND GOSPEL IN AFRICA BLOG

Welcome to the official blog of the the gospel singer, songwriter and teacher John Shabani. If you are one of the fans among the millions, feel free to get connected with John Shabani and stay updated on this blog.To learn more about John Shaban and his Ministry, please click the about button above.

GET THE LATEST FROM JOHN SHABAN AND THE GOSPEL NEWS COMMUNITY

You will be able to read and review the latest news on John Shabani's tour and other specials. You will also come across the best articles of news on Gospel from all across Africa and the International Community.Please do feel free to review our categories of news and events.

FEEL FREE TO LEARN MORE ABOUT JOHN SHABANI AND HIS MINISTRY

If you wish to learn more about John Shabani and his ministry, please feel free to connect with John Shabani on the social networks. You can keep up with John Shabani and the Gospel in Africa community on both twitter, facebook, google plus and many other more.

STAY UPDATED WITH INTERNATIONAL AND LOCAL GOSPEL NEWS

Gospel in Africa Blog is a comprehensive gathering place for African Gospel music fans. Offering the latest news and information about Local and International Gospel music and news, Gospel in Africa Blog also shares the spotlight with other genres of Christian music that more than ever, seemingly overlap musical genre lines, such as Bluegrass Gospel, Christian Country and others. Singing News, the leading African Gospel and International music Blog, features African and international Gospel lyrics, radio, news, Christian concerts, songs, artists, and more.

GET IN TOUCH AND STAY CONNECTED WITH JOHN SHABANI

If you are interested in contacting and staying in touch with John Shabani then here are the contacts. E- mail: touchingvoice@yahoo.com or , princejohntz@yahoo.com, Mob: +255 754 818 767 or +255 716 560 094, www.facebook.com/john.shabani.

30 October 2014

MKAKATI WA KUWASAIDIA WATOTO YATIMA



 Bi Warra Nnko akiwa amekumbatia kitoto kichanga kilicholetwa baada ya mama yake kufariki wakati wa kujifungua

 Baadhi ya watoto wakipata kifungua kinywa



 Muonekano wa jengo la Shalom Orphanage Center

 John shabani akitoa mafunzo kwa watoto




 Mwenyekiti wa Chama Cha Wajane Tanzania, akiwa katika hali ya huzuni baada ya kujionea hali mbaya ya baadhi ya watoto walioletwa katika kituo cha Shalom

Hawa ni watoto wanaolelewa katika kituo cha SHALOM! watoto hawa, waliookotwa vichakani hali zao zikiwa mbaya sana, kila mara baba yao mzazi ambaye ni mlevi wa kupindukia, aliwalawiti kwa zamu. Maisha yao yalikua ya kuokota vyakula vilivyotupwa jalalani, huku makazi yao yakiwa ni kulala vichakani baada ya nyumba yao ya majani kuanguka.

 Watoto wakisherekea sikukuu ya Christsmass

 Wageni mbalimbali hujitolea kufanya kazi za kijamii katika kituo


 Moja ya madarasa

Baada ya kuzunguka maeneo mbalimba, hii ni ziara nyingine ya kutembelea kituo cha watoto yatima
                              “SHALOM ORPHANAGE CENTER”!    
                                           Mimi na wewe tunaweza.

Jambo moja nililojifunza chini ya jua, ni kufanya Jambo sahihi, kwa mazingira sahihi, kwa watu sahihi, na kwa wakati sahihi. Jambo lako, wazo lako, uamuzi wako, mkakati wako vyaweza kuwa, sahihi lakini si kwa watu sahihi, labda si kwa mazingira sahihi, lakini pia labda si kwa wakati sahihi.
Inawezekana umekuwa ukifanya mambo mengi, lakini pia unataka uonekane na watu, upongezwe au uambiwe asante! Si vibaya, lakini wakati mwingine fanya jambo katika mazingira ambayo si ya kupongezwa wala kusifiwa bali kwako ni wajibu kama mwanadamu ambaye uhai wako hujaugharimia chochote.

Moja ya mambo nilioamua ni kuwaona watu wenye uhitaji haswa tena huko maeneo ya vijijini, hilo ni jukumu letu sote. Ndio maana baada ya kuzungukia vituo mbalimba vya watoto yatima Tanzania, ziara iliyoratibiwa na Chama cha Wajane Tanzania (Tanzania Widows Association), moja ya kituo kilichonigusa sana ni cha SHALOM ORPHANAGE CENTER, kilichopo huko karatu, kilomita 160 kutoka jiji la Arusha. 

Moja ya vitu nilivyoguswa navyo ni kumuona mama mjane Bi Warra Nnko, akiwa amegeuza nyumba yake kuwa kituo cha kulelea watoto. Vipo vyumba vya watoto wachanga haswa, wengine wameokotwa wakiwa wametupwa baada ya kuzaliwa na wengine wazazi kufariki wakati wa kujifungua. Pia wapo watoto ambao huletwa wakiwa katika hali mbaya, wangine wamebakwa na kulawitiwa. Nilitiwa moyo kuona hata serikali ya wilaya na hata mkoa huleta watoto katika kituo hicho. 

Vipo vyumba vya watoto wenye hali mbaya, wengine wanaulemavu wa aina mbalimbali, wengine wameathiki na ukimwi n.k. Shalom Orphanage center ni kama Hospital, Shule, na mji wa makimbilio. Pia nimeguswa kuona Bibi huyo ameanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ya ng’ombe wa maziwa, kuku wa mayai na mashamba ili watoto wapate lishe na afya bora. Ukifika shalom lazima ulie kidogo; lakini cha kushangaza watoto hao,kuanzia wachanga na wale wanaosomeshwa sekondari wote humwita Bibi Warra Mama!

Mimi kama mwalimu wa sauti na uimbaji, nikiwanimeambatana na mwenyekiti wa Chama Cha Wajane Tanzania na baadhi ya watu, pamoja na kila mtu kutoa kile alichokuwanacho, lakini pia niliamua kuanzisha mpango wa kuibua vipaji vya watoto.

Wito wangu kwako, ni kukuomba tuungane kwa pamoja safari hii tena, kwa chochote ulichonacho tukawaone watoto hao mwishoni mwa mwezi huu wa Novemba. Pia ikumbukwe kuwa karatu nisehemu nzuri ya utalii wa ndani, utajifunza mengi pale MTO WA MMBU, lakini pia kutembelea mbuga za SERENGETI, NGORONGORO, pamoja na kutembelea kwenye misitu na mapango ya mawe wanakoishi waadzabe. 

Unaweza ukaleta nguo, chakula, pesa yako na chochote ulichonacho kisha ukakabidhi katika ofisi za Chama cha Wajane Tanzania zilizopo maeneo ya kinyerezi.
Kwa mawasiliano zaidi tupigie: 0754 366 530, 0713778778

14 October 2014

KUTUMIA NGUVU ILI KUIMBA VIZURI



Hapa ni mwalimu John Shabani sambamba na Masanja mkandamizaji pamoja na Emmanuel Mabisa wakimtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji

Huu ni muendelezo wa masomo yanayofundishwa na John shabani, ili kukufanya unayetaka kujifunza kuimba, uwe mwanafunzi mzuri na yule mwimbaji awe bora zaidi.

Tahadhari: Usilazimishe kutumia nguvu ili uweze kuimba vizuri, kinyume chake jizoeshe kutumia nguvu kidogo lakini utaalam mwingi (Vocal Technique). Shida ni pale tunapodhani kwamba nguvu hizi ni kama za wanariadha au wacheza mieleka! Inawezekana nguvu hizi zisionekane kwa macho ya nyama lakini zinadhihirishwa na uimbaji wetu. Tunapoimba tunatakiwa kuwa na uhuru (freedom in singing), na sio kama mtu aliyelazimishwa. Lakini ikumbukwe pia nguvu hizi asili yake inatoka pia na mfumo wetu wa maisha ya kila siku iki pia ni pamoja na mazoezi ya viungo, vyakula na vinyaji tunavyotumia, makazi na malazi safi n.k.
Mazoezi mengi yanayofanyika kwenye vikundi mbalimbali, ni ya kupayuka na kutumia nguvu nyingi, matokeo yake watu wengi wamekaa kwenye zoezi hilo kwa muda mrefu bila kuwa na mabadiliko yoyote huku miili yao ikizoofika au kuishia kuwa mtu wa kupiga kelele na sio kujfunza kuimba vizuri. Haya sio mazoezi ya kumpata mshindi wa dansi mia mia, ni mazoezi ya kuimba. Imefika mahali sasa masikio hayawezi kujisikia vile tunavyoimba kwasababu ni kelele na kujichosha.
Ikumbukwe kuwa sauti hutunzwa kama yai; wengi wetu hufanyishwa mazoezi magumu yasiyolingana na umri wao na hali yao ya mfumo wa miili yao pamoja na kuzingatia afya zao, matokeo yake nimeshuhudia watu wakipata matatizo katika koo zao na hata bathi ya miili yao. 

Inashangaza kuona mtu ambaye hajawahi kukimbia maili moja unataka kumkimbiza maili kumi, matokeo yake ni kudondoka kama sio kupoteza fahamu kabisa. Yapo mazoezi ya kawaida ya jumla lakini mazoezi mengine ya uimbaji lazima yazingatie umri wa mtu, hali ya mtu huyo sambamba na afya yake. Nasikitika kusema kuwa wapo waliofundishwa kwamba akiweza kuimba noti za juu ndio amekuwa mwimbaji mzuri, matokeo yake mtu anatumia nguvu nyingi, kukaza misuli ya uso huku usoni akijaribu kuvimba na kutoa macho kama mjusi aliyebanwa na mlango ili tu awezekufika huko!...

Najua wapo waalimu wengi katika masomo haya ya uimbaji, na wengine inategemea amejifunza wapi, lakini bado mwisho wa siku ukweli unabaki kuwa ukweli. Mimi ningeshauri hata kama wewe ni mwalimu mzuri, mwimbaji mzuri, sote tubaki kuwa wanafunzi.

Kwa ushauri zaidi tupigie
0716560094, au  niandikie: touchingvoice@yahoo.com
Pia unaweza ukahudhuria masomo tunayofundisha sehemu mbalimbali.

12 October 2014

John Shabani - Mtoto wa Mfalme

11 October 2014

HATIMAYE CHAMA CHA WAJANE KIMEANZISHWA TANZANIA

Chama hicho kijulikanacho kwa jina la Chama cha Wajane Tanzania 
(Tanzania Widows Association - TAWIA)

lengo lake kuu ni kuwaweka wajane pamoja, ili kutambuana, kufahamiana, kujua changamoto mbalimbali anazopitia mjane, na kutafuta ufumbuzi wa kutatua changamoto hizo.  Ikiwemo kusomesha watoto, elimu ya sheria, afya, saikologia, biashara na ujasiriamali. Vilevile chama kitajihusisha na kutoa elimu kwa jamii juu ya mjane, iwatambue wajane, kuwapenda, kuwathamini na kuwasaidia kwa namna moja ama nyingine, pia kujitoa kwa hali na mali kusaidia kupambana na changamoto anazopitia mjane.
                                     Wajane wkieleza changamoto zinazowakabili

                                       Msaada wa nguo zilizotolewa na mfadhili


Pia chama kitasimamia sheria inayotetea haki za mjane Tanzania, ikiwemo hati ya mirathi na usimamizi wa mali za familia baada ya kifo cha mume wa mjane.  Hivyo chama hiki kitarejesha matumaini mapya kwa mjane, na wajane watarajiwa.  Pia kwa namna moja au nyingine, kujihusiha na haki za mgane na watoto walioachwa na wazazi (yatima).

Zipo changamoto nyingi zinazotokea pale mwanamke anapofiwa na mume wake. Huo kwake ndio wakati anaohitaji sana kupendwa na kutiwa moyo na jamii iliyobaki. Lakini kinyume chake, umekuwa ndio wakati wa kutengwa, kunyanyaswa na ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa wakaribu kabisa kabla ya kifo cha mume wake. Ikiwa ni pamoja na  kunyang’anywa mali zilizokuwa za familia, pamoja na kufukuzwa katika nyumba aliyokuwa akiishi na mume wake.  Mjane amekuwa mtu wa kuonewa na kuumizwa katika jamii, wengi wamenyanyasika kijinsia pamoja na kuathiriwa kabisa kisaikologia, na hata wengine kupoteza maisha, muda mfupi baada ya kufiwa na mume wake kutokana na mkandamizo na msongo wa mawazo.

Ikumbukwe kuwa Nchi mbalimbali duniani limeanzisha vyama vya aina hii. Kwasababu ya kuona changamoto anazopitia mjane, ndio maana tarehe 22/12/2010, Umoja wa Mataifa uliridhia kila ifikapo tarehe 23 mwezi wa sita, siku hiyo kuadhimishwa kama siku ya wajane duniani (Iternational Widows Day).

