Katika kikao hicho Mh. Januari Makamba aliweza kutoa hutuba ndefu yenye ufasaha
kwa wanamuziki wa Injili Tanzania. Hotuba yake ilikuwa na matumaini kwa
wanamuziki na iliweza kuwafurahisha sana wanamuziki hawa hasa pale alipoweza
kutoa ahadi zake za kukisaidia Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania ikiwemo kuwaahidi kuchangia katika kufanikisha zoezi la kuwa na
Channel ya TV ya waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, kuwa na studio ya kisasa itakayomilikiwa na chama cha muziki Tanzania, kufikia suala la kupata eneo la kuendeshea shughuli zao n.k. Aliomba sana wanamuziki
kuwa na nguvu za bidii za kuweza kufanikisha yale yote yanayowazunguka na
wasibweteke wakisubiria, na pia wanamuziki wa injili wanategemewa kuwa kioo na mfano wa kuigwa, hivyo wawe na nidhamu na uchaji wa Mungu na kujiepusha na skendo, maana nyimbo za injili zinapendwa na kila mtu hata wapagani na wale wa dini zingine. Pia ameahidi kutekeleza ahadi zake haraka iwezekanavyo
Wadau wa muziki wa Injili wakiwa kwenye mkutano huo.
Katibu wa Shirikisho la Muziki wa Injili John Shaban
akiendesha mkutano.
Kiongozi wa mtandao wa wanamuziki Tanzania, mzee John Kitime
George Mpella akiwakilisha vyombo vya habari vya kiristo
Kutoka TRA
Ofisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA, Doreen Sinare (kulia), akitoa
ufafanuzi wa masuala mbalimba kwa wadau wa muziki wa Injili. Wa pli kulia ni
Muimbaji wa nyimbo za Injili, Christina Shusho.
Watu mbali mbali wakiuliza maswali
Rais wa Shirikisho la Muziki wa Injili Tanzania (TAF), Ado
Novemba (kushoto), akizungumza na wadau wa Muziki wa Injili Tanzania
Hoteli ya Wanyama Sinza Dar es Salaam kabla ya kumakribisha mgeni rasmi wa
mkutanmo huo, Mhe. January Makamba.
Balozi mstaafu, Profesa Coster Mahalu akizungumza na wadau
wa muziki wa nyimbo za Injili. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Kinondoni Revival
Choir, Dk. Jotham Mackenzie
Wadau wa muziki wakiwa kwenye mkutano huo wakifuatiliamambo
mbalimbali.
Wadau wa muziki wakiwa kwenye mkutano huo.
Wawakilishi wa ATN (Agape Television Network)
Kiongozi CHAMUITA kutoka Morogoro akikabidhi MIC
baada ya kujitambulisha
Muwakilishi kutoka ATN akijitambulisha
John Shabani akihakikisha kila kitu kinakaa sawa
Wadau wa eneo la usambazaji wa kazi za wanamuziki
wakiwa kwenye mkutano huo
Mwanahabari wa Kituo cha TV 1, Gervas Mwaitebela naye
alikuwepo kupata taarifa za mkutano huo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Mhe.
January Makamba (kulia), akizungumza na wadau wa Muziki wa Injili Tanaznia
Hoteli ya Wanyama Sinza Dar es Salaam leo.