Pages

8 May 2014

Michelle Obama aunga mkono kampeni ya kuwarudisha wanafunzi wa kike waliotekwa huko Nigeria – “Bring back our girls”



Michelle Obama akiwa ameshikilia bango akiungana na dunia katika kampeni ya kuwarudisha wanafunzi waliotekwa huko Nigeria


 Mamia ya watu nnje ya ubalozi wa Nigeria huko Marekani, wakilalamikia serikali kutokuongeza bidii katika kuhakikisha wanafunzi wa kike waliotekwa wamerudishwa salama


 




Moja ya kati ya habari kubwa dunia, ni ile ya kutekwa kwa wanafunzi huko Nigeria baada shule ya mabweni ya wasichana kushambuliwa katika jimbo la Borno Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo huku wasichana wakitekwa nyara.
Wazazi wanasema kuwa zaidi ya wasichana miambili wametekwa nyara na washambuliaji hao. Kampeni hiyo ikiambatana na maandamano imefanyika karibu nchi mbalimbali duniani.
Taarifa zinazohusiana
Washambuliaji wanaaminika kuwa wanachama wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram. Utekaji nyara huo ulifanyika usiku wa manane katika shule ya Chibok Kusini mwa mji wa Borno , karibu na mpaka na Cameroon.
Inaarifiwa wasichana 300 walikuwa wanajiandaa kwa mitihani yao. Mmoja wa wasichana alifanikiwa kutoroka na aliambia BBC kuwa walikuwa wanalala wakati walipovamiwa na wanaume waliokuwa wamejihami.
Waliowashambulia wanaaminika kuwa wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Wanaume hao waliingiza magunia ya chakula katika malori yaona kuwaamuru wasichana kupanda lori hizo.
Wasichana 15 walifanikiwa kutoroka baada ya lori walimokuwa kukumbwa na hitilafu.
Wakazi wa kijiji cha Chibok wanasema kuwa walisikia milipuko kadhaa huku nyumba 170 zikiteketezwa.
Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa wanajeshi wawili waliuawa huku mali ikiharibiwa wakati wa shamblizi hilo mjini Chibok.

Ni wito wetu kuunga mkono kampeni hii na zaidi kumuomba Mungu ayanusuru maisha ya wanafuzi hao. 

Mungu ibariki Nigeria, 
Mungu ibariki Afrika, 
Mungu inusuru Dunia na matukio ya kutisha!

No comments:

Post a Comment