Hapa chini ni ujumbe wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa kuhusu siku ya wajane duniani:



Message from Ban Ki-moon, Secretary-General, United Nations
On International Widows’ Day, 23 June 2013

We commemorate the third International Widows’ Day for the hundreds of millions of women in the world who suffer exploitation, deprivation and exclusion when their husbands die. Today, we call for stronger action to end widespread discrimination against widows because no woman should lose her rights when she loses her husband.

Every human being has the right to live in dignity with equal rights and opportunities to realize their potential. Yet women and girls continue to face gender-based violence and discrimination, and this is the case for many widows around the world.

Many widows are denied their rights—from being evicted from their homes because they cannot inherit property or the land they live on to being forced into exploitative and risky sex work to support themselves and their families because they have no income and nowhere else to turn.
An estimated 115 million widows are currently living in poverty, and 81 million have suffered physical abuse, some from members of their own family. Adolescent girls, many of whom have been married off too early to much older men, are at great risk with very little protection.
It is our collective duty to ensure that widows of all ages and their children are treated as full and equal citizens, with equal opportunities for education, participation in the economy and decision-making, and a healthy life free of violence and discrimination.

We must recognize the role of widows as not only victims of poverty, conflict and natural disasters but as peace-builders and re-builders of families, communities and societies. National laws and policies that protect and promote the rights of widows should be guided by the Convention on the Elimination of Discrimination against Women and the Convention of the Rights of the Child.

UN Women works in partnership with governments and with the private sector, to support the economic empowerment of widows in Asia, Africa and Latin America.

Moja ya mambo ambayo chama kimeanza kuyatekeleza mapema tu baada ya kusaidiwa kupata ofisi ya muda, ni mafunzo mbalimbali yanayotolewa bure kwa wajane na watoto wao. 

Mafunzo hayo ni pamoja na kujifunza kompyuta, ushonaji, lugha, mapishi, ujasiriamali n.k. Mafunzo hayo yanatolewa bure hapohapo ofisini. Pia wajane wenye mahitaji madogomadogo kama mavazi na chakula wamekuwa wakisaidika mara moja. Pia mkakati wa watoto wa wajane kupata elimu bora ni moja ya malengo ya chama.



Chama kinawashukuru watu ambao wamejiguswa na changamoto za ujane na kukubali kujitolea kusaidia. Pia uongozi wa chama unawashukuru wale wote wanaoendelea kutoa ushauri wao ili kukiboresha, pamoja na wale wote wanaoendelea kupongeza wazo hili la kuanzisha Chama cha Wajane Tanzania.

Ili kufahamu mengi kuhusu Chama cha Wajane Tanzania, au labda ungependa kutoa mchango wako wa hali na mali, ushauri, au wewe ni mjane, mgane, mtoto wa mjane au una ndugu, jamaa na rafiki wa aina hii, unaweza kuwasiliana na uongozi kwa simu namba 0716 214 680/0754 366 530, pia unaweza ukatembelea ukurasa wa facebook wenye jina “Tanzania Widows Association”

Umoja wetu ndio mafanikio yetu!

 


3 October 2014

PONGEZI KWA MILCA KAKETE KWA KUSHINDA TUZO



 Huyu ndiye Milcah Kakete, mwanamama anayetuwakilisha vyema kwa nyimbo nzuri za injili


Pichani ni Milca Kakete akiwa na tuzo aliyoshinda ya best artist of 2014 ya African Gospel Music Contest. Video ya wimbo wa Nakung'ang'ania ndio uliompa ushindi 

Naungana na wapenzi wote wa nyimbo za Injili, kumpongeza  Milca Kakete kwa kushinda tuzo kwenye Africa Gospel Music Contest iliyofanyikia kwenye jiji la Washington DC, USA. Huyu ni kati ya wapeperusha bendera ya Tanzania ambaye mchango wake wa kuutangaza Muziki wa Injili Tanzania tunauona. Na zaidi tuzidi kumuombea kwani ana project nzuri sana zinakuja kwa utukufu wa Bwana.

John Shabani na upngozi mzima wa blogu hii, 
watanzania na Afrika tunakupongeza sana!

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP