CHAMUITA ni Chama cha Muziki wa Injili Tanzania ambacho kinasimamia haki za
mwanamuziki wa Injili Tanzania nzima. Chama hiki chenye malengo mazuri ya
kuhakikisha mwanamuziki hatokwi na machozi kwa kuonewa kupata kile
alichotarajia kukipata kutokana na jasho lake la kumtumikia Mungu kwa njia ya
muziki.
Mwanachama wa chama hiki ni yule tu aliyejiunga na chama hiki cha CHAMUITA na kupata kitambulisho halali kutoka kwa viongozi wa Chamuita.
CHAMUITA Imegawanyika katika kanda mbalimbali kama vile Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Mashariki na Pwana, Kanda ya kusini. Na kila kanda kuna uongozi ulioteuliwa na viongozi kutoka makao makuu ambayo yako jijini Dar es Salaam. Wanachama kutoka kanda hizo wana haki ya kujadilki yale yanowahusu wakishirikiana na uongozi wa juu kutoka makao makuu ya CHAMUITA.
Leo hii tunataka kukuletea baadhi ya picha za viongozi wa kanda ya kaskazini wa CHAMUITA waliofaya vikao vyao vya kanda kwa lengo la kulinda haki za mwanamuziki na mambo mengi yanayowahusu katika kanda yao.
Kikao hiki kilifanyika katika ukumbi wa Kimalia kikiwa na lengo la kuwafikia wanamuziki wa kada mbalimbali katika mikoa minne ya kanda ya kaskazini yaani Tanga, Arusha na Manyara, kupanga siku ya kukutana na kuweka wakfu Chama Cha Muziki wa Injili Kanda ya Kaskazini mwezi wa 10, 2014 katika uwanja wa Obedi. Na sasa wapo mbioni kuongea na mgeni rasmi kutoka serikalini na Baba wa Kiroho kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment