Pages

29 November 2012

TAMASHAS LA VICTOR ARON KUTIKISA DAR ES SALAA


 
Kutoka kuwa mvuvi wa migebuka na dagaa hadi kuwa mvuvi wa watu, ni Victor Aron, kijana kutoka mwisho wa reli kigoma mwimbaji  huyo wa nyimbo za injili Tanzania na Afrika Mashariki, anakuomba usikose katika uzinduzi wa albamu yake ya KANUNI katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B Assemblies of God kuanzia saa 9:00 mchana na hakutakuwa na kiingilio siku hiyo ya tarehe 2/12/2012.

Unaweza kujipatia  tshirts ambazo unaweza kuvaa wakati wa uzinduzi wake na siku zingine za kawaida, kwani kuvaa hizi tshirts unafanyika BANGO la Yesu. Zinapatika kwa Victor Aron Praise Power Radio Mikocheni B Aseemblies of God na ofisi ya RUMAFRICA sinza Afrikasana Sokoni hapa jijini Dar es Salaam.

19 November 2012

MUHUBIRI WA KIMATAIFA KUTIKISA DAR ES SALAAM

Maelfu duniani wameponywa na kufunguliwa kupitia huduma ya Dr. G. Kamese. Huu ni wakati wako, maliza mwaka na neema ya ki-Mungu.
Karibu sana

18 November 2012

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WATOA SEMINA KWA WASANII




 Meneja wa LAPF akiongelea faida za kujiunga na  mfuko huo
 Mfanyakazi wa LAPF akiwamakini kuandika maswali ya wasanii
 Nahibu katibu mwenezi wa chama cha muziki wa injili bwana John Shabani akitoa mchango wake katika kuboresha maisha ya wasanii nchini


 Waandishi wa habari hawakuwa mbali kurekodi matukio
 Mgao wa kalenda za LAPF
 Katibu wa shirikisho la muziki Tanzania akichangia jambo.
 Wasanii wakijaza famu za kujiunga na mfuko huo
Mfuko wa pensheni wa LAPF, watoa semina kwa wasanii ili waweze kujiunga na mfuko huo na kufaidika na pensheni mbalimbali kwa maisha yao yasasa na ya baadaye.

Mafao yanayotolewa na LAPF ni: Pensheni ya uzee, pensheni ya urithi, pensheni ya ulemavu, mafao ya uzazi, mafao ya mazishi, mikopo ya nyumba pamoja na mikopo ya wanachama kupitia saccos.

Kikao hicho cha aina yake kimefanyika katika majengo ya LAPF MILLENIUM TOWER  kijitonyama Dar es salaam, katika ukumbi wa mikutano gorofa ya nane.

Mengi yamezungumzwa na pia viongozi wa vyama mbalimbali vya wasanii wakiwemo wa nyimbi za injili, walipata fursa ya kuuliza maswali na baada ya hapo tukio la kujaza fomu za kujiunga na  mfuko huo liliendelea.

Kikao hicho kimedhuriwa na viongozi na wawakilishi wa vyama hai vinavyounda shirikisho la muziki Tanzania.

Baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na wasanii, ni kuangalia suala suala la matibabu pamoja na kujegewa nyumba za wasanii ili waendelee kulipia taratibu na baadaye kuwa wamiliki halali wa nyumba hizo.

16 November 2012

MKUTANO MKUBWA WA INJILI KUTIKISA DAR ES SALAAM






Dr. Godfrey Kamese na timu ya wahubiri wa kimataifa  kuwasha moto katika Jiji la Dar es salaam.
Mtumishi huyo wa Mungu raia wa uganda, amekua akizunguka duniani kote akihubiri habari njema za Bwana Yesu na kuwafungua maelfu ya watu waliofungwa na nguvu za giza.


Mkutano huo wa kiamataifa utafanyika katika viwanja vya Biafra Dar es salaam, kuanzia tarehe 5 hadi 9 Decemba. Waimbaji mbalimbali wa kimataifa wataimba. Endelea kufuatilia mengi kuhusu mkutano huo kupitia blog hii.

 ZIARA  NA MIKUTANO MBALIMBALI YA KIMATAIFA

Jipange kuhudhuria

15 November 2012

MWANADADA SARAH SHILLA KUFANYA KWELI KATIKA MUZIKI WA INJILI.





Kwa wapenzi wa muziki wa injili, Jina la sarah shilla siogeni masikioni. Pamoja na kuwa busy na mosomo huko India lakini suala la kumtukuza mwenyezi Mungu amelipa kipaumbele kuliko kawaida. Akifanya maojiano hivi karibuni na mmiliki wa blogu hii, amefunguka kwa mambo mengi.
Mahijiano yalikuwa hivi:
Sarah Shilla  :Kaka John Shabani Bwana Yesu asifiwe
John Shabani:  Amen, za huko india, vipi kuhusu masomo yako na huduma ya kumtukuza Bwana Yesu?
Sarah: Hakika namshukuru Mungu wangu, kilakukicha ananipa hatua mpya.

·  John Shabani :Tell me some few things: ningetaka kufahamu kuhusu hawa walioshiriki kwenye video, je ni wabongo? Uliorganize vipi kuwapata? Kampuni iliyoshoot, nani aliyekuwezesha. Unamikakati gani ki-huduma, ki-elimu na kazi.

5:36pm
Sarah Shilla :Well hawa ni wanafunzi wenzangu baadhi wakutoka burundi lesotho zimbabwe uganda ambao wapo huku. Video imefanywa na company inayofanya bollyhood movies huku india inaitwa kamal studio.
Video nilitumia hela nilizokua nafanya savings becuse nilitaka iwe suprise kwa wazazi wangu pia. Nina mialiko kadhaa ambazo nitazifanya nxt year kama tours ambao ni swaziland, south africa, zimbabwe na zambia na baada ya hapo nitarud kenya na uganda
Ingawa nikimaliza shule nitafanya huduma kwenye baadhi ya mikoa ya Tanzania
Nakushirikiana na waimbaj mbali mbali wa injili becsuse kaz ya Mungu nikufanya kwa pamoja
http://static.ak.fbcdn.net/rsrc.php/v2/y4/r/-PAXP-deijE.gif6:06pm
John Shabani :Umefanyia shooting kanisani au ukumbini, panaitwa je? Unatenga vipi muda wa shule na huduma? Ukiwa india unasali dhehebu gani?
6:13pm
Sarah Shilla :Nilifanyia. Mandhari tofauti kanisa la CNI church hulu nasali pentecoste church linaitwa adonia church ambapo na fanya huduma mbali mbali.

Picha mbalimbali za maandilizi ya video hiyo:




Endelea kumwombea!

12 November 2012

MWANADADA ROSE MUHANDO KUJA KIVINGINE

Kama uonavyo Rose akiwa katika pozi tofauti, ndivyo alivyoamua kufanya mageuzi katika huduma yake. Rose ambaye kwasasa ameanza kwa kuwa na blog itakayomtangaza zaidi kimataifa na itakayokuwa na mambo mengi ya kuujenga ufalme wa Mungu, Pia ameanza mchakato wa kuwa na taasisi itakayo saidia vijana, wanawake waliotelekezwa na waume zao, yatima, wajane na watu wenye ulemavu.

Kwa habari zaidi kuhusu Rose muhando na ujio mpya, endelea kutembelea blogu hii au www.rumaafrica.blogspot.com.

6 November 2012

JOHN SHABANI KUZURU UBELJIJI (BELGIUM) - ULAYA, NI MWALIKO WA KUSHIRIKI ALBUM YA INJILI




                                     John akiwa na Josiane

 Kundi la Destiny Sister
 
Baada ya kumshirikisha katika album yake mpya mwanadada wa kitanzania Josiane na kundi lake la Destiny sisters, mwanadada huyo anayeishi huko Ubeljiji kwa sasa, ameguswa na huduma ya John, na kuamua kumshirikisha katika baadhi ya nyimbo zake. Josiane amepata shavu ya kurekodi nyimbo zake baada ya promota mmoja kuridhika na kiwango kizuri cha uimbaji cha mwanadada huyu.. Josiane aliguswa sana na wimbo alioshirikishwa na John Shabani na pia baada ya John kutumia gharama kubwa kumleta mwanadada huyo 

kutoka ulaya ili kuja kushiriki katika mkanda wa video.
Albam hiyo mpya ya John Shabani inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu. Kuchelewa kutoka kwa video hiyo ya mwalimu wa muziki wa injili afrika mashariki, ni kutokana albam hiyo kushirikishwa waimbaji wengi hivyo kugharimu pesa nyingi na wakati mwingine imekuwa ni vigumu kuwapata waimbaji hao kiurahisi. Inakisiwa takribani shilingi miliono saba (Tsh 7000.000) kutumika katika kugharimia nyimbo hizo kwa maana ya audio na video.

Baadhi ya waimbaji walioshiriki katika album hiyo mpya ya John Shabani ni:
Mzee Cosmas Chidumule, Upendo Kilahiro, Faraja Ntaboba, Destiny Sisters, Bella kombo, Jane Misso, Christina mwang’onda, John Komanya, Children of praise na wengine kibao.

Baadhi ya picha katika maandalizi ya mkanda wa video


 John na Christina Mwang'onda
 John, John Komanya bna Upendo Kilahiro
 John na Comas Chidumule
 John na Faraja Ntaboba

 John na Childern of praise
 John na Destiny Sisters