29 November 2012
TAMASHAS LA VICTOR ARON KUTIKISA DAR ES SALAA
11:57
No comments
Kutoka
kuwa mvuvi wa migebuka na dagaa hadi kuwa mvuvi wa watu, ni Victor Aron, kijana
kutoka mwisho wa reli kigoma mwimbaji huyo wa nyimbo za injili Tanzania
na Afrika Mashariki, anakuomba usikose katika uzinduzi wa albamu yake ya KANUNI
katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B Assemblies of God kuanzia saa
9:00 mchana na hakutakuwa na kiingilio siku hiyo ya tarehe 2/12/2012.
Unaweza
kujipatia tshirts ambazo unaweza kuvaa wakati wa uzinduzi wake na siku
zingine za kawaida, kwani kuvaa hizi tshirts unafanyika BANGO la Yesu.
Zinapatika kwa Victor Aron Praise Power Radio Mikocheni B Aseemblies of God na
ofisi ya RUMAFRICA sinza Afrikasana Sokoni hapa jijini Dar es Salaam.
19 November 2012
MUHUBIRI WA KIMATAIFA KUTIKISA DAR ES SALAAM
07:35
No comments
Maelfu duniani wameponywa na kufunguliwa kupitia huduma ya Dr. G. Kamese. Huu ni wakati wako, maliza mwaka na neema ya ki-Mungu.
Karibu sana
Karibu sana
18 November 2012
MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WATOA SEMINA KWA WASANII
09:07
No comments
Meneja wa LAPF akiongelea faida za kujiunga na mfuko huo
Mfanyakazi wa LAPF akiwamakini kuandika maswali ya wasanii
Nahibu katibu mwenezi wa chama cha muziki wa injili bwana John Shabani akitoa mchango wake katika kuboresha maisha ya wasanii nchini
Waandishi wa habari hawakuwa mbali kurekodi matukio
Mgao wa kalenda za LAPF
Katibu wa shirikisho la muziki Tanzania akichangia jambo.
Wasanii wakijaza famu za kujiunga na mfuko huo
Mfuko
wa pensheni wa LAPF, watoa semina kwa wasanii ili waweze kujiunga na mfuko huo
na kufaidika na pensheni mbalimbali kwa maisha yao yasasa na ya baadaye.
Mafao
yanayotolewa na LAPF ni: Pensheni ya uzee, pensheni ya urithi, pensheni ya
ulemavu, mafao ya uzazi, mafao ya mazishi, mikopo ya nyumba pamoja na mikopo ya
wanachama kupitia saccos.
Kikao
hicho cha aina yake kimefanyika katika majengo ya LAPF MILLENIUM TOWER kijitonyama Dar es salaam, katika ukumbi wa
mikutano gorofa ya nane.
Mengi
yamezungumzwa na pia viongozi wa vyama mbalimbali vya wasanii wakiwemo wa
nyimbi za injili, walipata fursa ya kuuliza maswali na baada ya hapo tukio la
kujaza fomu za kujiunga na mfuko huo
liliendelea.
Kikao
hicho kimedhuriwa na viongozi na wawakilishi wa vyama hai vinavyounda
shirikisho la muziki Tanzania.
Baadhi
ya mapendekezo yaliyotolewa na wasanii, ni kuangalia suala suala la matibabu
pamoja na kujegewa nyumba za wasanii ili waendelee kulipia taratibu na baadaye
kuwa wamiliki halali wa nyumba hizo.
16 November 2012
MKUTANO MKUBWA WA INJILI KUTIKISA DAR ES SALAAM
09:17
No comments
Dr. Godfrey Kamese na timu ya wahubiri wa kimataifa kuwasha moto katika Jiji la Dar es salaam.
Mtumishi huyo wa Mungu raia wa uganda, amekua akizunguka duniani kote akihubiri habari njema za Bwana Yesu na kuwafungua maelfu ya watu waliofungwa na nguvu za giza.
Mkutano huo wa kiamataifa utafanyika katika viwanja vya Biafra Dar es salaam, kuanzia tarehe 5 hadi 9 Decemba. Waimbaji mbalimbali wa kimataifa wataimba. Endelea kufuatilia mengi kuhusu mkutano huo kupitia blog hii.
ZIARA NA MIKUTANO MBALIMBALI YA KIMATAIFA
Jipange kuhudhuria
15 November 2012
MWANADADA SARAH SHILLA KUFANYA KWELI KATIKA MUZIKI WA INJILI.
23:16
No comments
Kwa wapenzi wa muziki wa injili, Jina la sarah shilla
siogeni masikioni. Pamoja na kuwa busy na mosomo huko India lakini suala la
kumtukuza mwenyezi Mungu amelipa kipaumbele kuliko kawaida. Akifanya maojiano
hivi karibuni na mmiliki wa blogu hii, amefunguka kwa mambo mengi.
Mahijiano yalikuwa hivi:
Sarah
Shilla :Kaka John
Shabani Bwana Yesu asifiwe
John Shabani: Amen,
za huko india, vipi kuhusu masomo yako na huduma ya kumtukuza Bwana Yesu?
Sarah: Hakika namshukuru Mungu wangu, kilakukicha ananipa
hatua mpya.
·
John Shabani :Tell me some few things:
ningetaka kufahamu kuhusu hawa walioshiriki kwenye video, je ni wabongo?
Uliorganize vipi kuwapata? Kampuni iliyoshoot, nani aliyekuwezesha. Unamikakati
gani ki-huduma, ki-elimu na kazi.
5:36pm
Sarah
Shilla :Well hawa ni wanafunzi wenzangu
baadhi wakutoka burundi lesotho zimbabwe uganda ambao wapo huku. Video
imefanywa na company inayofanya bollyhood movies huku india inaitwa kamal studio.
Video nilitumia hela nilizokua nafanya savings becuse nilitaka iwe suprise kwa wazazi wangu pia. Nina mialiko kadhaa ambazo nitazifanya nxt year kama tours ambao ni swaziland, south africa, zimbabwe na zambia na baada ya hapo nitarud kenya na uganda
Ingawa nikimaliza shule nitafanya huduma kwenye baadhi ya mikoa ya Tanzania
Nakushirikiana na waimbaj mbali mbali wa injili becsuse kaz ya Mungu nikufanya kwa pamoja
Video nilitumia hela nilizokua nafanya savings becuse nilitaka iwe suprise kwa wazazi wangu pia. Nina mialiko kadhaa ambazo nitazifanya nxt year kama tours ambao ni swaziland, south africa, zimbabwe na zambia na baada ya hapo nitarud kenya na uganda
Ingawa nikimaliza shule nitafanya huduma kwenye baadhi ya mikoa ya Tanzania
Nakushirikiana na waimbaj mbali mbali wa injili becsuse kaz ya Mungu nikufanya kwa pamoja
John
Shabani :Umefanyia shooting kanisani au
ukumbini, panaitwa je? Unatenga vipi muda wa shule na huduma? Ukiwa india
unasali dhehebu gani?
6:13pm
Sarah
Shilla :Nilifanyia. Mandhari tofauti
kanisa la CNI church hulu nasali pentecoste church linaitwa adonia church
ambapo na fanya huduma mbali mbali.
Picha mbalimbali za maandilizi ya video hiyo:
Endelea kumwombea!
12 November 2012
MWANADADA ROSE MUHANDO KUJA KIVINGINE
09:12
No comments
Kama uonavyo Rose akiwa katika pozi tofauti, ndivyo alivyoamua kufanya mageuzi katika huduma yake. Rose ambaye kwasasa ameanza kwa kuwa na blog itakayomtangaza zaidi kimataifa na itakayokuwa na mambo mengi ya kuujenga ufalme wa Mungu, Pia ameanza mchakato wa kuwa na taasisi itakayo saidia vijana, wanawake waliotelekezwa na waume zao, yatima, wajane na watu wenye ulemavu.
Kwa habari zaidi kuhusu Rose muhando na ujio mpya, endelea kutembelea blogu hii au www.rumaafrica.blogspot.com.
Kwa habari zaidi kuhusu Rose muhando na ujio mpya, endelea kutembelea blogu hii au www.rumaafrica.blogspot.com.
6 November 2012
JOHN SHABANI KUZURU UBELJIJI (BELGIUM) - ULAYA, NI MWALIKO WA KUSHIRIKI ALBUM YA INJILI
23:29
No comments
John akiwa na Josiane
Baada ya kumshirikisha katika album yake mpya mwanadada
wa kitanzania Josiane na kundi lake la Destiny sisters, mwanadada huyo anayeishi
huko Ubeljiji kwa sasa, ameguswa na huduma ya John, na kuamua kumshirikisha
katika baadhi ya nyimbo zake. Josiane amepata shavu ya kurekodi nyimbo zake baada
ya promota mmoja kuridhika na kiwango kizuri cha uimbaji cha mwanadada huyu..
Josiane aliguswa sana na wimbo alioshirikishwa na John Shabani na pia baada ya
John kutumia gharama kubwa kumleta mwanadada huyo
kutoka ulaya ili kuja
kushiriki katika mkanda wa video.
Albam hiyo mpya ya John Shabani inatarajiwa kukamilika
mwishoni mwa mwezi huu. Kuchelewa kutoka kwa video hiyo ya mwalimu wa muziki wa
injili afrika mashariki, ni kutokana albam hiyo kushirikishwa waimbaji wengi
hivyo kugharimu pesa nyingi na wakati mwingine imekuwa ni vigumu kuwapata
waimbaji hao kiurahisi. Inakisiwa takribani shilingi miliono saba (Tsh 7000.000)
kutumika katika kugharimia nyimbo hizo kwa maana ya audio na video.
Baadhi ya waimbaji walioshiriki katika album hiyo mpya
ya John Shabani ni:
Mzee Cosmas Chidumule, Upendo Kilahiro, Faraja Ntaboba,
Destiny Sisters, Bella kombo, Jane Misso, Christina mwang’onda, John Komanya,
Children of praise na wengine kibao.
Baadhi ya picha katika maandalizi ya mkanda wa video
John na Christina Mwang'onda
John, John Komanya bna Upendo Kilahiro
John na Comas Chidumule
John na Faraja Ntaboba
John na Childern of praise
John na Destiny Sisters
Subscribe to:
Posts (Atom)