Mkutano wa waimbaji,wanamuziki na wadu wa
muziki wa Injili uliofanyika mwaka juzi katika hoteli ya wanyama iliyopo Sinza,
Dar. Kongamano hilo lilikua lilifadhiliwa na mfuko wa jamii NSSF
Ziara ya uongozi wa chama cha muziki wa Injili na wadau wengine, kuwatembelea watoto yatima huko mkuranga
Uongozi wa chama cha muziki wa Injili walipomtembelea mzee Makasy
Ziara ya kuhamasisha chama mikoani
Uongozi wa chama cha muziki wa injili wakimpongeza Bw. Msama
Mmoja wa wanachama, Bw. Magida Timotheo akiwa ameshikilia katiba ya chama
Moja ya sababu za msingi kutuweka pamoja
waimbaji na wanamuziki wa injili, ili tuwe na sauti moja katika kutetea na
kusimamia haki za waimbaji/wanamuziki na kila anayehusika na muziki wa injili
nchini na pia ni agizo la serikali kwamba, waliona kwa sababu muziki wa injili
unauzwa dukani kama miziki mingine kwa hiyo kitu chochote kikishauzwa dukani
lazima kiwe na sheria zake na kikishakuwa na sheria zake lazima kiwe na haki na
wale wanaofanya zile kazi wawezekujua faida zake na wawezekufaidika na zile
kazi zao
Pia ni kwamba baada ya
kuona sanaa ya muziki inakua kwa kasi hivyo ikaonekana kuna umuhimu wa kuwepo
na shirikisho la muziki Tanzania kama vile ilivyo shirikisho la mpira (TFF).
Hivyo basi shirikisho hilo lianundwa na vyama vilivyosajiliwa. Najua vipo
vikundi vingi vinavyounda umoja wa waimbaji kutoka makundi ya aina fulani ya
muziki, lakini ukweli ni kwamba, vyama vya muziki vinavyotambuliwa na serikali
ni vile vilivyosajiliwa kihalali na kupewa kibali kupitia Basata (Baraza la
sanaa la taifa), na moja kati ya vyama vyenye kibali cha serikali ni chama cha
muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) chenye usajili: BST 4598 . Najua waimbaji wa injili nchini wakiwemo
wanamuziki, maproducer na wapenzi wa nyimbo za injili wanaweza kuwa na maswali
mengi kuhusu chama hiki, pia kuwepo na hali ya kusitasita kujiunga, lakini huko
tunakoelekea kuna watu watajua umuhimu wa kujiunga na chama. Si vibaya kuhoji,
lakini ipo katiba inayotambulika na serikali, hivyo basi ni wajibu wa kila
mwanachama hai kuwa na nakala ya katiba hiyo.
Ni wito wangu kwa kila mtu anayehusika na
muziki wa injili Tanzania, uwe mwimbaji, mwanamuziki, mwinjilisti, mchungaji,
producer, Mc na mpenzi wa muziki wa injili, kujiunga na chama na kuwa na
kitambulisho chake halali kama mwanachama wa muziki wa injili Tanzania. Lakini
pia ikumbukwe jambo peekee alilolisema yesu muda mfupi kabla hajapaa mbinguni,
aliagiza upendo. Hivyo sioni sababu ya waimbaji kutokuwa wamoja,
kutokupendanda, kuweka matabaka, kutokubebana na kuinuana. Ebu tuamke,
tusiishie kuandaa matamasha ya kujipatia pesa, lakini tusimame katika agizo kuu
la kuwaleta watu kwa Yesu. Tunaweza kabisa kuandaa mikutano mikubwa ya injili
na makongamano, tunaweza kabisa kutenga muda wa kufunga na kuomba pamoja; na
huu ndio wakati, tusisubiri kusikia tu habari mbaya za mpendwa mwezetu na
kuzishabikia, tumeagizwa upendao!
Chama cha Muziki wa Injili kilianzishwa
mwaka 2011,Uongozi wa chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Mwenyekiti ni Addo November, katibu anayekaimu ni John Shabani,katibu mwenezi ni Stella Joel,Mwekahazina ni Upendo Kilahilo.. Idadi ya wanachama
waliojiunga kwa Dar es Salaam wanakaribia kuwa elfu nane, Morogoro na Pwani ni
mia tatu na Arusha na Kilamanjaro viongozi ndo wanahamasisha wanachama kujiunga
...Tuna kanda kama nne ambazo zinaviongozi kanda ya kaskazini inayojumuisha
Tanga,Kilimanjaro,Arusha na Manyara mwkt ni Samweli Nungwana katibu ni Anne
Annie,Morogoro na Pwani kiongozi ni Ester
mwamboma na wengine,Kanda ya ziwa kiongozi ni Jacob Mutashi na Kanda kusini pia wapo viongozi wao. Jinsi ya
kujiunga kwenye chama cha muziki wa injili kuna Ada ya uanachama utajiandikisha
kwa Tsh 20000/= na utatengeneza kitambulisho kizuri kwa Tsh 10000/= kwa hiyo ni
muhimu sana waimbaji na wanamuziki wa injili Tanzania wakajiunga kama unavyojua
mwanachama hai ni yule anaelipa Ada ya kila mwaka, ukishalipa ada unakuwa na
sauti ndani ya chama unakuchagua au kuchaguliwa na unaweza kufaidika na faida
zote zinazotokana na Chama cha Muziki Wa Injili Tanzania.
No comments:
Post a Comment